JK: Wezi wa Pesa za Umma Hawakamatiki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Wezi wa Pesa za Umma Hawakamatiki!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndebile, May 4, 2012.

 1. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,632
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Siku tatu baada ya rais 'kuwachimba mkwara' wezi wa pesa za umma hasa wa halmashauri za miji na manispaa milioni 62 zitaliwa muda mfupi ujao na wezi wazoefu wa Idara ya afya ya jiji la Mwanza.

  Wiki mbili zilizopita wizara ya afya ilitoa matangazo kupitia vyombo mbali mbali vya habari juu ya kuwepo kwa kampeni ya chanjo ya polio, surua kwa watoto chini ya miaka mitano. Katika hali isiyo ya kawaida hakukuwepo na zoezi hilo hapa jijini Mwanza na kilichofanyika ni janja ya kufanya kilele cha chanjo hizo kwenye zahanati ya Nyerere iliyopo mjini ambapo idadi ndogo sana watoto waliletwa kutokana na kutokuwepo na uhamasishaji wa kutosha pia nadhani ulikuwa ni mpango wa kufunika mpango wao wizi wa pesa za kampeni.

  Nilibaini wizi huo jana pale ofisi za idara ya afya pale nilipoona jamaa wanandaa voucher ya malipo ya zoezi la chanjo sh.milion 62 wakati zoezi halikufanyika kabisa.

  Nimeleta uzi huu kutokana na hasira za kunusurika kupigwa na akina mama walioleta watoto wao kupata chanjo kituoni kwangu wakidai wamesikia matangazo kwenye vyombo vya habari.
  Kibaya zaidi wizara iliwatangazia kuwa watapata kadi za kliniki za watoto bure wakati vituo havina kadi hizo kwa muda mrefu sasa.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  "Mafisadi hawakamatiki"-Pinda. Huo ndio ukweli, mengineyo usanii
   
 3. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Si mchezo...
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,620
  Trophy Points: 280
  wanakamatika tena kirahisi sana but not under ccm rule
   
 5. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hivi hawa viongozi wetu wakoje?yaani kuna watu wachache wanakuwa juu ya mamlaka kiivi.
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uwizi wa Kikwete na Utouh ni upi hapo? MoDa huu ni udhalilishaji wa viongozi kwa mambo yasiyo wahusu.

  No connection baina ya heading na content!!!!
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kichwa cha habari na habari yenyewe vitu viwili tofauti
   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mkuu inaonyesha wewe haupo kwenye huo mgao ndio maana umeleta huu uzi. Sisi waswahili tatizo letu ni kuwa tuna vijinasaba vya wizi kwenye damu!
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  badilisha habari yako isomeke vizuri
  andika. Kikwete na Utoh: Wezi wa pesa za umma hawakamatiki
  ulivoandika ni kuwa wao ndio wezi wa pesa za umma
  kuwa makini
   
 10. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,231
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  jamani...sasa hapo kikwete na utoh wameingia vipi??

  afu huyu mtu kaandika 'CONFIRMED' tukiwapeleka mahakamani kudai udhibitisho sijui utajibu nini

  tatizo mtu anaamka asubuhi akijisikia kuandika kitu JF baaasi anaandika tuuu.
   
 11. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  afadhali mkuu umenisaidia...mi nilikuwa sielewi heading na maelezo...
  nilishangaa wenzangu wanachangia nikadhani nimeamka vibaya
   
 12. M

  Moony JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kikwete na Utouh wanahusika vipi hapa?
   
 13. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,632
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Muuguzi na Mhasibu wapi na wapi? Hata kwenye vikao vya bajeti siruhusiwi kukanyaga!
   
 14. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,632
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Wakati unafikiria juu ya mleta mada kijijini kwenu watoto hawakupata chanjo! Aliyeshiba hamjuhi mwenye njaa.
   
Loading...