JK wawajibishe hawa Mawaziri wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK wawajibishe hawa Mawaziri wako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by landiis, Feb 21, 2012.

 1. l

  landiis Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (DK. Mponda),Waziri wa Ushirikiano wa Jumuia ya Africa Mashariki (Sitta) ,Naibu Waziri wa Miundo Mbinu na Ujenzi (Dr. Mwakyembe) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI- Manumba) wote hawa wanapaswa kutoswa na JK kwa kuvunja maadili ya uongozi kwa kubishana hadharani mbele ya wanaowaongoza juu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe. Sitta anatumia ugonjwa wa mwenzake kujipatia umaarufu baada ya kushindwa uspika na richmond.

  Mponda huyu amethibitisha hana uwezo wa uongozi hasa kushindwa kumaliza mgomo wa madaktari na baada ya DCI kukanusha juu ya madai ya Sitta kuwa Mwakyembe hakulishwa sumu alikurupuka na kusema yeye hahusiki na habari hiyo kama Wizara ya Afya HAKUPASWA KUPANUA MALUMBANO.


  Manumba alishazoea kuwazima walalahoi ndio maana alijisemea bila kufikiri kumbe akakumbana na washenzi zaidi yake. Mwakyembe tunakuombea upone ila una udhaifu mmoja kukubali imani yako kutekwa na maradhi yanayokusumbua kuwa agenda badala ya kutamka wazi sitaki ugonjwa wangu uwe agenda maana hufaidiki kitu bali familia yako inakosa msemaji mpaka sitta.

  Picha inayojionyesha hapa hakuna mtawala mwenye maamuzi magumu. NINGEKUWA MIMI JK NINGEWAPIGA WOTE CHINI ILI WAKALUMBANE MITAANI.
   
 2. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  That is not smart. but is just my opinion.
   
 3. L

  LISAH Senior Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Wewe kweli katili Mwakyembe yuko hoi halafu unataka kumuongezea MACHUNGU?
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  WEWE BILA SHAKA NI GAMBA; Hoja yko ni kumuogopa SITTA na MWAKYEMBE tu huna lingine.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 5. R

  RUTARE Senior Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini afanye ugonjwa wake kuwa agenda. kumwadhibu mtu sio ukatili waswahili husema mchelea mwana kulia hulia mwenyewe na Mungu anasema "wote niwapendao huwakemea na kuwarudi"
   
 6. m

  mbezibeach 2 Senior Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mmmmmh kwa style hii Great Thinker wangu nakupeleka Darasa la Chekechea.....Nilidhani utaongelea Constructive Issues kama ukosefu wa nishati ya umeme ambayo imesababisha kuongezeka mno kwa bei za bidhaa kutoka viwandani...Mfumuko wa bei unaotisha...Ukilaza na ukosefu wa mipango alionao nao Waziri wa fedha na wale jamaa wa pale Twin Towers uliofikisha Taifa hili katika hali hii kifedha....Madhara mapana yaliyosababishwa na Mgomo wa Madaktari...

  Anyway nakuunga mkono hoja yako...Kwamba u DCI apewe Millya....Waziri wa A.mashariki awe Serukamba...na Naibu waziri wa Nishati awe January...Nadhani hapo Ikulu lazima mtaingia...
   
 7. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kweli ubongo muhimu kuliko miguu! Hivi mtu aliyeshindwa kuwajibika yeye mwenyewe ana uwezo wa kuwawajibisha wenzake?
   
 8. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Pole, your wish is never going to be granted!
   
Loading...