Amoxlin
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 3,782
- 4,111
Habari wana-jamvi.
Katika kipindi hiki kumekuwa na ushindani mkubwa sana ktk sekta ya elimu hapa nchini.
Ushindani huo upo katika utoaji wa elimu bora, ajira kwa walimu sambamba na ufaulu mzuri wa wanafunzi ili kujiongezea wateja (soko) ktk shule binafsi.
Katika shule nyingi kumekuwa na wimbi kubwa la walimu wasio na sifa (hawajasomea ualimu / walioshindwa kuhitimu kutokana na maendeleo mabaya kitaaluma) ambao kazi yao ni kuwakaririsha wanafunzi vitabu hata kama vimekosewa kwakuwa sio fani yao.
Walimu hawa vishoka kwa kawaida hufundisha masomo yote, kila somo yeye twende... Ilimradi kuziba nafasi zisizo na walimu ila ufanisi hakuna.
Kwanini walimu wasio na sifa?
Wakuu wa shule binafsi hasa zilizopo chini ya jumuia ya wazazi ambazo baadhi huendeshwa kisiasa na sio kisayansi huajiri walimu wasio na sifa ili kuwalipa mishahara midogo sana bila kujali wanafunzi wanaathirika vipi darasani.
Baadhi ya walimu hao wasio na sifa ni ndugu wa viongozi wa ngazi za juu za shule au chama (katika shule zilizopo chini ya jumuia ya wazazi).
Kutokana na hali hii ya kuwa na walimu wasio na sifa kwa kawaida kunakuwa na kamati ya ufundi ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha wanafunzi hao wanafaulu hata kwa kupitia goli la mkono.
Wito wangu:
Wakaguzi wa masuala ya elimu wazikague shule binafsi hasa zilizopo chini ya jumuiya ya wazazi ambazo huendeshwa kisiasa ili kujiridhisha na hali halisi.
Wasikague tu maandalio ya somo ila wakague na vyeti vya walimu ktk shule hizo kwani wapo walimu wenye sifa mitaani ila hawapati ajira kutokana na kukumbatia vishoka wanaoteketeza taifa letu.
Mpango huu uanzie ktk mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Moshi, Mwanga, Rombo nk. Pia ktk mkoa wa Tanga ambapo hali hazitofautiani sana kutokana na wingi wa shule hizi.