Masulupwete
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 2,366
- 2,420
Leo katika hali ya kushangaza watumishi wa kivuko cha kigamboni wamesikika wakitangaza kwamba wameanzisha operesheni waliyoipa jina "Operesheni ya Kukusanya Mapato".
Operesheni hii inatia shaka na kuzua maswali mengi. Je ni lini wamegundua mapato yanapotea? Je wamejua sababu? Na je kwa kipindi chote cha huko nyuma ni fedha kiasi gani zimepotea hadi wanavyoanzisha hii operesheni?
Hawa jamaa ni wasanii na ukweli wanaujua. Wanapitisha watu wengi bila kuwalipisha. Hii operesheni ni usanii mtupu kwa sababu hao watu wanavuka bila kulipa wanaruhusiwa na watumishi wa hapohapo kivukoni, iweje leo watoe maspika nje na kuanza kuwapigia watu kelele eti wameanzisha operesheni tena bila hata kutaja wanamlenga nani?
Suala hapa ni kufuatwa kwa utaratibu na kutoa haki sawa kwa wote. Kama askari/mwanajeshi anaruhusiwa basi ijulikane ni wakati anaruhusiwa kuvuka kwa kipaumbele au la.
Ukweli ni kuwa kwa muda mrefu watumishi wa kivuko cha kigamboni wamekuwa wakiwaruhusu maaskari na wanajeshi wasio na MAVAZI rasmi ya kazi na maswahiba/marafiki zao kuvuka wao na MAGARI yao ya BINAFSI bila kulipia.
Kibaya zaidi licha ya kuwa watu hawa hawalipi hata senti moja ndo wanaopapatikiwa kwa kupewa kipaumbele cha wao kuvuka kwanza kama vile watu wengine hamna haraka!
Wahusika waache ubaguzi huu usio na kichwa wala miguu watu wote wakae foleni na kama kuna mtu anataka kuvuka mapema, basi ahakikishe anawahi mapema, sio unakuja saa mbili afu unategemea nyota zako zitakuvusha mapema wakati kuna watu wengine umewakuta wamefika hapo toka mapema saa 11 asubuhi!
Vinginevyo wananchi tuambiwe hawa wenzetu wanajenga taifa lipi?
Kwa waziri mhusika hili ni jipu kazi kazi kwako.