JK asisitiza barabara na uwanja wa ndege kujengwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK asisitiza barabara na uwanja wa ndege kujengwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Jul 5, 2010.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  4th July 10
  JK asisitiza barabara na uwanja wa ndege kujengwa

  George Marato

  Rais Jakaya Kikwete, amesisitiza kuwa miradi ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mugumu na barabara ya Lami kutoka Makutano wilayani Musoma hadi Mto wa Mbu mkoani Arusha lazima ijengwe.
  Rais Kikwete, alisema hayo juzi mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara, muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa maji wa Bwawa la Machira lilojengwa na serikali kwa zaidi ya sh. bilioni 10.2.
  “Kuna propoganda kwa wenzetu wa nchi jirani kuandika habari magazetini za kuzuia ujenzi wa kiwanja hiki cha ndege eti kikijengwa kitachangia Nyumbu kuharibu mamba, hiyo ni sayansi ya wapi…uwanja huu unajengwa, lazima ujengwe ili kusadia kuongeza watalii na kurahisisha mawasiliano pia kuchangia ukuaji wa uchumi, hayo maneno yao kamwe hatuwezi kuyasikiliza,”alisema Rais Kikwete na kushangiliwa.
  Kuhusu ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutoka Makutano - Musoma kupitia Mugumu hadi Mto wa Mbu mkoani Arusha, Kikwete alisema lazima barabara hiyo ijengwe pamoja na kuwepo maneno mengi kujitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.
  “Ahadi yetu ni kujenga Barabara hii na ahadi hii iko pale pale kuna maneno mengi yamesemwa kuhusu ujenzi wa barabara hii lakini nasema lazima ijengwe kitakachofanyika ni kuacha kuweka lami katika kilometa 50 tu ambazo ziko ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti lakini maeneo mengine yote yatawekwa lami ili wananchi wanaoishi nje ya hifadhi pia waweze kunufaika na barabara hiyo,” alisema.
  Hata hivyo, alisema miradi hiyo itatekelezwa kulingana na uwezo wa fedha kama ilivyoahidiwa na Serikali ya CCM na baada ya kukamilika itachangia ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo ya wananchi wa maeneo husika.
  Rais Kikwete alitumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio mbalimbali ambayo yamepatikana kwa serikali ya awamu ya nne katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
  Alisema hivi sasa Serikali yake inaandaa mpango wa ujenzi wa chuo kikuu kingine kikubwa baada ya kile cha Dodoma na wakati ukifika azma hiyo itatangazwa rasmi na ikiwezekana kwa asilimia kubwa chuo hicho kitajengwa mkoani Mara.
  Kuhusu ombi la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, Rais Kikwete alisema tayari serikali imeanza kutenga fedha za ujenzi wa hospitali hiyo huku akiutoa hofu uongozi wa kanisa la Menonite ambalo hospitali yake hivi sasa inatumika kama teule ya mkoa wa Mara kuwa pamoja na ujenzi wa hospitali hiyo lakini Serikali itaendelea kutoa mchango wake kwa hospitali hiyo kama ilivyo hivi sasa.  JK asisitiza barabara na uwanja wa ndege kujengwa
   
Loading...