JK mfukuze kazi Kandoro badala ya kuwa "Disappointed" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK mfukuze kazi Kandoro badala ya kuwa "Disappointed"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,616
  Trophy Points: 280
  Kikwete disappointed by Dar City fathers

  2009-01-02 12:15:51
  By Lusekelo Philemon​

  President Jakaya Kikwete has expressed his disappointment over the Dar es Salaam City fathers` failure to put up proper strategies to beautify the country`s commercial hub.

  Speaking at this year`s National Tree Planting Day yesterday in the city, Kikwete directed the city fathers to ensure that the country`s key commercial capital was among the best in east and central Africa.

  He said that the situation in the city was in total jumble of untidiness making it unable to attract tourists.

  ``So, I call upon municipalities to ensure that the city is maintained to boost tourism in the country,`` he said, adding that in most cases foreign tourists did not visit it but rather treated it as a transit point.

  For instance, he said most tourists preferred to visit Zanzibar and the northern tourist circuit of Arusha and Kilimanjaro regions.

  President Kikwete urged city fathers to wake up and restore the beauty of Dar es Salaam, making both local and foreign tourists enjoy their stay in the same.

  He however cited Coco Beach along the Indian Ocean coast as a very beautiful place, adding that it had been abandoned by the city authorities.

  ``This is a very good beach that if maintained would attract more tourists to visit Dar es Salaam. Nothing has been done to transform it,`` he said.

  According to the president, cities like Durban in South Africa and Abidjan in Ivory Coast were among the most attractive on the African continent.

  He said those two cities had similar geographical location with Dar es Salaam.

  Kikwete also urged urban planners to ensure that the city was designed in a very beautiful manner and made attractive.

  He said that currently there was no uniformity of buildings in the city, a thing that rendered it be in an awkward situation.

  He further said trees planted along Dar es Salaam roads also had no uniformity, making it to be in a total mess.

  On the issue of global warming, President Kikwete urged people to plant more trees as that would create more employment opportunities as well as sustain the ecosystems.

  He said there were socio-economic benefits of reforestation including direct employment, infrastructure development, skills-transfer and creation of markets for related products and services.

  ``Trees provide local communities with additional products such as fuel-wood, fruit, nuts and herbs, and opportunities for agricultural activities,`` he said.

  He said trees also helped to curb the negative impacts of global warming, including increased human mortality, shifts in crops and agriculture production and further degradation of the local ecosystems.

  The National Tree Planting campaign started in 2001, with a projection of planting a total of 31m trees every year. Yesterday about 2000 palm trees were planted along Kilwa Highway in the city.

  SOURCE: Guardian
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa sijui kama Kandoro, ni mkurugenzi ama meya wa Jiji la Dar...
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa Mkoa anastahili kuwa mtu wa kwanza kuwajibika pale ambapo wilaya zake hazifanyi vizuri maana yeye yupo pale kuhakikisha utendaji wao ni mzuri, vinginevyo ana haki ya kumtaarifu Rais ambaye ndiye kutoridhishwa na utendaji wao na yeye kuamua kuwaondoa madarakani.

  Mrema alipokuwa Mambo ya nje alifanya kampeni za kusafisha na kupendezesha jiji la Dar ambazo wananchi walizifurahia na kuziunga mkono maana Mkuu wa Mkoa wa wakati huo alikuwa amezembea. Na kweli kulikuwa na mabadiliko ya kutia moyo katika wilaya zote tatu.

  Kama Rais wa nchi kaweza kulizungumza hili, basi Mkuu wa Mkoa angeweza kabisa kulifuatilia.
   
 4. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Yote sawa lakini hili la Mrema kuwa mambo yanje naona, Bubu hapo anaanza na fyongo.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Bado sioni umuhimu wa Mkuu wa Mkoa katika masuala ambayo yapo chini ya uwezo wa Jiji.
   
 6. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Dar Tourist waje kuangalia nini? Kwa sababu mnataka kubomoa majengo yoote ambayo ni ya zamani ambayo yangukuwa tourist atraction, sasa waje kuangalia maghorofa makubwa? Kama maghorofa huko walikotoka wanayo mengi sanaa. Labda hao tourist wa maghorofa watoke Mwakaleli na sio hao anaowategemea. kitu cha kufanyika ni kuweka vizuri majengo ya zamani na ku-keep mtu wa kuhakikisha yanatunzwa halafu mnaweka na Route kabisa ya kuyaelezea hayo majengo na vitu vingine wakiuliza hata hapa JF watapewa miongozo mizuri ya kufanya hivyo.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,616
  Trophy Points: 280
  LOL!...Ni mambo ya ndani...:)
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa Mkoa akiona mashimo yanazidi kuongezeka barabarani, uchafu unazidi kulundikana kila kona ya jiji, mji unaonekana mchovu na hauna seheme zozote za kupendeza kama bustani na sehemu za kupumzikia aendelee kunyamaza tu kwa kuwa hayamuhusu!!! Basi hatuna haja ya kuwa na Kandoro Dar maana kama mkuu wa mkoa kwa namna moja au nyingine anastahili kabisa kufuatilia chochote kile ambacho hakimridhishi yeye kama Mkuu wa Mkoa, labda alikuwa anaona mambo ni shwari tu. Lakini si ajabu alionyesha pua yake katika kampeni ya kupanda miti ambapo JK alikuwepo, pamoja na kuwa swala la kupendezesha jiji 'halimhusu'.
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  I don't get it, whoever has prepared this speech was not serious. My take is that source of all these problems is the Ministry of Lands and Urban Planning. Jamani, Look at all open areas including beach plots where by the Land Laws (1998) has made it very clear about beaches but the very governments has embraced and blessed wabaka uchumi to encroach these beaches as a result the only place to go for a pleasure is coco beach the rest of the beaches are privately owned (ingawa ni kinyume cha sheria).
  Mipango na sera za miji haziko wazi, a lot of ujanja ujanja. Genuine investors normally tend to shy away from dealing with unprofessional civil servants who normally believe in bahasha and not the quality to be rendered by the investor.
  Mr. President, problem has been inherited from Awamu ya 3, It is crystal clear that your government needs to start rectifying these problems from top downward and not otherwise. The three municipals have a lot of problems but the place to start with is a ministry of lands and urban planning.

  I beg to disagree.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,616
  Trophy Points: 280
  Kuhusu poor planning ya miji yetu hili nakubaliana nawe, lakini kuna hili la mashimo barabarani, uchafu kurundikana sehemu mbali mbali na jiji kutokuwa na sehemu zozote za kupendeza hili mkuu wa mkoa pia anastahili kuwajibika.

  Kama mkuu wa mkoa aliyedai Mrema alipokuwa mambo ya ndani alimuingilia eneo lake la kazi kwa kuanzisha na kusimamia kampeni ya usafi na kupendezesha jiji la Dar, alipoteza kazi yake kwa kauli hiyo, basi Kandoro pia ana haki ya kuwajibika.

  Huu utamaduni wenye kasoro ambao kingunge anaona mahali kuna kasoro kubwa za kiutendaji lakini hasemi lolote kuhusiana na kasoro hizo kwa sababu hilo 'siyo eneo lake' la kazi umepitwa na wakati na kuna kila sababu ya kuupinga usiendelee kuwepo.
   
 11. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka kama miaka mitano hivi iliyopita kuwasikia kundi la vijana fulani wa kizungu waliokuwa wamefika Dar International Airport (kama ilivyojulikana) wakisema kuwa Dar ilionekana kama vile ilikuwa imekumbwa na Operation Desert Storm (ile vita ya kwanza ya Marekani dhidi ya Iraq ya Sadaam Hussein). Kweli nilipoangalia maeneo ya Buguruni tulipokuwa tukipita niliweza kuona mantiki ya kilichokuwa kikiongelewa. Tatizo la miji ya Tanzania ni kwamba watu kwanza wanaruhusiwa kufanya ujenzi na mambo mengine kiholela bila mipango halafu Serikali inatoka nyuma na kubariki au kubomoa. Kwa mtindo huu hatuwezi hata siku moja kurekebisha hali hii. Hivi hao wataalamu wetu wa mipango miji huwa wamasoma vyuo gani? Wanafundishwa kupanga au kuvuruga?
   
 12. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #12
  Jan 5, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  i think this should be additional points, unachosema wewe na watu kushindwa kuweka mazingira vizuri sidhani kama vinapingana ila vinaonyesha macahfuko zaidi.

  Du humu ndani tuna viongozi wazuri sana, nadhani tukiwapa urais hata sisi tutaweza kuwa angalau wakuu wa wilaya maana watu wengi watakuwa recruited and fired. kila ukiwa dissappointed hukemei au kutoa maelekezo, unafukuza na kuwaambia watu wajiuzuru,
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuna point katika maelezo aliyoyatoa Mh Rais hasa pale aliposema kuwa watalii wengi wanaokwenda Zanzibar hupitia Dar es Salaam.

  Ninapenda kutoa wazo ambalo ni rahisi kutekelezeka. Wadau wote wanahusika na sekta ya utalii kitaifa na mkoa wa Dar es Salaam wajaribu kutafuta vivutio ambavyo vitatangazwa mahususi kabisa kama starting point ya kuelekea Zanzibar.

  Kwa mfano, kwa watalii wanakwenda kupanda mlima kwa Kilimanjaro wakitokea Nairobi wamezoshwa kuwa ni lazima usiku wa kuamkia siku ya kwenda Kilimanjaro ni lazima wawepo Carnival kwa ajili ya kupata nyama choma. Hiki kivutio kimeongeza thamani kwa mtalii anayepanda mlima kutokea Nairobi.
   
 14. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu. Mheshimiwa Rais amechukua hatua ya kwanza kulizungumzia suala hilo.

  Inatisha ukiangalia Jiji la Dar ukiwa juu (kwenye ndege), linaonekana kama jalala. Ujenzi holela, tena usio na hadhi wala style unalifanya Jiji litie aibu kabisa. Kuna siku nilikuwa kwenye ndege iliyokuwa ikitoka nje ya nchi, wakati ikikaribia kutua, kila abiria (hasa wakigeni) alikuwa akitazama mandhari ya Jiji kwa mshangao wa wazi kabisa. Ilikuwa inatia aibu kiasi kwamba nilifumba macho.

  Nadhani tunawajibika wote kuhakikisha mazingira yetu yanavuti. Na serikali iwe kali zaidi wakati ikiona watu wakivunja sheria za ujenzi waziwazi. Si watu hao wanaonekana wakifanya shughuli hizo? Tupande miti ya matunda zaidi na tuipande kwa mpangilio. Natumaini Jiji litapendeza tu.
   
Loading...