JK akerwa na mapinduzi ya kijeshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK akerwa na mapinduzi ya kijeshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kite Munganga, Nov 27, 2009.

 1. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kikwete akerwa mapinduzi ya kijeshi Afrika
  Na Mwandishi maalum NIPASHE  27th November 2009
  Rais Jakaya Kikwete, ameutaka Umoja wa Mataifa (UN) na jumuia ya kimataifa, kuamua kuufanya msimamo wa kupinga mapinduzi ya kijeshi katika Afrika kuwa rasmi wa Umoja na jumuia hiyo.
  Aidha, Rais Kikwete amesema kinyume na baadhi ya madai ya baadhi ya watu, nchi za Afrika, zimepiga hatua kubwa katika kujenga demokrasia na kupambana na rushwa.
  Vile vile, ametaka watu wenye asili ya Afrika wanaoishi nje ya bara hilo kusaidia na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa bara lao ili nalo liweze kuondokana na umasikini kama zilivyo sehemu nyingine duniani.
  Rais Kikwete alikuwa akihutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Jamaica kwenye jengo la Bunge hilo la Gordon House mjini Kingston.
  Alihutubia kikao hicho cha Bunge kama sehemu ya ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku nne nchini humo.
  Katika hotuba yake iliyokatishwa mara kwa mara na makofi ya kushangiliwa, Rais Kikwete aliwaambia wabunge wa Baraza la Wawakilishi na Baraza la Seneti la nchi hiyo kuwa demokrasia inajichimbia katika Afrika na kuwa leo hii ramani ya kisiasa ya Afrika imebadilika kabisa.
  “Katika karne tatu za mwanzo za uhuru, Serikali nyingi za Afrika zilitawaliwa na mfumo wa chama kimoja na katika hali mbaya zaidi zilitawaliwa na udikteta wa kijeshi. Lakini sasa hali imebadilika. Mfumo wa vyama vingi sasa ni kawaida katika karibu nchi zote barani.
  Matukio ya ukamataji madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi na njia nyingine sasa ni mambo nadra,” alisema. Aliongeza: “Habari nzuri ni kwamba Afrika ina msimamo thabiti kuhusu mabadiliko haya yasiyokuwa ya kikatiba ya Serikali. Hili liko katika Katiba ya Umoja wa Afrika kwamba Serikali zinazoingia madarakani kwa namna hii hazitatambuliwa. Tatizo pekee ni kwamba hatupati ushirikiano kutoka kwa jumuia ya kimataifa.”
  Alisema baadhi ya nchi na taasisi za kimataifa zimefikia uamuzi wa kuzitambua Serikali zinazoingia madarakani kwa njia zisizo halali na hivyo kudhoofisha msimamo wa Afrika.
  Alisema wanaona msimamo huo kama mwamko mpya na hatua sahihi ambao unalipa Bara la Afrika matumaini na hivyo kuuomba Umoja wa Mataifa kuufanya msimamo huo rasmi wa umoja huo.”
  Kuhusu demokrasia na rushwa, Rais aliwaambia wabunge hao kuwa sasa hivi kuna ufahamu mkubwa zaidi miongoni mwa tabaka la wanasiasa wa Afrika kuhusu umuhimu wa kuanzisha na kudumisha misingi ya utawala wa kidemokrasia, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya rushwa.
  Juu ya ushiriki wa watu wenye asili ya Afrika lakini wanaishi nje katika maendeleo ya Afrika, Rais Kikwete alisema ni sehemu muhimu ambayo Bara la Afrika linataka kushirikiana nao.
  Wakati huo huo, Taifa la Jamaica limemtunukia Rais Kikwete nishani ya juu kabisa kutolewa na taifa hilo kwa kiongozi wa nchi za nje.
  Nishani hiyo ya Utumishi Uliotukuka, ilitolewa kwa Rais Kikwete na Gavana Mkuu wa Jamaica, Sir Patrick Allen juzi jioni katika halfa iliyofanyika kabla ya chakula rasmi cha usiku kilichoandaliwa na Sir Patrick Allen kwa heshima ya Rais Kikwete. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Gavana Mkuu huyo alisema Jamaica imeamua kutoa nishani hiyo kwa kutambua uongozi imara na uliotukuka wa Rais Kikwete katika nyanja na masuala mengi.
  Naye Rais Kikwete ameishukuru Serikali na wananchi wa Jamaica kwa heshima ya kutunukiwa nishani hiyo yenye kuheshimiwa mno katika Jamaica

  .....Je anatatua upande wa pili?.....
   
 2. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Quote
  Gavana Mkuu huyo alisema Jamaica imeamua kutoa nishani hiyo kwa kutambua uongozi imara na uliotukuka wa Rais Kikwete katika nyanja na masuala mengi.
  Naye Rais Kikwete ameishukuru Serikali na wananchi wa Jamaica kwa heshima ya kutunukiwa nishani hiyo yenye kuheshimiwa mno katika Jamaica

  Mkapa amepewa tuzo la uongozi bora na mfano wa kuigwa Africa, tena hapa Jamaica imetambua uongozi imara na uliotukuka wa JK....hapa kuna mawili either sisi wa Tz hatutambui mchango wa viongozi wetu kwa sababu nabii hakosi heshima isipokuwa kwao AMA hawa watu wanaowatunukia wanafanya hivyo bila tathmini ya kweli wanapenda tu kuwafurahisha hawa watunukiwa.
  Inakera sana kuona mtu huyo huyo katika dunia hiyo hiyo na kazi hiyo hiyo anapata sura mbili tofauti zenye kukinzana sana!

  Jamaica: Uongozi imara na uliotukuka kwa JK
  Tz: kuna malalamiko kuwa kuna ombwe la uongozi....

  Uganda: Uongozi bora na mfano wa kuigwa kwa Mkapa
  Tz: Ametumia nafasi yake ya uongozi kujinufaisha na familia yake/ ametuingiza katika mikataba mibovu isiyojali maslahi ya wananchi
  Tz: huyu mcha Mungu

  Kaaazi kweli kweli


  NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Anawasiwasi yatamkumba nini?
   
Loading...