JK akiri kushindwa, Tutamsaidia - Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK akiri kushindwa, Tutamsaidia - Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 29, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  JK akiri kushindwa, Tutamsaidia - Mbowe

  • Asema taifa linapita katika majaribu mazito kiuongozi

  na Edward Kinabo
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemtaka Rais Jakaya Kikwete akiri kushindwa kuiongoza nchi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

  Mbowe aliyasema hayo jana wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA, uliofanyika katika Ukumbi wa Keys Hotel, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia mustakabali wa nchi katika kipindi hiki.

  "Ndugu wajumbe tunakutana katika mazingira na katika wakati ambapo taifa letu linahitaji uponyaji. Linahitaji uponyaji wa kisiasa, kijamii, kiuchumi na pia linahitaji uponyaji wa kiroho. Leo taifa linapitia kwenye majaribu makubwa na viongozi wetu hawana majibu, wala kauli thabiti. Hawana nia wala uwezo wa kuhimili changamoto zinazolikabili taifa hivi sasa. Tuna tatizo kubwa la uongozi, tuna ombwe la uongozi.

  '‘Rais ameshindwa kutumia fursa ya kuwapo kwa vyama vingi nchini. Umefika wakati sasa rais wetu akiri kushindwa kuliongoza taifa, CHADEMA tutamsaidia. Asione aibu. Asione CHADEMA kama genge la watu wanaotaka kumpinga bila kumsaidia. CHADEMA haifurahii kuona rais wetu akishindwa kuongoza nchi," alisema Mbowe na kushangiliwa na wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho.

  Akizungumzia hali ya kisiasa, alisema Rais Kikwete alipolihutubia Bunge Desemba 30, 2005, aliahidi mambo mengi na kudhaniwa kuwa ni rais mwenye uwezo na dhamira ya kweli ya kutekeleza ahadi hizo, lakini hadi leo azima yake ya kufanikisha maisha bora kwa kila Mtanzania haijatekelezwa.

  Alisema Rais Kikwete aliahidi kuimarisha demokrasia ya vyama vingi nchini, lakini yeye na chama chake ndio wamekuwa wa kwanza kukandamiza demokrasia, kwa kupitisha marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa yanayokwaza muungano wa vyama hivyo.

  "Wanapitisha sheria wakifikiri wao (CCM) watatawala milele. Wanapitisha sheria wakitazama maslahi ya sasa ya CCM. Leo vyama haviwezi kuungana bila kufuta madiwani, wabunge na viongozi wote wa kuchaguliwa katika chaguzi za kiserikali. Huku ni kukosa busara za kiuongozi, haya ni matumizi mabaya ya wingi wao bungeni. CHADEMA tunasema tutafuta ubabe huu mwaka 2010, tutashinda na kuwa na Bunge lenye uwiano mzuri kwa ajili ya maslahi ya taifa dhidi ya maslahi ya chama," alisema Mbowe.

  Alisema CHADEMA itaendelea na mikutano yake ya hadhara, almaarufu Operesheni Sangara, kwa lengo la kuwaamsha Watanzania hadi siku watakapopiga kura kuchagua madiwani, wabunge na rais wao.

  Alimtaka Rais Kikwete kuhakikisha kuwa anamaliza ngwe yake akiwa anaheshimika, kwa kutumia vema kipindi chake kilichosalia, kufanya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na serikali yake kufanya marekebisho ya katiba, Sheria za Uchaguzi, na Sheria ya Vyama vya Siasa.

  "Tunamtaka Kikwete ahakikishe kuwa anamaliza ngwe yake akiwa anaheshimika, hatutaki awe kama Mkapa. Na tunamuonya Kikwete, yeye mwenyewe na serikali yake watalipa gharama ikiwa watayapuuza haya.


  '‘Tunaposema haya, Kikwete asifikiri kuwa tuna tamaa ya madaraka. Tunasema haya kwa lengo la kumsaidia. Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, akizungumzia nia ya kudai uhuru kule UN alisema, ‘tunapodai uhuru wa Tanganyika, na tunapodai kujitawala kama Watanganyika, si kwa sababu tuna tamaa ya uongozi, bali ni kwa sababu mkoloni mweupe ameshindwa kutusomesha, kuondoa maradhi na umaskini'. Leo, katika uongozi wa Kikwete, umaskini, maradhi na ujinga, vyote vimeongezeka," alisema Mbowe.

  Alisema katika kipindi cha uongozi wa Kikwete, taifa limeshuhudia mbinu chafu za kulinda mafisadi, hususan kwa CCM na serikali yake kutumia kesi za watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), kama kinga ya kulinda mafisadi wengine wengi, ambao bado hawajafikishwa mahakamani.

  Alisema mafisadi hao bado wanaendelea kuitumia CCM na serikali yake kama njia ya kutafutia madaraka na kujitengenezea kipato.

  Akizungumzia uchumi, alisema Rais Kikwete na serikali yake, ameanza kulitumia suala la kutetereka kwa uchumi wa dunia kama kisingizio cha hali mbaya ya uchumi nchini, huku akijua fika kuwa, uchumi wa Tanzania umekuwa ukitetereka siku zote za utawala wa CCM.

  Alisema serikali haina mkakati wowote wa kukabiliana na hali mbaya ya uchumi nchini zaidi ya kupiga porojo tu kwenye vyombo vya habari kuhusu kuyumba kwa uchumi wa dunia.

  Akitoa mfano katika suala la nishati ya umeme, alisema taifa linalazimishwa kuingia kwenye mjadala usio na tija kuhusu matumizi ya umeme wa dharura, badala ya kutafuta sera endelevu na mikakati madhubuti ya kutatua tatizo la uhaba wa umeme nchini.

  "Tunalazimishwa kujadili Dowans, IPTL... Awamu zote za Serikali ya CCM hazijawahi kuja na mpango endelevu wa kulipatia taifa hili umeme wa uhakika. Leo tunaongozwa na kizungumkuti cha umeme wa dharura. Tunataka sera endelevu na mikakati madhubuti ya kutupatia umeme wa sasa na wa miaka hamsini ijayo," alisema Mbowe na kushangiliwa.

  Aidha, alitoa msimamo wa chama chake kuhusu mradi wa vitambulisho vya taifa, na kusema kuwa CHADEMA inatambua umuhimu na haja ya msingi ya kuwa na vitambulisho vya taifa, lakini matumizi ya bilioni 229 kwa ajili ya mradi huo, si kipaumbele cha taifa.


  Alisema serikali makini haiwezi kutumia bilioni 229 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho vya wananchi, ambao wanapoteza maisha yao kwa kukosa dawa mahospitalini.

  "Naheshimu ‘national identity' (kitambulisho cha taifa), lakini si kipaumbele cha taifa kwa sasa. Huu ni mradi wa CCM kutafuta fedha za uchaguzi ujao. Ni sawa na suala la ununuzi wa rada ambapo fedha zililiwa. Ni mradi wa ulaji. Jambo moja ambalo ndugu wajumbe na pengine Watanzania hawalielewi, ni kufikiri kuwa, mradi huu utagharimu bilioni 229 tu. Huu unakusudiwa kuwa mradi endelevu ambao gharama zake zitakuwa zikiongezeka kila mara kwa mara," alisema Mbowe.

  Akizungumzia chama chake, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, CHADEMA imepitia katika majaribu makubwa ya kupandikiziwa mamluki na baadhi ya vyombo vya habari kutumiwa vibaya na CCM, kwa lengo la kukivuruga na kukisambaratisha.

  Alisisitiza akisema CHADEMA bado iko imara, haijagawanyika, na iko tayari kukabiliana na changamoto yoyote ile kwani inajiamini, ina dhamira safi, na maslahi ya taifa hili yapo mikononi mwa chama hicho, kinachoyapigania.

  Aidha, Mbowe alikanusha madai ya kuwapo mgawanyiko kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na viongozi wenzake, na kutaarifu kuwa kiongozi huyo yuko nje ya nchi kikazi.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Mar 29, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Nadhani hata mtoto mdogo anajua kuwa Kikwete ameshindwa, alishashindwa siku nyingi sana, kusema kuwa akiri, hakusaidii kuondoa matatizo wala kuiondoa CCM madarakani, nadhani ni vizuri kufanya siasa za 'kufunga goli' kuwa mtafanya nini hapo ifikapo 2010, maana ni mwakani tu.

  Operation sangara sawa, lakini anzisheni vitu vya kuivuta zaidi jamii, KAENI MBALI NA CCM, MNACHOFANYA SASA NI KUIPROMOTE CCM, mara mnamuunga mkono Mwakyembe, HAINIINGII AKILINI MNAVYOWASIFIA BAADHI YA WANACHAMA NA VIONGOZI WA CCM, HUKU BOSI WAO WOTE HAO NI KIKWETE!!!!!

  KAENI MBALI NA CCM, MSITAJE JINA LA KIONGOZI YEYOTE WA CCM, HII HAITAWALETEA MATATIZO KAMA YA SASA YA 'DOWANS' MNAPOONA NCHI INATATIZO FULANI, MTOE BACKUP PLAN, TOENI NA TATUENI MATATIZO KAMA CHADEMA, HATA KAMA LIMETATULIWA VIVYO HIVYO NA WATU WA CCM, I MEAN HATA KAMA 'MMEDESA'

  EBU NIWAULIZE, HIVI KWENYE JIMBO LA MWAKYEMBE MTAMSIMAMISHA MGOMBEA WA CHADEMA??

  NARUDIA HATA KAMA CCM WAKO SAHIHI, NA NYIE SEMENI HIVYO HIVYO HATA KAMA WATASEMA MMEIGA, HII NI KUEPUSHA KUPROMOTE CCM BILA WENYEWE KUJIJUA!!!!

  ANZISHENI KOMBE LA CHADEMA, BENDI YA CHADEMA, YAANI KILA KITU CHA CHADEMA CHADEMA, HOSPITALI, HATA DALA DALA, NDALA, KEY HOLDER etc let people feel you!
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu kumbe tupo wote, yaani hapa umepiga msumari panapotakiwa, kwamba ya ndani ya CCM hayawahusu. Yanayowahusu ni ya serikali ya CCM sio chama cha siasa cha CCM. Kama CCM haifai wao ni kutushawishi wananchi tusiichague.

  Respect.

  FMES!

   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kumbuka hii ni siasa mkuu, kukiri ndo goli sasa.

  Hizi ndo siasa za kisasa. Mnataka siasa za akina Malecela?

  Tembelea website yao na kama unahitaji details i hope they will help. Sioni sababu ya kutoa tentative plan at this stage.

  Hivi utaweza kuongelea siasa za Tanzania, Serikali na mabaya/mazuri bila CCM? nitakushangaa.

  Sitashangaa CHADEMA kama hawatasimamisha. Naamini huenda wasisimamishe


  Chama chochote cha siasa kila lengo la kuongoza dola ili kuleta maisha bora. Kama wengine wamepatia lazima wasifiwe na waungwe mkono.

  CCM watawapa leseni ya kuanzisha redio?
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Utumbo mtupu......!
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 29, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Mkuu nadhani lengo lako ni kubishana au unaonca raha kujibi kila sentensi, wanachofanya Chadema ni kui-promote CCM, wakae mbali nao, sijui unafikiri nini kusema kuwa serikali haiwezi kuwapa leseni ya redio Chadema, hayo mawazo ya kizamani, serikali haina tatizo hilo!!!

  Lengo langu ni kkuwa 2010, 2015 Chdema washike nchi, sasa kama maoni yangu UNAONA YA KIPINZANI POLE WEE, unanionyesha ni jinsi gani nyie chadema msivyokubali ushauri?? na vipi kama na mimi ni Chadema??

  acha ubishi ihsi kwenye relity, vyama vya upinzania bado sana kushika nchi!!

  wazo nililowapa ni la kushika nchi na si vinginevyo!

  Chadema wanamsifia kilango, mwakyembe, huku wanamponda Kikwete, haya Kikwete sasa anamsifia Kilango kwa kupigana na ufisadi!!!!! huoni Chadema hapo wamefungwa goli?????

  hiyo siasa unayosema ya wapi??
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chadema mtajibandua sana lakini bado mnatumiwa na CCM,na hapo kwenye uhubiri wa Mbowe amekiri wazi kuwa wanatumika japo amelinda kuwa walikuwemo wanaotumika ,nasema bado wamo wanaotumika si hasha wakiwemo hao viongozi wa juu ,maana ikiwa umeamua kumsaidia Kikwete ni wazi kabisa hata ushirika upo ,Lipumba alisema na kumwambia Kikwete tukae tuzungumze hali ya nchi yetu ,kwa maana ya majadiliano na si kushirikiana.

  Mbowe anajaribu kuponda lakini bado anasema hatuko tayari kuona Rais wetu anashindwa ,ameshindwa kufahamu kuwa sio Raisi anaeshindwa bali ni Sultani CCM na wafuasi wake wote ,si Raisi kabisa kabisa ,wafuasi wote wa CCM wameshindwa kuongoza kuanzia juu mpaka balozi wa nyumba kumi ,hivi utamsaidiaje Kikwete________!Mtamsaidia kubadilisha viongozi ,amebadilisha mpaka amechoka na kuwashukia wakuu wa wilaya mwisho atawashukia makatibu kata ,maana hakuna uongozi ndani ya CCM na huna vya kuisaidia zaidi ya kuiondoa madarakani huo utakuwa msaada mkubwa kwao ,maana watapumzika na kungojea kama kuna au wana kesi za kujibu.

  Kosa la Chadema ni kujihusisha kikamilifu na matatizo ya wafuasi wa Sultani CCM ,hili ni kosa kubwa kisiasa ,Zitto ameingia kwenye kamati inayowachunguza wafuasi wa Sultani CCM ,almanusura apoteze umaarufu ,hawajakaa vizuri wanaonekana wakimsapoti Mwakiembe na kundi lake huku Zitto akiisapoti Serikali ,hatujui nani ni bora hadi sasa ,itajulikana baada ya kununua au kutonunuliwa ,lakini fununu nilizozipata kuwa miwaya itanunuliwa ,hapo inaonyesha Mwakiyembe na kundi lake la Wana Chadema litakuwa limeshindwa ,wanasema wataanzisha matatizo ya katiba katika Bunge kwa maana wataivaa serikali .Kwa mimi I dont care maana kwa sasa nipo upande wa upinzani msaada wangu itakuwa kuvuruga mipango yao na kuipaka matope mbele ya macho ya wananchi. Sitajiingiza kwa kusema tununue au tusinunue mpaka nione kuna maslahi ya upinzani ,maslahi ya upinzani ni yatapatikana wapi ,pale serikali itakaponunua mitambo hiyo ,hapo nitafaidika kisiasa kama mpinzani na si vinginevyo.

  Zito Lipumba wamesema mitambo inunuliwe ,hivi hawajui kama ni kosa ? Wanajua vizuri sana,lakini kisiasa kwa wao ni bora kwa kuipeleka serikali mchomo ,ndipo nikasema kuwa hakuna kabisa kuionyesha serikali njia ,ukiona inatumbukia unasema na kuwambia hapo ni pazuri zaidi ,jamani upinzani unatakiwa uwe upinzani ,kila jambo linalofanywa na Chama na serikali yao lazima mlitie doa ,wao wakisema Victoria ni ziwa kubwa barani Afrika nyie mseme hapana Victoria ni bahari ndogo ndani ya jungle ya Africa hata meli inapita.

  Zitto amekimbia au amekimbizwa kuhudhuria kwenye Mkutano au amefanyiwa njama asiwepo ,maana ingekuwa mkutano wa kawaida ingeonekana ni sawa lakini Mkutano wa Baraza kuu ,kitu ambacho wakubwa wote wa Chama lazima wawepo.Mambo yanafichwa lakini yatakuja juu tu.Na bado Chadema itaendelea kutumiwa na tutaona.
   
Loading...