JK atakumbukwa kwa tatizo la umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK atakumbukwa kwa tatizo la umeme

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JOHN MADIBA, Jun 29, 2011.

 1. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Suala la umeme ni miongoni mwa ahadi kadhaa wa kadhaa zilizotolewa na Rais Kikwete wakati wa kampeni zake mwaka 2010 kuwa atahakikisha nchi haiingii gizani, umeme utawaka kwenye makao makuu ya wilaya zote na nguvu zaidi zitaelekezwa vijijini kupitia mradi wa maendeleo ya usambazaji umeme kwenda vijijini.

  Hizo zote ni ahadi na zilikuwa ahadi nzuri zilizopigiwa makofi na wananchi wengi ambao hawajawahi kuwasha taa za umeme tangu nchi hii ilipopata uhuru na hawana njia mbadala ahadi siku zote ndizo zinazowapa matumaini kuwa jambo fulani litafanikiwa kutokana na kauli iliyotoka kwenye kinywa cha kiongozi wa nchi.

  Kwa maana hiyo watanzania hawadanganywi na hawakudanganywa kuwa tatizo la umeme litabaki kwenye historia isipokuwa walijengewa matumaini mapya kuwa hakuna mtu atakayekuwa anapigia kelele umeme, kila kona utakuwa ukiwaka kwa saa 24.

  Sasa tatizo la umeme ndani ya miezi sita tangu rais alipoapishwa kushika gidamu za nchi haliepukiki, mgawo wa umeme unakuwa wa kihistoria, malengo ya kufikisha nishati hiyo hadi vijijini inageuka ndoto na watu wa mijini wanashindana kununua ‘TOCHI’ za Mchina ili kupata mwanga.

  Adha, ya umeme inavuruga vichwa vya watanzania kwa kiasi kikubwa na inawezekana kabisa tatizo hili ni baya na sugu pengine kuliko vipaumbele vingine ambavyo kwa fikra sahihi hakuna haja ya kuvikumbatia lakini suala la umeme halipaswi kuchezewa.

  Nchi yenye matatizo ya umeme ni sawa na ‘Mtu mfu’nchi inakufa kiuchumi na haiwezi kuendelea kama kwa kiwango kikubwa namna hii kunakuwa na tatizo lisilokwisha, mgawo wa umeme ni taswira mbaya na unaonyesha wazi ukomo wa utawala ulioshindwa kufanya kazi.Rais Kikwete utakumbukwa kwa lipi,ili uweze kuacha kumbukumbu nzuri kwa watanzania na kamwe wasije wakakusahau milele fanya jambo moja kubwa na la muhimu,serikali yako ifanye iwezalo ili kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linakwisha kabisa, mijini na vijijini.

  Nchi hii ni kubwa na hatuna sababu ya kulalamikia ukubwa wake kwa kuwa kila kona kuna vyanzo vya umeme, uwe wa maji, mkaa, upepo na vingine vingi, utakumbukwa kwa kuamua kwa uwezo wako madhubuti kuwa mambo mengine yaendeshwe kwa viwango vya kawaida ili tatizo la umeme likome.

  Tatizo la umeme linaweza kusababisha historia ya kiongozi mzuri kiutawala ifutike na nashauri historia ya CCM na serikali yake inaweza kufutwa endapo tatizo la umeme litashindwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu, hili ni tatizo na ni tatizo sugu, Rais wangu Kikwete.
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Kwakua tatizo la umeme halikuanzia wakati wa utawala wa JK, nitamkumbuka kama kiongozi aliyetumia tatizo la umeme kujinufaisha yeye na marafiki zake wa karibu na kushindwa hata kuonyesha nia ya kulitatua.
   
 3. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jk anapaswa kuiondoa aibu hii aliyoileta tanzania alidhani urais ni kucheza bao uswahilini chalinze
   
Loading...