Elections 2010 JK alidanganya kuhusu Obama UN General Assembly?

Obama on Tanzania:

".......The United States will focus our development efforts on countries like Tanzania that promote good governance and democracy; the rule of law and equal administration of justice; transparent institutions with strong civil societies; and respect for human rights. Because over the long run, democracy and economic growth go hand in hand......."

Hizo karata tu. Kikwete msanii.

Hiyo paragragh LAZIMA kailipia.

Watapataje Tanzanite nauranium bila kumwaga sifa hata kama ni za kinafiki??
....Kailipia Paragraph?....
....By the way US kama wanakutaka watakusifia tu, na kama hawakutaki wataanza kukushupalia na mambo ya Human Rights....!!! Democracy etc...
 
Hivi alivyosema Balozi kampigia simu alikuwa ana maanisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania, au Balozi wa Tanzania nchini Marekani!! Nitamshangaa sana Balozi wa US Tanzania kumpigia simu JK kumueleza kuhusu paragraph moja ya hotuba ya Obama ambayo haina specifics!! I think kuna shida hapo
 
mwananchi quotes"akizungumzia ujumbe aliopewa kwenye simu na balozi wa marekani nchini, kikwete alisema kuwa amehakikishiwa misaada kuendelea kumiminika tanzania kutoka taifa hilo kubwa duniani

"nilikuwa nazungumza na balozi wa marekani nchini na amenieleza kuwa rais wa nchi hiyo, barack obama akiwa katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa alitolea mfano kuwa tanzania ni nchi inayofuata utawala bora hivyo wataendelea kutusaidia," alisema kikwete,

"maneno haya yanasemwa na wamarekani sio mimi... Watu wanasema tu marekani, marekani lakini huo ndio ukweli wenyewe; huo ndio ujumbe niliopata; wameonyesha kutusaidia na watatusaidia,".

OMBA OMBA jamani mpaka lini?....yaani rais mzima wa nchi anasifia msaada...jamani yaani tumekuwa vilema kiasi hicho?

Angalau ungesema ee wananchi vasco da gama wenu nimewafungulia line ya ku export to usa...lakini sio misaada na misaada yenyewe haifiki kwa walengwa.....pole sana nchi yangu Tanzania...
 
CCM a....li.. za kukopa hizi zitawaponza.Tz.kutajwa mara moja basi kama hotuba nzima ilikuwa kuhusu Tz. ametaja nchi nyingine pia za Africa. CCM mbona mnajikweza sana labda Obama alikuwa na maana UPINZANI unashamiri kwa kasi maana kwamba demokrasia ipo mahala pake sio kwamba CCM ndio chama kilichofanyia mema Tz. acheni kutudanganya wote tumeisoma na kuisikiliza hotuba yote sasa sijui mwenzetu JK yeye ana Speech Script tofauti na sisi.
 
Suala la Utegemezi usimlaumu JK, hilo limefanywa kuwa hivyo na the so called Super Powers!!!! kama hutaki utakiona cha Moto...!!!.

Mpaka leo tunaambiwa kuwa chanzo cha umaskini wetu ni ukoloni, lakini ukiangalia ukweli wa mambo utaona kuwa wezi na waharibifu wakubwa ni wale walioko madarakani leo na sio wale waliofukuzwa. Suala la utegemezi wa kujilaumu ni sisi wenyewe.

Obama anasema vitu kwa mijibu wa mashali ya sera ya mambo ya nje ya Marekani. Si kweli kama Tanzania kuna good governance (yes kuna elements) si kweli kama kuna rule of law (for sure kuna elements). Anatakiwa aje ajionee mwenyewe hali halisi ya Tanzania na sio kuambiwa tu na JK anapokuwa US.

We will now start to make it clear that US government is now conniving with our government to make our lives harder.
 
wajinga ndiyo waliwao...........je,watz ni wajinga kiasi hicho ndiyo maana tunaliwa na ccm?
 
sisi wa enzi zetu tunatunyimbo twetu twa kujifariji namna hii..."UONGO NA ULOZI NI WATU WA KUCHOMA"........kikwete ni muongo na mlozi kupitia kwa sheikh yahaya.........kwa hiyo ni mtu wa kuchomwa?
 
Soyry, kuna hotuba mbili: kuna hotuba aliyotoa tarehe 22 kwenye Millennium Development Summit na ile aliyotoa kwenye UN General Assembly tarehe 23. Hiyo ya tarahe 22 ni kweli aliitaja Tanzania isipokuwa hakusema kuwa tuna utawala mzuri kama Kikwete anavyodai ila alisema kuwa nchi zinazojitahidi kuwa na utawala mzuri kama Tanzania. Kujitahidi kuwa na utawala mzuri siyo kuwa una utawala mzuri.

Imaneiudhi zaidi kwa kiongozi kama Kikwete kutamba kuwa tutaenedela kupata misaada: ujinga gani huu jamani, yaani yeye anategemea kutawala nchi kwa kutegemea misaada?

mtu akianza kutumia mpaka mtamshi yasio endana na shughuli husika ili kuhalalisha jambo, kama wale marafiki zangu wa salamander/mkwepu street basi ujue ana shida kweli kweli, "makambozali minene" yaani mambo ni mazito/makubwa (maji yako mdomoni)
 
Hivi alivyosema Balozi kampigia simu alikuwa ana maanisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania, au Balozi wa Tanzania nchini Marekani!! Nitamshangaa sana Balozi wa US Tanzania kumpigia simu JK kumueleza kuhusu paragraph moja ya hotuba ya Obama ambayo haina specifics!! I think kuna shida hapo

inawezekana alikuwa anaongea na "wana familia" wake akasema alikuwa anaongea na balozi wa merekani, jamani hata mawasiliano binafsi watu wanayatumia kuwa haadaa wa tanzania? kama ilikuwa ni official aweke waze hiyo script/or voice message of the conversation si ina manufaa kwake na kwetu?
 
White House Press Release: A Video with English Subtitles: Titled:president Obama at Millenium Development Goals Conference:
  • Development Vision
  • What is development?
  • Ultimate goal of development
  • Food Aid dependency is not development
  • How to get people out of poverty
  • Fighting Corruption
  • Development that take the child and citizen out of poverty to prosperity
  • Not only achieving MDGs but exceeding them
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi kuwa JK alipokuwa kwenye ziara yake huko Ludewa, kabla ya kupanda kwenye jukwaa alipokea simu kutoka kwa balozi wa marekani nchini Bw. Alfonso E. Lenhardt. JK alidai kuwa balozi huyo alimwambia kuwa Rais Obama aliisifia Tanzania Kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufuata utawala bora.
Ni vizuri pale Rais kama Obama kutambua uzuri wa taifa letu, lakini inatia shaka kama Obama aliongelea Tanzania kuhusu utawala bora. Nilisikia akiongelea South Africa (From Tyranny to democratic reforms), Congo Kinshasa (Human rights abuse), Kenya (New constitution).

Je wapi Obama aliongelea utawala bora wakati kuna fisadiz wengine bado wanadunda. Je Kikwete alidanganya ili aonekane kuwa ni kiongozi bora na kujiongezea kura? Je ni kweli balozi Alfonso E. Lenhardt alisema hayo wakati Rais wake hakuongelea hiyo mada kwa Tanzania? Nani hapa alidanganya? na kwa nini?

MWANANCHI quotes"Akizungumzia ujumbe aliopewa kwenye simu na balozi wa Marekani nchini, Kikwete alisema kuwa amehakikishiwa misaada kuendelea kumiminika Tanzania kutoka taifa hilo kubwa duniani

"Nilikuwa nazungumza na balozi wa Marekani nchini na amenieleza kuwa rais wa nchi hiyo, Barack Obama akiwa katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa alitolea mfano kuwa Tanzania ni nchi inayofuata utawala bora hivyo wataendelea kutusaidia," alisema Kikwete,

"Maneno haya yanasemwa na Wamarekani sio mimi... watu wanasema tu Marekani, Marekani lakini huo ndio ukweli wenyewe; huo ndio ujumbe niliopata; wameonyesha kutusaidia na watatusaidia,".


Angalia video ujiridhishe. Karibu kwa maoni.
http://www.youtube.com/watch?v=1s7eHoRBqKI




ANGALIA HIYO VIDEO HALAFU MSEME MISAADA IPI?? halafu why tunakuwa watu w kuombaomba, sijawahi kuona TZ kama hii, wanajua MA VX V8, mil 280 each, CCM basi, ciao
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom