Jk na philosophy mpya ya utawala; street governance | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk na philosophy mpya ya utawala; street governance

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NewDawnTz, Mar 24, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa wale watazamaji wa ITV au Channel-e ya South Africa watakuwa wanafahamu kipindi maarufu cha mwanasheria anaendesha kesi nje ya majengo ya mahakama (Street Court)....inarahisisha badala ya watu kubanana mahakamani

  JK nae ameanza....Sasa ana aina falsafa mpya ya kuiongoza serikali yake...Street Governenace....Hataki kubanwa na kuta kwa mujibu wa taratibu za vyombo vilivyopo.........Anatawala nchi akiwa mitaani....anaongoza serikali mitaani na kwenye vyombo vya habari...Ndivyo ninavyomuona

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka chombo kimoja muhimu san kinachoitwa Baraza la Mawaziri. Pamoja na mapungufu yake, katiba hii kuanzia Ibara ya 54 mpaka ibara ya 59 inaunda rasmi baraza la mawaziri kama chombo kikubwa cha msaada wa karibu kwa utendaji kazi wa Raisi.

  Kimantiki, japo si mtaalamu wa Sheria, baraza la mawaziri linaloundwa na mawaziri wote ndiyo sehemu ya Raisi kukaa na mawaziri wake, kujadili utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwamo usimamizi wa sheria pamoja na namna ya uendeshaji uchumi ikiwamo pia kutoa maazimio na msimamo wa Raisi ambao mawaziri wanapaswa kwenda kutekeleza baada ya kikao cha baraza la mawaziri

  Ninapoangalia ziara za Raisi na maagizo yake wizarani, anavyoshushua mawaziri wake kana kwamba yeye ni MWENYEKITI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI, na jinsi baraza lake linavyotofautiana na kujichanganya naanza kuhoji kama nchi hii ina BARZA LA MAWAZIRI.....

  Hata hivyo huwa wanakaa vikao vya baraza la mawaziri, Hivi huwa wanafanya nini huko kwenye baraza la mawaziri? Au ni kuijadili CHADEMA tu? Kama sivyo, mbona maagizo ya Kikwete yanaonekana angepaswa kuyatoa kwenye baraza la mawaziri na sio akitembelea wizarani? Je hizi wizara atazitembelea kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu? Je hayangekuwa na uzito kama angeyatolea kwenye Baraza la Mawaziri zaidi ya kuyatolea mitaani?

  Sikatai wajibu wa Raisi kutembelea wizara, ila ninachohoji ni madhumuni yake na kule kushushua na kuagiza ambako angepaswa kufanya ndani ya baraza la mawaziri

  Hayay yote yananifanya niwaze hivi

  1. Yawezekana ni katika kutafuta huruma ya watanzania kuwa yeye ni mchapakazi ila watendaji wake wanamuangusha na ndio maana anaona akitoa kwenye baraza wananchi hawatamuona "live" zaidi tu ya kusikia kwenye media.....Je ameshapima tija kati ya umaarufu na ziara zake na ulegevu katika utendaji? Naona zinaleta umaarufu zaidi kuliko tija kwa jinsi zinavyoendeshwa
  2. Yawezekana kwenye baraza la mawaziri hakuna kuelewana kuna mgawanyiko na LABDA Mh. ni mdhaifu kutoa kauli yenye busara yenye kukata maneno na itakayofuatwa na wote
  3. Au ameamua kuua rasmi baraza la mawaziri kwa kutoendesha hoja zenye msingi na PIA INAONEKANA HAPOKEI TAARIFA ZA UTENDAJI WA WIZARA KWENYE BARAZA LAKE
  JK usingoje ziara, tumia vema Baraza la mawaziri....La sivyo itakula kwako....Watalipa watumishi hewa na haijadiliwi kwenye baraza mpaka miaka ikatike tena u-revive tena ziara zako wakati watu washakula....Yale yale ya Magufuli uliyomsema kuwa walikuwa wapi wakati watu wanajenga wakati na wewe mwenyewe ni Mtanzania, tena namba moja....Je ulikuwa wapi na baraza lako wakati watu wanasogea barabarani

  Achana na "Street Governance" na tumia baraza lako la mawaziri
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Je falsafa ya uwajibikaji wa pamoja anaiweka mfukoni ili yeye peke yake aonekane anafanya kazi.Nini maana ya kuwadhalilisha mawaziri wake kwenye runinga huku akijua wazi kuwa anayo nafasi ya kupata taarifa za kila mwezi, robo mwaka, nusu mwaka kutoka kwa mawaziri wake???? Hapa hajatushawishi yeye ndiyo anaonekana kilaza kwani utawala una kanuni zake si kama anavyofanya yeye.

  JK hujatushawishi bado hatuwezi kukuonea huruma kirahisi.
   
 3. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Huyo ndo ****** usanii mpaka kupitiliza anauza sura.
   
 4. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Hii analysis yako nimeipenda mkuu!!
   
Loading...