Jk atapata wapi ‘watakatifu’ wapya?

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
RAISJakaya Kikwete anakabiliwa na mtihani mgumu. Ana jukumu zito la kuchekecha upyamiongoni mwa wabunge wa CCM kupata “watakatifu” wapya.
Hiini baada ya “watakatifu” wake wa awali kutikiswa. Wametuhumiwa kwa wizi, ubadhirifuna kushindwa kutekeleza majukumu yao. Kwa maneno machache wameonekanawanamwangusha aliyewateua.
RaisKikwete alipochekecha miongoni mwa wabunge wa chama chake baada ya uchaguzi wamwaka 2010, alipata wateule wake takriban 47. Bila shaka aliona wenginehawatoshi kuvaa viatu vya uwaziri, hadi akaamua kuchukua kwenye akiba yake.
Ilikuziba pengo la “watakatifu” lililojitokeza, Rais Kikwete kwenye mkoba wake wapembeni aliwateua Profesa Makame Mbarawa na Shamsi Vuai Nahodha kuwa wabunge,ili kujazia baraza lake.
Hizizilikuwa dalili tosha kuwa kwenye kapu la wabunge wa kuchaguliwa na vitimaalum, “watakatifu” walikuwa wamekwisha hadi akachukua nje ya bunge. Hii simbaya, kwa kuwa katiba inamruhusu kufanya hivyo.
Sasakibao kimegeuka. Wale aliowaona “watakatifu” wakati ule wamechafuka. Wamejaatuhuma na baadhi yao wametajwa hadi bungeni kuwa ni wezi. Wananchi hawawaaminitena. Wabunge wenzao wamewakataa, wanawalazimisha wajiuzulu, si hivyo bosi wao,Waziri Mkuu Mizengo Pinda aachie ngazi.
Mawaziriwanaotuhumiwa ni Mustafa Mkulo (Fedha), Cyril Chami (Viwanda na Biashara),William Ngeleja (Nishati na Madini), Omar Nundu (Uchukuzi), Ezekiel Maige(Maliasili na Utalii), George Mkuchika (Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEAMI),Profesa Jumanne (Kilimo Chakula na Ushirika) na Dk Hadji Mponda (Afya).
Tuhumadhidi ya mawaziri hawa zimeibuliwa katika ripoti za kamati za kudumu za bungeza Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Serikali za Mitaa (LAAC), na Mashirika ya Umma(POAC) zilizotokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Baadaya dalili kuonekana kuwa mawaziri wanaotuhumiwa wasingejiuzulu, hata baada yawenzao wa CCM kuwashinikiza, umeandaliwa mkakati mbadala wa kuwalazimisha –kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Tayarihoja imewasilishwa bungeni, ikiungwa mkono na saini za wabunge zaidi ya 70,kutaka ipigwe kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Kurahiyo ikipigwa, na zaidi ya nusu ya wabunge wakaiafiki, rais anaarifiwa nawaziri mkuu anaachia ngazi.
Wazirimkuu kuachia ngazi si kazi ndogo wala si mchezo. Ni jambo linalomaanisha kwambaBaraza la Mawaziri linakuwa limevunjwa. Kwa maneno mengine, serikali inakuwaimeanguka, isipokuwa rais peke yake.
Wabungewamefikia hatua hiyo baada ya kuona hakuna dalili za mawaziri hao kujiuzulu.Wameamua kuwashinikiza wafanye hivyo, au wajikute wako nje ya baraza, baada yawaziri mkuu kuenguliwa.
Pamojana tuhuma dhidi yao sasa, Rais Kikwete aliona hawa ndio “watakatifu” wakemiongoni mwa wengi. Inawezekana alifanya kazi hii mwenyewe, akachambua naniawemo na yupi asiwemo. Au alisaidiwa na vyombo vya dola vya kuchuja wateulewake.
Mawazirihawa wameshutumiwa waziwazi ndani na nje ya bunge. Wachache kati yaowamejitetea na wengine wamekaa kimya.
Penginehii ndiyo sababu Rais Kikwete amevuta subira akiwa safarini Brazil na baadayeMalawi, ili apate fursa ya kuchambua ili kubaini pumba ipi na mchele ni upi.Labda anachekecha kichwa kwanza, kuona ni wapi atapata “watakatifu” wapya ndaniya muda mfupi wa serikali.
Itakumbukwahata katika kipindi chake cha kwanza, alilazimika kuunda upya serikali baada yakujiuzulu waziri wake mkuu wa kwanza, Edward Lowassa na mawaziri wawili wenginekutokana na kashfa ya kushinikiza mkataba wa ukodishaji wa mitambo ya kufuaumeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond.
Mawaziriwaliojiuzulu pamoja naye ni Dk. Ibrahim Msabaha wa Afrika Mashariki na NazirKaramagi wa Nishati na Madini.
Haiingiiakilini kuona hata kabla ya miaka miwili kupita “watakatifu” wa Kikwetewanafunikwa na uchafu usiosafishika. Miaka miwili ni kipindi kifupi kwakiongozi msafi kubadilika na kuwa mchafu, hasa kama kuna usimamizi makini juuyake.
Kamatuhuma dhidi ya mawaziri hawa ni za kweli, ninashawishika kuamini kwambawateule hawa huenda walikuwa wachafu hata kabla ya kuteuliwa au itakuwa usimamiziuliopo juu yao ni legelege unaotoa mwanya kwao kuchafuka haraka.
Lakinipia, kama mawaziri hawa waliteuliwa wakiwa wachafu, napata mashaka kama nchiyetu ina vyombo makini vya kuchunguza watu na kubaini uwezo na udhaifu waokabla ya kupendekezwa kwa rais wateliwe, hasahasa kwenye nafasi nyeti kamauwaziri.
Wasiwasiwangu ni iwapo Rais Kikwete akichekecha tena kwenye “makapi” aliyoyaacha wakatiule, atapata watu wa namna gani, ikiwa “watakatifu” walimalizika mwaka 2010.
Nirais kusema ohoo bado wabunge kibao, au ukasema Watanzania ni wengi hadimilioni 45. Lakini nani asiyejua kuwa wananchi kwa sasa hawana imani naserikali yake karibu yote?
Naniasiyejua kuwa wabunge waliopo pia hawaaminiki kwa wananchi waliowachagua? Naniasiyesikia kuwa wabunge wengi ni wala rushwa na wengine walitoa rushwa iliwachaguliwe?
Aunani asiyejua kuwa wabunge wengi walifadhiliwa na matajiri wachafu ili kupatanyadhifa walizonazo? Hivi ni nani asiyejua kuwa mtu yeyote aliyetoa rushwakupata ubunge, akipata nafasi ya madaraka kipaumbele chake ni kurejesha fedhaza waliomwingiza madarakani?
Tukiola karibuni la rushwa iliyokithiri kwa wabunge wakati wa mchakato wa kuwaniaubunge wa Afrika Mashariki na mwaka jana wakati wa sakata la aliyekuwa KatibuMkuu wa Nishati na Madini, David Jairo la kutuhumiwa kuhonga wabunge iliwapitishe bajeti ya wizara hiyo, ni mifano michache ya uchafu wa wabunge.
Kutokanana uchafu huo, hapana shaka ni kazi ngumu kwa Rais Kikwete kupata “watakatifu”wapya. Kitakachosaidia, ni “mkoba” wake aliopewa na katiba, ambao bado unanafasi saba za kuteua wabunge.
Kwamujibu wa katiba, Ibara ya 66 (1) (e), Rais Kikwete anazo nafasi 10 za kuteuawabunge. Ametumia tatu kwa kuwateua Nahodha, Profesa Mbarawa na Zakia Meghji.
Bilashaka atalazimika kuingia kwenye mkoba huo kutafuta Watanzania wengine wenyeuwezo ili awateue kuwa wabunge na baadaye mawaziri, vinginevyo itakuwa vigumukwake kupata “watakatifu” wapya.

 
Back
Top Bottom