JK akabidhi kadi za CCM 1138 ktk ziara yake LINDI.

Huyu aliyeshindwa kuwaunganisha watanzania na kuwatilia sumu ya udin?

Laana ya baba wa taifa itamfaata popote aendapo.

Kama rais alitakiwa atuambie mpaka sasa amefikia wapi kuutokomeza udini aliousisi na kupelekea makanisa zaidi ya 20 kuchomwa zanzibar, zaid ya matatu kuharibiwa Dar, zaid ya mawili kuharibiwa Ruvuma zaid ya mawili kuharibiwa Kigoma nk.

Kama Rais anatakiwa kutuongoza watanzania kuitafuta amani ya kweli na maendeleo yetu. Kutuletea habari za kagawa kadi ngapi, wapi na kwa nani ni kama upuuzi akiacha masuala mazito nayamuhimu yakitutesa watanzania kama

Mfumko wa bei

Afya duni

Elimu mbovu

Ufisadi na kuwakumbatia mafisadi nk

Amwachie mangula, Nape na mzee wa mikasi kupokea kadi na takataka zingine yeye ashughulikie mambo ya kitaifa zaidi sio kichama.
 
hakuna ubaya acheni JK amwage Kadi wapo watu wanaikubali CCM kama wwe unavyoikuibali Chadema
 
sasa kama amewapa kadi wanachama wapya 1138 tupeni picha nasi tushuhudie mlichokiandika.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewapokea na kuwakabidhi kadi wanachama wapya 1138 walipojiunga na Chama Cha Mapinduzi, katika wilaya za Liwale na Nachingwea Mkoani Lindi.


Mwenyekiti Huyo wa Chama Tawala aliwapokea wanachama hao wapya baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake wa hadhara katika uzinduzi wa Boma la Wananchi Nachingwea na mkutano wa Hadhara Liwale, ambapo wanachama hao wapya walikabidhiwa kadi za chama na kisha kuapishwa kwa Imani na Ahadi za Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi.


Mheshimiwa Rais yupo katika ziara ya Kikazi Mkoani humo ambapo alishiriki maazimisho ya siku ya Ukimwi Duniani tarehe 01[SUP]st[/SUP] Dec 2012 kisha kufanya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ya wananchi Mkoani Lindi pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali na Changamoto zinazoikabili Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.


Mheshimiwa Rais anaendelea na Ziara yake Mkoani umo ambapo leo yupo katika wilaya ya Kilwa ambayo iko chini ya Mheshimiwa Abdallah Ulega aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani. Mheshimiwa Rais anategemea kumalizia ziara yake wilayani Kilwa,alasiri ya leo, tarehe 5[SUP]th[/SUP] Dec 2012.

Ndicho kilichompeleka Lindi? Vipi akufungua matawi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom