Mkuu Papa hata mimi kama umesoma bandiko langu naunga mkono azimio hili la SADC kupeleka neutral force Goma, DRC kuzima operesheni za waasi wa M23,tena naona wamechelewa sana.Hoja yangu niliyonayo na JK ni yeye kushindwa kuwaeleza ukweli akina Kagame na Museveni kwenye kikao cha awali cha Kampala na yeye kushiriki kutoa maazimio ambayo kwa kweli yalikuwa kama ya kitoto na yenye kuwabeba waasi hawa.
Nadhani JK was supposed to be firm on the matter na kuonesha kutokukubaliana na maazimio hayo.Kitendo cha yeye kushiriki kikao kile ambacho kilitoa maazimio ya Kampala bila kuonesha kuyapinga na baadaye kushiriki kikao cha SADC ambacho kimekuja na maazimio yanayokanyaga kikao cha Kampala (Hata kama ni mema na tunayaona ya busara) kinampunguzia credit na kama Rais anayeongoza moja ya majeshi imara Afrika alipaswa kuwaonesha akina Museveni kwa nini wanapaswa kuacha undumilakuwili na kusitisha miradi yao huko Goma.
WanaJF,
Tukumbuke, Kabila mkubwa (Baba yake na Joseph) aliingia madarakani kwa msaada wa vikosi vya Rwanda na Uganda. Rwanda na Uganda sio kuwa walikuwa wanampenda sana Mzee kabila bali walikuwa na maslahi wanayonyemelea. Masharika mwa DRC, kuna ou kabila la wanyamulenge, hawa ni watutsi wenye asili ya Rwanda. Wanyankole wa Uganda (kabila la mseven) ni watutsi bila hata kuacha shaka lolote. Pamoja na kwamba Rwanda na Uganda walikuwa wanafukuzia mali asili za DRC pia nia yao kama walivyokuwa wamekubaliana na Kabila mkubwa ni kuanzisha kile kinachoitwa 'HIMA (TUTSI) EMPIRE, ambayo itamega sehemu ya mashariki mwa DRC na kuunganishwa na nchi za Rwanda na Uganda, pia tukumbuke Kagame alikuwa Mkuu wa Intelijensia wa Mseven kabla Kagame hajapata madaraka ya urais nchini Rwanda na Kagame aliingia madarakani kwa msaada wa vikosi vya Uganda.
Baada ya Kabila mkubwa kuingia madarakani, wananchi wa DRC walianza kupiga kelele kuhusu uwepo wa watutsi wengi kwenye serikali na hasa Jeshi la DRC. Generali Kabarebe ambaye kwa sasa ni Waziri kama sio Mkuu wa Majeshi ya Rwanda alikuwa Mkuu wa majeshi ya DRC wakati wa kabila mkubwa. Bizima Karaha (Jina halisi ni Bizimana) alikuwa member wa cabinet kwenye serikali ya DRC naye alikuwa mnyarwanda achilia mbali nafasi nyingine nyeti ambazo hadi leo wanyarwanda wamejichomeka. Sasa Kabila mkubwa baada ya kelele nyingi za wananchi wa DRC aliamua kuvunja makubaliano na kuamuru majeshi ya Rwanda kuondoka nchini DRC, kutokana na tamko hilo wote tunajua yaliyompata Mzee kabila.
Sasa hujuma za M23 mashariki mwa DRC, ni kagame na Mseven wanaotaka kujaribu kutimiza ndoto zao za kuanzisha na kjenga HIMA EMPIRE AU TUTSI EMPIRE. Bahati mbaya jumuia ya kimataifa imeshawashtukia kuhusu kusudio lao hilo. Lakini tutazame madhara ya kukosekana utulivu mashariki mwa DRC kwa Tanzania. Asilimia kubwa ya biashara zinazoendeshwa nchini DRC zinatokea Tanzania au zinafka DRC baada ya kuingilia Tanzania, kwa maana nyingine Tanzania kiuchumi inaitegemea sana DRC. Kuiacha DRC iendelee kuandamwa na hao watutsi ni sawa na kuacha uchumi wa Tanzania uzidi kudidimia kisa kagame na mseven wanataka kuanzisha hima empire na kuiba raslimali za DRC.
My take,
Acha tupeleke majeshi DRC ili tulinde miraji yetu, tufahamu pia kwamba sio rahisi kupigana na waasi waliozoea mazingira na jiografia ya mashariki mwa DRC lakini ni bora kufanya hivyo kuliko kusubiri na kushuhudia maslahi yetu ya kiuchumi yakianguka. Mugambe aliwahi kutoa pendekezo wakati ule Rwanda inaivamia DRC, yeye alisema, wakti Rwanda inapigana mashariki mwa DRC, Tanzania kama mwananchama wa SADC itoa ardhi yake ili vikosi vya SADC vianzishe mashambulizi vikitokea Tanzania kwenda Rwanda, Hapo Mhe. Mkapa aliona noma na kukataa pendekezo sahihi la Mugambe kwani lingmfanya kagame ku-withdraw majeshi yake ili aje atetee nchi yake kwa uvamizi huo. Tumuunge mkono mhe. Rais kwa hatua ya kuungana na wananchama wa SADEC kupelekea askari mashariki mwa DRC. lAKINI MWISHO, mashariki mwa DRC kuna waswahili wengi sana wenye mafungamano na watu wa kigoma, kwa hiyo kwa interest ile ile ya akina kagame na mseven na sisi ni hivyo. Haya wenye kujua zaidi tuchangia.
katika SADC hakuna wa rais wa kuaminika wote wapiga deal, wameona uganda na rwanda wanafaidi nao wanataka wapige za kwao, DRC like JAY Z it is a real deal,
Huwa sielewi hii kitu,tuna ndoto ya kuunganisha bara la Afrika huku tukiendelea kuligawa vipande! Kesho mtaigawa Kivu alafu baadae Kivu na Congo zitaomba kujiunga EAC ambayo tunaota ije kuwa nchi moja what a dream!!!
Ni tamaa za viongozi tu,Kwa mfano Tanzania ni nchi kubwa sana pia kuliko zote EA,unadhani mkuu DSN tukitofautiana solution itakuwa kuigawa pia?
Kongo ni ya Wakongo tuwaache waamue wenyewe bila kuwaingilia na cha kuwasaidia ni kuimarisha usalama na kulijenga upya jeshi lao ili lisimamie usalama bila kuingiliwa na watawala wenye uchu.
Wowowo!!
JK alifanya jambo la msingi sana kutowapinga papo hapo!! hata ningekuwa mimi ningefanya vivyo hivo katika misingi ifuatayo:-
1. JK alienda kikaoni alishatoa msimamo wa Tanzania ila wao walikuwa hawajasema msimamo wao hadharani. kwa hiyo chochote kile kitachosemwa kinyume cha ule msimamo wa wazi ulotolewa na Tanzania kingekuwa hakikubaliki straight away. and thats what happened!! Na kwamba wale jamaa wangekuwa na akili wangeahirisha hicho kikao maana jamaa alishasema mambo ambayo yapo nje ya mpango wao!!
2. Haikua jambo la busara kwa Tanzania kutoa hdharani tamko lolote linalopingana na yaliyosemwa na mseveni kwa sababu yangeongeza mpasuko katika ule mgogoro kwani kila mmoja wetu anajua jinsi gani Uganda na Rwanda wanavyokwiba rasilimali za Wakongomani.
3. Aliye na nguvu siku zote hana haja ya kujibizana bali huchukua hatua. Tanzania ilichukua hatua za kiutawala dhidi ya M7 na KG kupitia SADC. Tanzania ina nguvu na uzoefu katika kusimamia amani katika nchi zenye civil wars [refer:- Lebanon; Liberia; Sudan; Zimbabwe; Namibia; e.t.c] kwa hivo wanajua intelijensia ya civil wars.
Mkuu Papa D again naomba nikuulize swali dogo tu.Kulikuwa na tatizo gani JK kuurudia msimamo wake kwenye kikao hicho cha Kampala? Njia nzuri ni yeye kukubali kushiriki na kuwa sehemu ya maazimio yake au alipaswa kutokukubaliana mapema? Huoni kwa sasa Kampala na Kigali wanaendelea na utekelezaji wa maazimio hayo (ambayo JK alikuwa sehemu yake)? Sasa huu mkanganyiko wa maazimio ya SADC na Kampala si ndiyo mpasuko zaidi?
waswahili wanasema mchawi mpe mwana amlelee .suala la kongo na museveni na kagame na mikataba ya msituni vinajulikana ,kuwapa hii kazi ya kuleta amani congo ni kuona hawa jamaa wana muelekeo gani na congo naona ni mapema kusema zaidi kwa kuwa hapa tunaona wamekuja kukutana tena kwenye jumuia ya sadc na kuunda jeshi moja ,kuilinda congo itakuwa ni miujiza viongozi hawa kukiuka makubaliano hayo. kimsingi congo inatakiwa iwe ni tulivu uchumi ukue .
We unaonekana ni walewale,subiri unaogopa nini?. Kabila kesha wakamata askari 10 wa Rwanda pale Goma jana!. Kama alivyowahi sema Nyerere wakati wa vita na Idd Amin wa Uganda wakati huo'za masika zinawanyeshea kwa sasa,subirini za vuli'!
Kesho mazungumzo yanaendelea mjini Kampala. Tusubiri tuone.
Ni ajabu sana Kagame na Museven wanatuhumiwa kusaidia waasi wa M23 na haohao (watuhumiwa) ndiyo wako moto kweli kutafuta suluhu DRC.Ati wanajifanya kuratibu mazungumzo kati ya Waasi na Serikali ya Kinshasa. Kweli kuna suluhu hapo? Si kutaka kumtesa na kumbana Joseph Kabila kuishia kuruhusu nchi kukaliwa na waasi hawa?
Ninachoshindwa kuelewa ni kitendo cha JK kuafikiana na akina Museveni na leo ghafla anaingia makubaliano mengine na SADC tena yenye kutengua makubailiano ya Kampala. Je JK hakuona tatizo katika maazimio ya Kampala? Alizidiwa nguvu na akina Kagame? Maswali ni mengi hapa.
Museveni meets Russian President Vladimir Putin
By In2EastAfrica Reporter
President Yoweri Museveni has held talks with the Russian president Vladimir Putin at the Novo-Ogaryovo state residence outside Moscow.
Russias President Vladimir Putin (R) meets with his counterpart Yoweri Museveni at the Novo-Ogaryovo state residence outside Moscow December 11
Wapeni Congo nafasi waje waletee vijana Wao waje kufundishwa kuwa wanajeshi thabiti mbona wakati wa nyerere swapo na ANC walileta Askari hapa . Let us consolidate our position, we can make a difference