JK anafahamu vizuri neno "Masoko ya Mitaji?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK anafahamu vizuri neno "Masoko ya Mitaji?"

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mwana wa Mungu, Nov 22, 2009.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jamani, hivi JK amesomea uchumi kweli, mbona hana akili? siku zote akiongelea mambo ya kiuchumi huwa anaboronga mbele za watu na kututilia aibu. Sasa jana anaposema kuwa kwenye soko la Africa, ame include transferability ya masoko ya mitaji, halafu akaeleza kuwa, sasa wakenya au watanzania wanaweza wakaleta mitaji hapa nchini au sisi tukapeleka kule kwao, akiwa anamaanisha kuwa, ni mtaji kama wa kuanzishia biashara hivi, yaani chukua fungu la pesa la kuanzishia biashara nenda nalo kenya kaanze biashara. huo ndo uelewa wake kuhusu masoko ya mitaji.

  Mimi pamoja na kwamba sio mwanauchumi, naelewa sana masoko ya mitaji. nilifikiri mkuu wetu angeongelea vizuri kuhusu mambo ya share/stocks, bonds za selikali pamoja na corporate bonds, futures and securities zingine, pamoja na kuunganisha Dar stock exchange na zile za Nairobi na Kampala etc. yeye akasema unachukua mtaji na kwenda kuanzisha biashara kenya ndo biashara ya mitaji hiyo, na anaongea mbele ya kadamnasi, ya wana east africa..hahaha. hivi wenzangu mlimwelewa huyu jamaa?
   
 2. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,049
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Huu ni udaku au HUKUMUELEWA VIZURI.Mods plzz ipeleke huko kwenye udaku au tuoneshe source.
  JF ni jukwaa la great thinkers mambo ya kidaku yanaanza kushusha hadhi yetu especially udaku wa kibinafsi kama huu......ndio hio.
   
 3. M

  Mundu JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mwenye habari nzima aliyosema JK aiweke hapa, ili tuitazame kwa kina. maana maneno yameshaanza, mara oooh hii habari ipelekwe kwenye udaku, mara ooooh fulani hajui maana ya soko la mitaji. Sasa lipi ni lipi?
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mbona nina muelewa.
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Usiwe ni mwenye kucritisize kila kitu tena kwa kumuita mtu mjinga wakati wewe ndio umeonyesha ujinga wako. Ungeliweka swali inamaanisha nini ili tukusaidie. Hapo hakuna tatizo. Unakumbukumbu na wakati ile kampuni ya safari ilivyoaka kufloat share Tanzania, what happened?
   
 6. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Get into your head that JK au president yeyote yule haendeshi nchi kwa kutumia degree aliyosemea...bali anongea kile ambacho wizara na wasahuri wake walivyo-summarise.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  pumbavu kabisa..hutazami habari unaanza kuleta urguments za kitoto hapa.JK kasema kwenye hotuba yake pale Sheikh Amri Abeid kuwa masoko ya mitaji yataunganika...in short JK haelewi anachoongea na huo uchumi aliosoma ni ule wa supply and demand,demand curve na demand schedule..hawezi kuelewa mambo kama haya.we hukumuona Kibaki anacheka
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo waki summarize upumbavu naye atalipuka na kuongea upumbavu au?
   
 9. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  true lakini ukiwa msomi upumbavu wa washauri una uona hivyo ni muhimu kumchagua kiongozi makini na mwenye pasavyo hili haendeshe. Si ajabu amna physicians into politics. Kwa sababu utalaamu wa jamii hawana.

  Hivyo ni useless tu wala si washauri wake.
   
 10. b

  bnhai JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hebu weka argument hapa. Kosa ni lipi? Huna sababu ya kutukana. Very likely wewe ndio huelewi nini kinachozumgumzwa. Punguza matusi weka hoja. Nini sio sahihi hapo?
   
 11. b

  bnhai JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Tungependa tuuone huo upumbavu. Km unakumbuka vyema kampuni ya simu ya Kenya ilishindwa kuuza hisa zake kwenye soko la Tanzania kutokana na sheria zilizopo. Huoni kuwa integration itafanya waweze kuuza? Huko si kuunganika? Unless una argue vingine, ni vyema ukaonyesha kosa si kashfa na matusi.
   
 12. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Si vizuri kutoa matusi kwa rais, na hasa kwa kitu ambacho hata wewe mwenyewe hukijui. Tafuta wasaa usome kuhusu stock exchange zinavyo fanya kazi kabla ya kukurupuka kwa jambo usilolijua.

  Kwa taarifa yako Rais hatoi hotuba kutoka kichwani kwake mara zote hotuba huandaliwa na jopo la wataalam.
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mwana wa Mungu, Yawezekana kabisa una hoja ya msingi kutokana na yaliyojiri. Ila kwa kweli lugha unayoitumia kwenye jukwaa la uchumi dhidi ya Mh. Rais haifai. Hapa ni pahala pa kujulishana ukweli wa mambo, kuelezana na kufafanuliana mambo ya kiuchumi na maendeleo kadiri ya jinsi mtu unavyoelewa. Lakini kuanza tu kwa kumuita Rais ni mjinga, haileti ladha yoyote ya maana kwenye mjadala huu bali inaufifisha na kuonekana umekaa kisiasa na kimajungu badala ya kiuchumi.

  SteveD.
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ninawaelewa, naomba muelewe kuwa, kumuita mtu mjinga, manake haelewi anatakiwa aeleweshwe. kuna kitu kikubwa sana napata hapa, kwamba, wakati rais anaongea, watu huwa hawawi makini kusikiliza point, hasa pale anapoongea mbele za watu kutuwakilisha watz. wengi hapa wanakuja na kusema kuwa mimi sijui masuala ya stock exchange, kwa kifupi, mimi ni mdau, na ni mtaalam sana wa ulimwengu huo hapo. niliandika kama siko huko ili kupata tu mawazo yenu. nashangaa kwamba mnamtetea rais wakati alichemsha, na sio kitu cha kwanza kuchemsha kwa huyu rais wetu. mara zote rais akiongea kwenye majukwaa ya kimataifa, lazima utashindwa kumuelewa kama alijiandaa au vipi, anasomaga vitabu au la, ana uelewa mzuri au la, hakika utashindwa kumuelewa.

  point yangu ilikuwa ni hii. siku ile alipokuwa anaongea, aliongea akimaanisha kuwa, kuhamishika kwa masoko ya mitaji, yaani capital markets, ni kuhamisha mitaji ya pesa, sio shares/stocks hizo unazofikilia, sio corporate bonds wala bonds zinazotolewa na selikali. alikuwa hamaanishi kufanya biashara kwa kuunganisha stock exchange za kampala, nairobi na Dar etc. aliongea kwa kutokuelewa anachoongea akimaanisha/akielewa kuwa labda huwa inakuwa ni kuhamisha mitaji kama hii ya maduka ya wachagga na wakinga yaani akina mangi, au makampuni ya biashara ya uwekezaji kwenda kuwekeza (si kwa njia ya hisa)bali kwa njia ya kufungua biashara za kawaida kule. alikuwa anamaanisha wabongo wanaweza wakaenda kuwekeza (si kwa kutumia soko la mitaji) kenya na nchi zingine, na wakenya na wengine wanaweza kuja kufanya hivyo hapa. huu ndo uelewa aliousema.

  tatizo hapa, si kuwekeza, tatizo hapa ni mwanauchumi kutokuelewa maana ya capital markets and securities na ufanyaji biashara wake. hata kama atakuwa ameandaliwa taarifa kuongea, anatakiwa basi aipitie ili asichemshe. haoni marais wenzie wanaongea bila hata kuangalia sehemu lakini wanaongea vitu material vitupu? hivi mnafikiri tz hakuna wenye akili zaidi ya hawa wanaotuongoza bila kujua wanafanya nini?

  cha ajabu, watu wengi, sijui wamesoma degree za history huko, wengine degree za kilimo, sijui wengine za kiingereza, tukiongea kitu kama hicho, wanawaza tu walichosikia kwenye magazeti kuhusu hisa za safari com ya kenya. nothing more than that. ukiona jambo haulielewei, hasa kwahabari ya darasani, waachie wale waliosomea hilo jambo walijadili, wewe ishia kuuliza maswali tu. nampa pole jk, nawapa pole watz kwasababu tunaongozwa na watu wasio na uelewa wa kutosha, wamesafisha tu nyota bagamoyo huko ili wapendwe na watu ila hamuna kitu bwasheee!
   
 15. b

  bnhai JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  This is very low. Honestly huna utaalam wowote. Maana kama share zinahama inamaana na pesa zinahama. Huelewi unachotaka kukisema kabisa. I am ready to help you with the knowledge kama hutajali. Maana wewe ndio hujui kabisa. Tumekutolea mfano wa Hisa. Go back and read liberalisation na Intergration ya Capital markets. Inasikitisha umerudisha hii thread ungeiacha ife taratibu.
  Angalia allegations zako, eti watu wamesoma degree za history nani kakueleza? Huo ndio ujuvi wa Soko la Hisa. Inawezekana wewe ndio hukumuelewa kabisa.
   
 16. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Yeye bado anaamini kwamba alichosikia kilielezwa visivyo. Haitakuwa sahihi kumnyima fursa au ulingo wa kueleza dukuduku lake.

  Naona mmeanza kutukanana. Bnhai, wewe hiyo hotuba uliisikia au kuisoma? Ni vyema mkajadili hicho kilichosemwa, kuliko malumbano ya nani anajua nini. Mambo ya degree za history sijui yanatoka wapi.

  Mwana wa Mungu, tutafutie hiyo hotuba utuwekee hapa, itasaidia wengine kukuelewa. Usipoangalia utavunja keyboard yako bure!
   
 17. b

  bnhai JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  LazyDog hebu soma post yake vizuri uone hiyo degree ya history nani kaizungumza? Rudi nyuma kidogo nadhani ndiyo utaona kejeli. Binafsi nimeoffer kushare naye knowledge. Maana anasema ni mtaalam. Kajaribu kuielezea hotuba hapo juu. Can you go through it? Unaujua likija suala la kitaalam hebu siasa zikae kando. Ndio maana tunapatikana kwenye hii category ya business. Mwana wa Mungu inawezekana anataka kusema kitu. Lakini nina mashaka km anafaham hasa kuhusu masoko ya mtaji. Labda nimkumbushe Kikwete alivyopata madaraka alikwenda kwenye soka la Hisa la Marekani. Sasa umbumbumbu wa kuunganisha na yale ya kina Mangi inatoka wapi. Pamoja na mapungufu yake pale kwenye ukweli lazima usemeke.
   
 18. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ni ajabu kuwa jamaa haunielewi. ungeniacha nikueleze ndio utoa koment kama hizo. actually, kila mtu alikuwa anategemea jk kuongea vizuri mbele za watu, kugonga nyundo kule wall street siku ile sio sababu kuwa anafahamu kitu. ongea point. nitaleta hotuba nikiipata. ila nakushauri, uwe unafuatilia hotuba za huyo mshikaji wako. utaweza kumsaidia labda.

  kila mtu alikuwa anategemea kama anaongelea mambo ya stock exchange, angeongea katika lugha ya kiuchumi, kwasababu yeye mwenyewe amesoma uchumi. wengi tulitegemea kuwa angeongelea namna ya kuliunganisha vizuri soko la hisa afrika mashariki, kwa kurekebisha sheria hasa za uingiaji kwa mara ya kwanza kwa makampuni yetu ili yawe listed kwenye DSE. sheria ya mwaka 1994 ina ukiritimba kidogo ndio maana hata hisa za NMB na zingine watu wakenya na waganda walipata shida kidogo. pia makampuni ya kenya siyo yote yanaweza kuwa listed DSE. kuna vitu vingi. urekebishaji wa sheria, na pia kuyahamasisha au kuyawezesha makampuni ya tz kuwa listed dse ilikuwa muhimu.

  uelewa wako mkuu sijauelewa vizuri. ni kweli kama hisa zitahamishika kwenda nchi zingine za EA, ndo kuhama kwa mitaji huko,hivi kuna mtu asolijua hilo?. lakini jamaa yako hakumaanisha hivyo, nafikiri walimwandikia aongee hivyo lakini yeye hakujua namna ya kuongea vizuri kwasababu kichwani kwake hakikuwapo kitu. zaidi ya yote, alipoongea hii point, ilionyesha kuwa haikuwa imeandikwa kwenye karatasi, ili kuwa ni nyongeza tu aliyoitoa kichwani kama maelezo binafsi ya kwake kabla ya kuendelea kusoma. bahati mbaya akachemsha.

  ni muhimu sana kumsikiliza mtu anachoongea, sio kuangalia tu uso wake. wengi hasa wewe, kazi yenu ni kusifia tu mtu, wakati anachemka na nchi anaipeleka bondeni. wengi wame critisaizi yale matamshi yake. NINAAHIDI kuwapatia faul nyingine ili mumuelewe huyu jamaa yenu mpenzi. asateni.
   
 19. b

  bnhai JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Katika post zote kwenye mjadala huu post hii umeiandika vizuri na umeonyesha uelewa. Na hii ndiyo namna ya kuargue. Kwenye hiyo nyekundu nakubaliana na wewe. Let take a simple scenario. Investor from country A ameona opportunity country B kutoka na regulations au IPOs. Sasa ameamua kuuza share zake huko country A na kununua kule country B kutokana na kuwa kuna company inakuwa listed au inapeform vizuri. Kitendo hiki ndio kuhamisha mtaji. Kwenye maelezo yako unasema wengi mlitegemea angeongelea namna ya kuliunganisha soko, kwahiyo tatizo hakuongea ulichotaraji au alikosea? Pia unakumbuka audience ya Rais inahusisha watu wa aina gani? Ile sio proffessional gathering pls. Rais anatakiwa aeleweke. Mwisho mie sina ubia na JK na hanifaham kabisa ninachofanya ni kuhakikisha ukweli unaelezeka. Sasa nadhani tumekubaliana mh Rais hakukosea bali hakuongea kile ulichopenda kukisikia. Nashauri title ya thread iwe edited.
   
 20. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote, punguza jazba mkuu! hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kufurahi kuambiwa "hana akili", seuze president ambae hata wewe una wajibu( wajibu wa kikatiba) wa kumuheshimu?! Hata Lipumba( na wengine kama yeye), pamoja na upinzani wao kisiasa, hawezi kusema JK hana akili!! if u want 2b respected, u have to learn how to respect ur self! Tukija kwenye hoja, JK ana akili zake timamu, hawezi kuzungumzia masuala ya stock markets wakati the only DSE lililopo ni the weakest market!! kivipi azungumzie masuala ya stocks wakati hizo kampuni zenyewe tulizonazo haziwezi ku-qualify hata kuingia DSE? wht the in NSE kwenye corps abt 50? naamini alichotaka kueleweka ni suala la free movement of capital(money&equipments). Si kwavile una mihela, ndo basi unaweza kwenda kuwekeza popote, lazima kutakuwa na barriers. Nazani alichomaanisha, ni ama hizo barriers zimeondolewa au kupunguzwa kwahiyo kama una mtaji wa kutosha, na soko lako limekuwa saturated, then u have the room to look for other investment opportunities outside ur country. kwa maana nyingine, ni kama kawa-encourage wakenya wazidi kuja kuwekeza na kama wewe unahisi huwezi kwenda kuwekeza mahali kama kenya, basi jitahidi ufike hata burundi. Kwani mkuu ww hujui kwamba serikali ina-trade bonds ili ipate mkwanja na yule anayenunua anafanya hivyo ili apate interest(among other things)? sasa kwanini awa-encourage the rest of EA kuja kununua bonds wakati bonds hizo ingekuwa biashara tosha kwa kampuni zilizopo TZ? Take a deep breath, JK yupo sahii kuzungumzia suala la mitaji(capital) badala ya soko la mitaji(capital markets)
   
Loading...