Ninafikiri ni uzushi. Kama sio uzushi, basi Mhe Dkt JK kazi anayo! Rais wa nchi, waziri wa mambo ya nchi za nje huyo huyo, waziri wa mazingira na tabianchi huyo huyo, mkurugenzi wa kitengo cha tabianchi huyo huyo! Kuna haja ya Katiba Mpya kuweka kwa uwazi ni mikutano ipi, makongamano yapi , na semina na warsha zipi Rais (simaanishi JK, namaanisha Rais wa JMT) anastahiki kuhudhuria sio kwa nia mbaya au wivu wa kike bali kulinda hadhi ya urais wa JMT!