JK ana taarifa za mgomo wa madaktari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ana taarifa za mgomo wa madaktari?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Feb 6, 2012.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 477"]
  [TR]
  [TD]
  [FONT=&quot]Sauli Giliard
  Tanzania Daima
  [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&quot]SINA nia ya kukuchekesha msomaji wangu lakini nimekaa nikawaza kisha nikadhani kuwa yawezekana Rais wetu Jakaya Kikwete, hana taarifa kama madaktari nchini wako kwenye mgomo kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Sijui kama rais anajua kuwa huduma za matibabu kwenye hospitali kubwa ikiwemo ile ya Taifa Muhimbili zimesimama, wagonjwa wamekosa huduma na kujiondokea wodini huku wananchi wake wengi wakipoteza maisha kila uchao kutokana na mgomo huo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Narudia, wala sifanyi mzaha, yawezekana rais hana taarifa kama hawa watumishi wa sekta ya afya wamegoma wakishinikiza kuboreshewa masilahi yao. Sina hakika kama wasaidizi wake wanamweleza ukweli kuwa wapiga kura wake wanakufa kwa kukosa huduma hospitalini.[/FONT]
  [FONT=&quot]Lazima tukumbuke kuwa wakati vuguvugu la mgomo linaanza, Rais Kikwete alisafiri kwenda mjini Davos Uswisi kutuwakilisha kwenye mkutano wa dunia wa kichumi, na alipotoka huko akaunganisha kutuwakilisha kwenye mkutano mwingine wa Umoja wa Afrika kule nchini Ethiopia.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Rais wetu Kikwete, aliporejea nchini juzi, alikuta amepangiwa majukumu mengine ya kuzindua benki ya wawekezaji na siku iliyofuata akawa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mahakama, halafu huyo huyo leo anapaswa kuwa jijini Mwanza kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya Chama chake cha Mapinduzi (CCM).

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa hiyo ndugu msomaji lazima utakubaliana na mimi kuwa kiongozi wetu alikuwa ametingwa na majukumu mengine mazito, hivyo ilikuwa vigumu kwake kupata muda wa kukaa na madaktari na kuwasikiliza ama kufika katika baadhi ya hospitali kujionea hali halisi ya vifo na huduma hafifu za wananchi ili kujua hatua za kuchukua.[/FONT]
  [FONT=&quot]Lakini kama ilivyokuwa kwa Rais Mwai Kibaki wa Kenya, kuachana na safari ya Uswisi na badala yake akamtuma Waziri Mkuu wake, Raila Odinga, ili yeye aendelee na majukumu mengine ya kuwatumikia Wakenya, ndivyo hata Rais Kikwete alimwachia Waziri Mkuu Mizengo Pinda jukumu la kukutana na madaktari wakati yeye akiwa Uswisi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Sina hakika kama Pinda alimpa taarifa mkubwa wake wa kazi kuwa madaktari walimsusa kwa kutojitokeza kwenye mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika pale ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Vile vile sina hakika kama Pinda amemweleza Rais Kikwete kuwa aliwapa madaktari siku moja wawe wamerejea kazini, vinginevyo vibarua vyao vinaota mbawa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Sasa ndugu msomaji wala naomba usije kuniuliza amri hiyo ya waziri mkuu imefia wapi, maana madaktari hawajarudi kazini.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Juma lililopita niliandika kuhusu taswira ya viongozi tulionao nchini, nikijaribu kueleza kuwa kauli zao hazirandani kabisa na matendo yao. Hawa wanatuhubiria tunywe maji lakini wao wanakunywa mvinyo.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Binafsi kwa hali ya mgomo wa madaktari ulivyoendelea kushika kasi na kuwahangaisha wananchi, nilitegemea kusikia rais wetu amekatisha ziara ya Uswisi na kurejea nchini mara moja kujaribu kukaa na wasaidizi wake kuona ni jinsi gani wanaweza kuupatia ufumbuzi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hili si jambo la kushangaza kwa rais kukatisha ziara na kurejea nchini mwake hasa kunapokuwa kumetokea jambo la dharura, hili tumeliona sana kwa baadhi ya viongozi wa mataifa mbalimbali wakiwamo wa Bara letu la Afrika.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Ni ajabu sana hadi naandika makala hii, hakuna kauli yoyote kutoka Ikulu kwa mkuu wa nchi kuhusiana na mgomo huu. Zaidi tumesikia taarifa ya Ikulu ikimtakasa rais kwenye kauli tata kuhusu nyongeza ya posho za wabunge kutoka sh 70,000 hadi sh 200,000.[/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya kusikia na kusoma taarifa hiyo ya kumtakasa rais kuwa hakuwahi kuidhinisha posho hizo, nikashangaa na kujiuliza hivi ni kweli Ikulu imeona mjadala wa posho una umhimu sana kuliko tabu wanayoipata wananchi kwa kukosa huduma za afya hospitalini?[/FONT]
  [FONT=&quot]Ilinichukua muda mrefu kupata jibu sahihi lakini mwishowe nikabakia na nadharia yangu kuwa huenda Rais Kikwete hana taarifa kama madaktari wamegoma na hali ni mbaya kwenye hospitali nyingi nchini.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Lakini wakati naanza kujiaminisha hivyo, nikajiuliza swali kuwa mbona wakati anaondoka kwenda Uswisi vuguvugu likikwishaanza kwa madaktari wanafunzi ‘interns’? Kwamba baada ya kurejea si hata angeweza kuwauliza wasaidizi wake kama sakata hilo wamelimaliza?[/FONT]
  [FONT=&quot]Kweli tunayo serikali yenye viongozi wa aina yake, kama madaktari wanagoma na huduma zinasimama halafu wahusika wanapigana chenga kukutana na watumishi hao kuwasikiliza, basi hiyo ni hatari.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Hivi baada ya waziri mkuu kutoa amri ya kuwataka warejee kazini, vinginevyo wamejifuta kazi, mbona hatuambiwi ni madaktari wangapi wanastahili kuendelea kutumikia taaluma hiyo na wangapi wamefukuzwa?

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kama una akili timamu ebu kwa Jumapili ya leo jiulize swali hili, kuwa ikiwa watumishi wa sekta moja wamegoma kwa zaidi ya wiki mbili na serikali imeparaganyika, itakuwa kesho na kesho kutwa wakigoma walimu, askari, mahakimu na watumishi wengi[/FONT]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mods saidia kuhariri kwa kuondoka box katika story hii, asante
   
Loading...