JK aliingizwa mjini na NICOL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aliingizwa mjini na NICOL

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbalinga, Jul 13, 2010.

 1. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Habari nilizozipata hivi karibuni ni kuwa kumbe JK alidanganywa na maafisa wa NICOL na kwenda kufungua kiwanda cha samaki Mwanza na baada tu ya kufanyiwa usaini wa kuonyeshwa process ya kuakata samaki, kiwanda hicho hakikufanya kazi tena. DOH! jamaa yetu aliingizwa mjini.

  Na taarifa za hivi karibuni ni kuwa kiwanda hicho kiko chini ya mufilisi na kimetangazwa kuuzwa kwa kuwa wameshindwa kulipa deni la Bank (ABC). Sasa huu ni utapeli wa kupitiliza. Kwanza wamewatapeli Watanzania masikini kabisa wamekusanya pesa nchi nzima, halafu wakawekeza kisanii, halafu kana kwamba hiyo haitoshi wakamualika Raisi wetu mpendwa kwenda kuweka muhuri usanii wao.

  Haya jamani, wakifanya wahindi, ni mafisadi mapapa, je hawa waswahili wenzetu tutawaitaje?

  Kazi kweli kweli.
   
 2. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #2
  Jul 13, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,505
  Trophy Points: 280
  Tushamzoea huyo...
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Umefuatilia kwa nini hakikufanya kazi baada ya kufunguliwa na raisi? Walikosa mtaji wa kuendeshea, samaki au wafanyakazi?
   
 4. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Nimefuatilia sana, ni usanii tu uliofanywa, ili watanzania wadhani kuwa fedha zao kweli zimewekezwa. Nimefuatilia zaidi ya hapo na kugundua kuwa mwenyekiti wa NICOL na wenzake wachache walifisadi kiwanda toka wakati wa ujenzi. Haiingilii akilini kuwa mnawezaje kumuita Rais kufungua kiwanda hali mkijua kuwa hamna mtaji wa kuendeshea kiwanda. In fact baada ya Raisi kufungua tu ndipo wakaanza kuomba mkopo kwenye bank ya ABC. Kazi ya samaki inahitaji mtaji mkubwa sana, ABC wakawapa fedha kwa mafungu, na biashara ikawashinda.

  Labda baya zaidi ni uamuzi wa mzee Mosha wa kumwajiri Meneja Mkuu, raia wa India, na sisi watu wa Mwanza tunafahamu fitina ambazo wahindi wenye viwanda vingine wana vifanya. Kwa kifupi huyo meneja alinunuliwa ili kuua kiwanda, na baada ya kufanikisha alikimbia nje ya nchi. Sasa sijui kama JK anaambiwa mambo haya. Kama mimi mkuu wa nchi nisingekubali jina langu liishie kwenye kiwanda kisichofanya kazi.
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Tatizo haki za Watanzania haziko wazi sana. Nakumbuka kampuni ya kwanza kuandikishwa DSE ilileta mahesabu yenye sura ya ushawishi na wengi tukanunua hisa baadaye kumbe sehemu ya madeni yalikuwa hayalipiki hivyo wananchi wakawa tayari wamenunua hisa kwa bei ya juu ya thamani halisi ya kampuni, wataalamu waliohusika bado wanaendelea na kazi na hakuna mtu aliyedai fidia hadi leo. Nathani haw NICOL vile vile walichukuwa pesa hizo wakakopesha kiwanda mfu kule Moshi, nacho kiko katika hali muflisi.

  Hivi kwani nchi hairuhusiwi kuanzima sheria za nchi nyingine kama zake hazilete ufanisi? China wana sheria nzuri sana za kuthibiti wanahujumu mali za umma - Death Sentense
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huenda hivi ndivyo watanzania tulivyoooo..kutwaa kulalamaa lakini nafasi ikitokea (kama uanzishwaji wa NICOL) mambo huwaa hovyohovyo..

  sishangai NICOL kushindwaa kuendesha hicho kiwanda kwani hii kampuni hata CMSA wameshailalamikia kuwa ianendesha mambo sivyooo..wanatumia siasa na ule ujeuri wao wakujiona eti senior citzen!!! hawa wazee ni wasanii kuliko tunavyoweza kufikirii..

  kuanzisha investmet company na kuchangishaa hela za umma kupitia vipande inahitaji uwekezaji makini na uwazii katika kila jambo..

  muda si mrefu itaangukaa na watanzania tutagunduaa kwa nini biashara za kukamata uchumi twashindwaa..inaumaa..

  vijana wa leo tusiigee mbinuu mbovuu za hawa NICOL..
   
 7. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Najuta sana sana kwani mie ni mmoja kati ya wanahisa wa NICOL, nilinunua hisa hizo toka 28 juni, 2008. Hadi leo hii sijapata mgao hata wa senti moja, nasasa eti NICOL ni mufilisi, duu tumeibiwa.

  Hivi huyu Felix Mosha, duu kumbe nae ni bonge la fisadi, inatisha!!!
  Tunaiomba menejimenti ya NICOL itupe feedback sisi wanahisa mmoja mmoja.
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Uwekezaji wa pamoja ni changa la macho. Kwani say Dividend toka NMB iende NICOL - gharama za uendeshaji=gawio la wanaisa. Uwekezaji wa moja kwa moja Gawio toka CRDB=mwanahisa mmoja mmoja
   
 9. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walienda kununua kiwanda chenye deni kubwa mara baada ya kuingiza mtaji ,ukaenda kufidia benki, kumbe haikuwa hivyo matokeao yake wakawa bado wanadaiwa mojakwa moja wakaingia kwenye receivership, lakini naamini management walikuwa wanajua hilo, walifanya usanii ili wajinufaishe wao na familia zao
   
 10. M

  MJM JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Huo uwekezaji wa NICOL nayo ilikuwa kama upatu. Kwa nini Wadanganyika hamuendi kwenye makampuni yaliyo katika soko la hisa mkawekeza huko? Mnadanganyika mno.

  Huyu raisi naye kazidi na style yake kila kitu ni yeye tuuuuuuuu! Mawaziri anao lakini kila siku kafungua hoteli inayomega barabara, branch ya benki fulani, kiwanda fake kwa nini wasimpige changa la macho. Yeye size yake kabisa ila ndugu zangu wadanganyika poleni sana
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kama kiwanda tayari kilikuwa kinafanya kazi ufunguzi ulifanyika wa nini? Na walinunua "As a going concern entity" au "Assets i.e. outright sale" kwa maana kama ni Outright sale hawawajibiki kulipa madeni yaliyoachwa na mmiliki wa kwanza.
   
 12. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu ana NICOL financial yearly report ending 31st December 2009? natafuta jamani naona mwisho ni ya 2008!
   
 13. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  NICOL ilinunua majengo toka kwa Mzee Paul Bomani baada ya yeye kushindwa kuendesha, haikuwa Outright sale, baada ya kununua hilo jengo moja ndipo walipoanza kujenga na kuagiza mashine toka nje. Utashangaa ukisikia kuwa ujenzi ulifanywa kiholela mno, hakuna mkandarasi maalum aliyewekwa kujenga, Mosha na Mkurugenzi wa fedha wa NICOL walihamia Mwanza kusimamia ujenzi, mimi nilishuhudia huo usanii, sheria ya manunuzi ya umma haikufuatwa, walikuwa wao wenyewe wanakwenda kwa wahindi kununua vifaa vya ujenzi, wenyewe wanawasimamia wajenzi, ajabu leo hii ukienda kwenye hicho kiwanda utashuhudia mipasuko mikubwa ya kutisha. Nilibahatika kusoma management letter ya auditors 2007, tshs 200m/= zilipwa bila viambatanisho vyovyote. Ningeweza kuandika mengi ninayoyajua lakini inaniuma sana kama mwana hisa kuona kiwanda kimekufa kwa utapeli mtupu. Nina ushahidi wa maandishi jinsi hawa jamaa walivyowatapeli wadanganyika.
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Si ndio kawaida yaku huyo KIKWETE anapenda kweli kufanya mambo yanayomdhalilisha nchi nyingine angelazimishwa ajiuzulu kabisa kwa sababu hayuko makini kabisa,atafunguaje kiwanda kilichowaaibia wananchi,kweli Tanzania shamba la bibi na KIKWETE ndio mpiga filimbi kabla hajaingia kwenye uchaguzi ataiingizwa mjini tena na tena ,huyu ndie raisi wa miaka mitano ijayo kazi kwelikweli ,tuna mbumbu mzungu wa reli raisi wetu huyo
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Andika tuu tuyajue yote wala usipate kigugumizi,baada ya hapo wewe nawanahisa wenzako wenye mapenzi na nchi hii pelekeni kesi mahakama ya afrika mashariki au the hague ,hapa hamtaambulia kitu chochote watawaambia shauri yenu mulihiari wenyewe
   
 16. L

  Lorah JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  huyo Rais wenu kimeo, yeye kila siku anadanganywa tuuu,
  si ajabu alijua nini kinaendele huyu, Mbayumbayu imeishia wapi.....
  kwa nini lakini
   
Loading...