JK: Nitawatenganisha Dk. Mponda, Nkya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Nitawatenganisha Dk. Mponda, Nkya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 14, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMANNE, 13 MACHI 2012 06:51 BENJAMIN MASESE NA GABRIEL MUSHI, DAR ES SALAAM


  HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete,

  Amesema mgomo wa madaktari ulikuwa batili, huku akiahidi kufanya mabadiliko ya kuwatenganisha Waziri wa Afya, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, katika kuiongoza Wizara hiyo.

  Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo alitumia mkutano huo kueleza kwa kina sakata la mgomo wa madaktari uliokuwa ukiendelea nchini.

  Alisema pamoja na mambo mengine, katika suala ya uwajibikaji, hasa kwa viongozi wa kisiasa, wakiwemo mawaziri hawezi kuwafukuza kazi mawaziri hao, kwa sababu hawana tuhuma zozote kuhusu mgogoro huo.

  “Lakini siwezi kuwafukuza waziri na naibu wake kwa sababu hawana tuhuma zozote juu ya mgogoro huo.

  “Ndiyo maana niliwaomba kuhusu tuhuma za viongozi hawa mziweke pembeni kwa sababu zile za Katibu Mkuu, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa, ziliwekwa wazi.

  “Nilipokutana nao waliniambia wanataka kuzungumza na viongozi wapya, lakini nikawaambia kwa kuwa mimi ndiye mteuzi na ninaweza kuwaondoa leo au kesho, hivyo wasubiri waniachie masuala hayo ili wasitafsiriwe kisiasa.

  “Nikawaambia kitu mfumo kwa sababu hizi wizara mawaziri wanapita, kama Dk. Magufuli amehama kutoka kwenye Wizara ya Mifugo, Uvuvi na sasa Ujenzi,” alisema Rais Kikwete.

  Alisema jambo kubwa alilojifunza katika mgomo huo ni kutokuaminiana kati ya pande mbili hizo, hasa viongozi wa Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).

  “Kikubwa nilichogundua hapo ni kutokuaminiana, lakini nawataka waniamini kama walivyosema wananiamini, hivyo waniache nitayatekeleza.

  “Kwa sababu katika wizara wapo viongozi ambao kweli hawaaminiani, Katibu Mkuu hamuamini Naibu au Waziri hamuamini Naibu wake kwa kudhania kuwa atamchukulia nafasi yake.

  MGOMO BATILI

  Kutokana na hatua hiyo, Rais Kikwete, alisema wazi mgomo huo ulikuwa batili na haustahili kurudiwa tena.

  “Taasisi ambazo hazitakiwi kugoma ni TANESCO na Idara ya Maji, maana hivyo ni vitu muhimu ambavyo watendaji wake wakigoma madhara yake ni vifo, tofauti na migomo kama ya watu wa bandarini ambao wakigoma baada ya mgomo watafanya kazi usiku na mchana kupakua mizigo, lakini madaktari hawawezi kurudisha roho za watu.

  “Hata nchi nyingine duniani madaktari wakigoma wagonjwa wakafariki, hushtakiwa kwa kosa la mauaji ya kukusudia kama ilivyokuwa kwa migomo yote miwili ya Tanzania.

  AWAPONDA WANAHARAKATI

  Rais Kikwete alisema amefadhaishwa sana na kitendo cha wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kwa kuingilia mgomo huo wa madaktari na kuwaunga mkono.

  “Yaani nimeshangazwa na watu wanaojiita wanatetea haki za binadamu, wameshindwa kutetea haki ya watu kuishi wanatetea migomo? Kitendo hicho kimenifadhaisha sana.

  “Tusitafute umaarufu kwa kupitia migogoro, haya mambo mengine ya kisiasa tuyaweke pembeni, tunajua kuwa wana agenda za kisiasa lakini wasiziingize huku, kwa sababu haki muhimu ya kutetea kwa binadamu ni kuishi.

  “Sijapata taswira za wanaharakati hao, lengo lao sijui nini,” alisema Kikwete na kushangiliwa na wazee hao, huku wakisema ‘wape ukweli’.

  AWAONYA MADAKTARI

  Aidha aliwataka madaktari hao hata kama wanaichukia Serikali wasitoe masharti ili watekelezewe madai yao.

  “Hata kama mnatuchukia, mkiri kwamba kuna vitu vingine Serikali imetekeleza, kwa mfano mwaka 2006 tuliongeza mishahara ya wauguzi na madaktari kwa asilimia 100.

  “Yaani kutoka Sh 200,000 hadi 400,000 kwa wauguzi, kwa madaktari tuliongeza kutoka Sh 700,000 hadi Sh 900,000 kwa madaktari wanaoanza.

  “Sasa hayo madai yao ya kutaka kuongezwa mishahara kutoka 900,000 hadi milioni 3.5 ni vitu ambavyo haviwezekani, lakini tumwelekeze Gavana Mkuu wa BoT achapishe noti mpya ambapo ingesababisha mfumuko wa bei uzidi kupaa kutoka asilimia 19 hadi 50.

  ASEMA MGOMO NI HATARI

  Pamoja na kuwapongeza madaktari kumaliza mgomo huo, lakini kwa vipindi vyote viwili mgomo huo ulikuwa mgumu sana.

  “Mgomo wa madaktari gharama yake ni maisha ya binadamu, lakini mgomo wa madereva wa daladala matokeo yake ni adhabu kwa abiria kutembea kwa miguu, lakini watafika wakiwa hai.

  “Mgomo huu ulikuwa na wakati mgumu, mashaka kwa kiongozi yeyote, unatishia uhai wa wananchi, nawashukuru wauguzi ambao walikuwa wanapewa vitisho lakini hawakushiriki,” alisema.

  Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mawaziri, Makatibu na viongozi wa Idara za Serikali.

  Mgogoro huo wa madaktari ulianza Desemba mwaka 26, baada ya madaktari wa mafunzo kwa vitendo kucheleweshewa kupewa posho zao za kujikimu.

   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,237
  Trophy Points: 280
  Ndo watakuwa wamewajibishwa??siasa za bongo fujo mtindo mmoja!!:A S 13:
   
 3. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Jenerali Ulimwengu alisemaga hamna siasa sikuhizi bali kuna mipangilio ya kula dili
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hakuna kuwajibishwa... wanagawiwa vyeo vingine!!! Ni hatari kwa taifa la serikali ya CCM
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kikwete hakusema hayo maneno,sijui mwandishi kapata wapi hiyo mambo.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,473
  Trophy Points: 280
  madaktari na wanaharakati watasema wenyewe.
   
 7. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Hivi ukikosa cha kuandika ndio unapayuka tu! Ulisikiliza hotuba au ulisimuliwa tu na babu yako 'mzee wa dar es salaam!' mbona yote hayo yapo kwenye hotuba?
   
 8. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,650
  Likes Received: 3,299
  Trophy Points: 280
  haja kubwa hupelekwa chooni ila ndogo waweza jistiri vichakani vilevile upumbavu una jukwaa lake. Sina hakika kama ni kwa wazee wa dar. Na sio wa moshi wala mwanza!!
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hakusema kitu kama hicho labda kama masikio yako yana makengeza.
   
 10. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mponda na Nkya wameshindwa kazi - Full stop!
   
 11. A

  August JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kuna nafasi wizara ya mwamaji na wizara ya mwaujenzi
   
 12. S

  Saashisha Elinikyo Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki Tanzania
   
 13. loiboo

  loiboo New Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  "personality is humanity and not a thing" amakweli JK NI POPO he chewing and spreying<kung'ata na kupuliza > nikiwa na maana anawabase madaktari na kuwaomba msamaha ana maana gn ? kiongozi wa nchi anafundisha ni jamii halisi ya kitanzania
   
Loading...