Job Application FAILED

Arch OAK

Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
25
Reaction score
26
Habarini za saa hizi.

Nimejiunga muda mrefu sana hii portal ya ajira ila mpaka naandika hii thread haijawahi kukubari ku-upload picha.
Nimekuwa nikiapply inaniandikia Job Appl... FAILED nikajua labda sababu ya kozi yangu inaingia katka related courses ila zimetoka post za kazi ambapo kozi yangu ndio chaguo number 1 ila bado inaniandikia hivyo hivyo
Naomba mwenye kujua Je, shida ni nini??
Account yangu inasoma 90%

Shukran.
 
unaaply kazi zipi na requirements zinataka level gani ya elimu
 
Kuupload picha hakikisha picha ina

Kb chini ya 500
Na size 400×400

Kama picha ni kubwa ingia online zipi site mbali mbali kwa ajili ya ku resize picha.
 
Oh nilifikiria hivi pia sasa nimetoa ipo degree tu na bado inagoma.
Wewe ulishakuwa na qualifications za Masters kamwe hata ukiondoa vyeti hutobadili qualification kamwe…..vyeti ukishaweka vinatengeneza qualification ambayo data base ina kariri na hata ukiondoa vyeti lakini qualification ina baki! Uwezi badili sifa ulizinazi za elimu ambazo umeandika kwenye portal
 
Umewezaje kutoa?
Ok, ni hivi kabla sijakuwa verified na TCU niliweka tu level ya form 6 nikasave account kama mtu ambaye sina elimu ya juu na nikaiacha hivyo. Baada sasa ya kuverify vyeti nikarudi tena ku-update education ili niweke level ya juu hapo ndipo nikaitoa hiyo masters kwa kujua nitakosa kazi kwa hiyo level niache tu undergraduate.

Na ndio hivyo inaFail kuomba kazi labda kama mchangiaji hapo juu alivyosema inawezekana imekariri nina A-level certificate tu so sikidhi vigezo.
 
Update:

Nimefungua Account mpya kila kitu kiko sawa mpaka picha, sasa tatizo lililojitokeza ni kuwa ile ya mwanzo nilishaweka NIDA number hii ya pili siwezi tumia number ile ile.
Acha tukomae na Private sectors tu.
Shukran kwa michango yenu.
 
Kuupload picha hakikisha picha ina

Kb chini ya 500
Na size 400×400

Kama picha ni kubwa ingia online zipi site mbali mbali kwa ajili ya ku resize picha.
@Arch OAK fuata ushauri wa Youngblood kuwa na masters haikuzuii kuomba Kazi ya undergraduate. Narudia Tena kuwa na masters haikuzuii kuomba Kazi ya bachelor Nina ushahidi juu ya hili ndio maana naweka msisitizo. Pia jua kwamba nida ikishatumika kufungua account moja haiwezi kufungua account nyingine.
Tatu, tatizo ulilonalo ni aina ya picha unayojaribu kuiweka haipo compatible na system ya PSRS. So nenda google type image resolution then ifanyie adjustments accordingly
 
Mkuu, ishu yako inatatulika tu. WAPIGIE SIMU, waombe wafute cheti cha Masters. wengi wamefanya hivyo na mambo yamekuwa poa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…