Joe Biden apewa chanjo ya COVID19

Joe Biden apewa chanjo ya COVID19

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Rais mteule wa Marekani Joe Biden jana Jumatatu amepokea chanjo dhidi ya virusi vya corona wakati akitazamwa moja kwa moja kwenye televisheni ili kushawishi wamarekani kuwa zoezi hilo ni salama.

Kabla ya kupokea chanjo hiyo, Biden alionekana akijiandaa na kisha kumweleza muuguzi kuendelea na shuguli wakati akiwa kwenye hospitali moja mjini Newark, Delaware.

Mkewe Jill Biden saa kadhaa kabla pia alipokea chanjo kwenye hospitali hiyo ambayo iko karibu na kwao nyumbani.

Baadhi ya viongozi wengine mashuhuri wa Marekani waliopokea chanjo hiyo tayari ni pamoja na makamu wa rais Mike Pence, spika wa bunge Nancy Pelosi na kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la senate Mitch McConnell.

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye mwezi Oktoba alipatikana kuwa na virusi vya corona kufikia sasa hajasema ni lini amepanga kuipokea.

Marekani inaongoza ulimwenguni kwenye idadi ya maambukizi huku tayari ikiwa imeshuhudia zaidi ya vifo 318,000 kutokana na Covid-19 kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins.
 
Trump yeye ni mbishiiii na mtu wa League na hapendi kufanya mambo ambayo wengine pia wamefanya.

Ingawa kashasema kwamba Chanjo ni Juhudi za utawala wake lakini Kwasababu kaona Democratic wameanza kuchukua, yeye atakataa na kuanza kuipinga!
 
Kama lengo la chanjo ni kuamsha kingamwili dhidi ya aina fulani ya kimelea cha magonjwa, hawa ambao wameshapata maambukizi tayari wakapona kuna umuhimu gani wa kuchoma ilhali kinga zimeshatengenezwa?

Ama hii chanjo ya kirusi ni tofauti na zile za aina nyingine ya vimelea.
 
Kirusi kina uwezo wa kufanya mutation au kujibadilisha kuwa variant tofauti kisichoathiriwa na mfumo wa awali wa kinga ya mwili. Halafu ugonjwa huu hausababishwi na kirusi cha korona cha aina moja tu.
 
Actually, huo si mpango wa leo wala jana. The world's bourgeoisies have been dreaming of a pandemic of world class kama huu tangu kitambo tu. Malengo yao ya kuiweka dunia pamoja kimfumo bado yangali palepale.
 
Kirusi kina uwezo wa kufanya mutation au kujibadilisha kuwa variant tofauti kisichoathiriwa na mfumo wa awali wa kinga ya mwili. Halafu ugonjwa huu hausababishwi na kirusi cha korona cha aina moja tu.
Kwa maana hiyo chanjo hii haitatosha kumfanya mtu asiambukizwe, maana inaenda kuufanya mwili utengeneze kinga ya kirusi ambacho huenda kikabadilika. Ama chanjo hii imejumuisha virusi vyote ndani?
 
Ndiyo maana ya chanjo husika ambapo ina-activate kinga yako kusaka "mawimbi" yoyote yenye ufanano na korona. Similarity za mutants ni kubwa na ndiyo maana magonjwa tokezi ni almost the same.
 
Inawezekana sijaeleweka swali langu.

Ni kwamba, kama kumchanja mtu ni kumuwekea kimelea kinachoweza kusababisha ugonjwa fulani ili mwili wake uamshe kingamwili (ni kama kumpa maambukizi yasiyo na madhara),

Inakuwaje wale ambao walipata kimelea ambae sio attenuated kama wanaepewa kwenye chanjo wasiweze kutengeneza kinga mwili baada ya kukutana na huyo kimelea?

Kama suala ni mutation ya kirusi, tutaaminije kwamba sampuli zilizopo kwenye chanjo zitaweza kutengeneza kinga itakayopambana na kirusi aliejibadilisha?
 
Natural immunity iliyosababishwa na kirusi fulani ni specific kwa variant husika wa virus; chanjo imezingatia almost thousands of the virus variants.
 
Rais mteule wa Marekani Joe Biden jana Jumatatu amepokea chanjo dhidi ya virusi vya corona wakati akitazamwa moja kwa moja kwenye televisheni ili kushawishi wamarekani kuwa zoezi hilo ni salama.

Kabla ya kupokea chanjo hiyo, Biden alionekana akijiandaa na kisha kumweleza muuguzi kuendelea na shuguli wakati akiwa kwenye hospitali moja mjini Newark, Delaware.

Mkewe Jill Biden saa kadhaa kabla pia alipokea chanjo kwenye hospitali hiyo ambayo iko karibu na kwao nyumbani.

Baadhi ya viongozi wengine mashuhuri wa Marekani waliopokea chanjo hiyo tayari ni pamoja na makamu wa rais Mike Pence, spika wa bunge Nancy Pelosi na kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la senate Mitch McConnell.

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye mwezi Oktoba alipatikana kuwa na virusi vya corona kufikia sasa hajasema ni lini amepanga kuipokea.

Marekani inaongoza ulimwenguni kwenye idadi ya maambukizi huku tayari ikiwa imeshuhudia zaidi ya vifo 318,000 kutokana na Covid-19 kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Sidhani kama ni kweli kuna maigizo mengi sana kutuhadaa mtu anachoma sindani ya maji unaambiwa covid ili uingie mkenge shtuka hamna kitu hapo
 
Back
Top Bottom