babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,426
- 3,308
HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amekamilisha kuunda safu mpya ya wajumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho ambayo mwaka jana alishindwa kuiunda mjini Dodoma, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
Habari kutoka ndani ya chama hicho tawala zilisema kuwa, Rais Kikwete anatarajia kuwatangaza wajumbe hao wapya Februari mjini Dodoma wakati wa kikao cha kwanza cha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya CCM, vilisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa Rais Kikwete kupata wajumbe hao, ndiyo maana alihitaji muda mrefu aweze kuwajua ili kuepuka kufanya uteuzi wa sura na majina yaliyozoeleka.
Kwa mujibu wa habari hizo, CC hiyo ina baadhi ya sura mpya na uteuzi wake umezingatia uwakilishi wa mikoa, hasa Kanda ya Ziwa ambayo safari hii haina hata mjumbe mmoja wa sekretarieti.
Kuna sura mpya, zipo pia sura zilizozoeleka, lakini baadhi ya mawaziri waliotupwa kwenye uteuzi wa Rais Kikwete mwaka jana, wamo kwenye Kamati Kuu, kilisema chanzo chetu cha habari.
Mara baada ya kuteua sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana mwaka jana, Rais Kikwete alishindwa kuunda Kamati Kuu.
Rais Kikwete alisema anahitaji muda zaidi kuwajua baadhi ya wajumbe wapya wa NEC ili kuepuka kuteua majina na sura. zilezile.
Nimewaomba wajumbe wa NEC wanipe muda kidogo wa kufanya uteuzi wa wajumbe wa Kamati Kuu, kwa sababu tuna wajumbe wengi wapya ambao nahitaji kuwajua kwanza, alisema Kikwete wakati akizungumza na wajumbe wa NEC mjini Dodoma.
Katika uteuzi wake huo mpya wa sekretarieti, Kikwete alimtupa nje aliyekuwa Katibu Mkuu, Wilson Mukama na nafasi yake kutwaliwa na kada mkongwe na mzoefu, Kinana.
Aliwateua wajumbe wapya wanane, wakiwamo wanawake wawili, Zakhia Meghji, ambaye amerithi mikoba ya. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, anayekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, hivyo kumtupa nje, John Chiligati, aliyekuwa akishikilia wadhifa huo.
Mwanamke mwingine aliyechomoza katika sekretarieti hiyo mpya ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, ambaye anavaa viatu vya Januari Makamba, kwenye nafasi ya Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje.
Makamba ameachwa ili abaki na nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Hata hivyo, kitendo cha Kikwete kumuingiza Dk. Migiro kwenye sekretarieti na kuwa mjumbe wa NEC na CC, kimetafsiriwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni kumjengea mazingira ya kuwania urais mwaka 2015.
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar imeendelea kushikiliwa na Vuai Ali Vuai, huku Nape Nnauye, ameendelea kushikilia nafasi yake ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, ambayo ameonekana kuimudu vema
tangu alipoteuliwa.
Mohammed Seif Khatib, amekuwa Katibu wa Oganaizesheni, ambayo awali ilishikiliwa na Asha Abdallah Juma, ambaye safari hii ametupwa nje.
Mohamed Seif Khatib na Kinana wanaingia kwenye Kamati Kuu (CC), kutokana na nafasi zao.