Jayspeed
Senior Member
- Feb 23, 2014
- 156
- 168
1:KIJANA JITAMBUE
Pana kila sababu ya kijana kujitambua maana kijana anapojitambua anakuwa na uwezo mpana wa kuchanganua mambo kiyakinifu, anakuwa na uwezo wa kuona mbali ki-fikra..
Kijana ambae hajitambui hata ukimpa mtaji wa mabilioni ya pesa hawezi kufanikiwa.
Mungu amekujalia akili na nguvu je kwanini usijitambue..jiulize vilema wangapi wanafanya kazi na kufanikiwa wewe uliebarikiwa kila kitu na Mungu wako kwanini usifanye na kufanikiwa? Yote haya yanatokana na kutojitambua kama kijana ...utakuja kujitambua muda ukiwa umeshakuacha ndio utajipa moyo muda unao lakini akili na mwili vitakua vimechoka vimekata tamaa vyote kwa pamoja.
Paul Gascoine "Gazza" mchezaji mpira maarufu wa Uingereza na vilabu 9 tofauti..kipindi akiwa kijana alijaliwa kipaji ndani ya miguu yake na aliweza kukitumia vizuri kwa kuwapa mashabiki wake wanachohitaji na yeye aliingiza fedha kupitia miguu yake uwanjani lakini tatizo hakujitambua Gazza, hakutambua kuwa mpira ni mchezo wa muda mfupi hakutambua kuwa kuna maisha baada ya mpira akajikuta anatumia pesa zake kwenye ulevi wa pombe uliopindukia..alicheza mpira kwa mafanikio lakini hakuyaona mafanikio yake Gazza alikosa kitu kichwani mwake na kitu alichokosa ilikua KUJITAMBUA yeye kama yeye alijikuta akizitambua pombe zaidi kuliko yeye mwenyewe. Endapo Gazza angejitambua angekuwepo mbali kimaisha kama Antonio Conte Mourinho hata Guardiola na ana umri wa miaka 49 kwa sasa lakini maisha yake ni kama ameishi karne moja.
Vijana tuna mifano mingi ya kuangalia na kujifunza kwa vijana wenzetu ambao hawakujitambua na sasa wanaishi maisha yaliowachagua na sio waliyoyachagua mfano kama Chid Benz na Daz Baba. Sidhani kama kuna mtu anatamani maisha kama hayo
Mifano hiyo hapo juu ni hasara za kutojitambua kama vijana lakini endapo utajitambua ukajua umekuja duniani kufanya nini na unatakiwa kuwa wapi Mungu yu pamoja nawe hakika utafanikiwa.
Kumbuka ukishindwa kujitambua na mafanikio pia yanashindwa kukutambua
.
.
.
.
.
By Jay Speed