mwl. mziray
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 597
- 398
Habari wanaJF.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukishuhudia uvujaji wa mitihani ktk shule mbalimbali au kitaifa hali inayopelekea baadhi ya wanafunzi kufutiwa matokeo ya mitihani yao.
Uvujaji wa mitihani upo wa aina mbalimbali kama nje ya chumba cha mtihani na ndani ya chumba cha mtihani.
Leo nataka nizungumzie uvujaji/wizi wa mtihani ndani ya chumba cha mtihani. Wizi huu wa mtihani hutokea ndani ya chumba cha mtihani na huwahusisha wasimamizi wa mitihani pamoja na wanafunzi kwa hisani ya mkuu wa shule au mwalimu wa taaluma.
Mchakato wa wizi huu hufanyika kwa wanafunzi kuchangishwa fedha kati ya 30,000/= mpaka 50,000/= (mara nyingi hupewa barua wapeleke nyumbani kwamba kuna safari ya kitaaluma). Fedha hizi hutumika kuwahonga wasimamizi wasio waaminifu mf. Wanafunzi 100 wakitoa 50,000/= kila mmoja itapatikana 5,000,000/= (5.m) ambapo kwa mwl anaelipwa mshahara wa laki 4 na makato juu kupewa 1.m isiyo na makato ni jambo ambalo si rahisi kulikataa.
Mipango hii inafanyika wakati mwingine bila msimanizi mkuu kufahamu kinachoendelea kwani anapozunguka ktk vyumba vya mitihani mchezo huendelea kwa umakini wa hali ya juu.
Walimu wa masomo husika nao hawapo nyuma ktk mchezo huu kwani baadhi huhusika ktk kujibu maswali ya mtihani yanayotolewa nje ya chumba cha mtihani kisha majibu kupenyezwa ndani ya chumba cha mtihani.
Wengi mnafahamu kuna shule nyingi zisizo na walimu au zenye walimu wa kuungaunga ambazo zinafanya vizuri ktk mitihani ya taifa halikuwa darasani hakuna kitu. Mara nyingi pia wanafunzi hawa wasio na uwezo wanapofaulu kwa wizi wanakataa kuendelea na kidato cha tano kwa kuogopa kuumbuka mbeleni. Wachache wanaojitoa mhanga kuendelea na kidato cha tano huambulia matokeo mabovu.
Wito: wizi wa mitihani huchangia kuzalisha watumishi mizigo kwa taifa ambao wanaweza kuliangamiza taifa. Tuungane kuupinga mchezo huo mchafu. Pia shule binafsi ziangaliwe kwa jicho la pekee kwani bila kutakatisha matokeo hawawezi kupata wateja hivyo mchezo huu ni maarufu zaidi huko.
Nawasilisha.