Jipu hili limeiva! Wizi kupitia Vodacom internet bundle!

Mjasiriamali1

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
891
237
Kampuni ya Vodacom kifurushi cha 500 unapata mb 150 plus 20 mb bonus. Kifurushi cha 1000 unapata mb 500 plus 50 mb bonus. Sasa usanii uko hapa ukitumia ukimaliza hizo bonus tuu, wanabadilisha charges! Zinakuwa kawaida kama hujaweka bundle! Kwa kila bundele inakuwa sh 0.2/kb, ni sawa na 200TSH kwa Mb 1. ambayo pia haikai! Sasa najiuliza kwanini mb za bonus ziende bila limitation kwanini hizi ambazo nimenunua ziwe 200tsh kwa Mb? Sio jipu hili?
 
Sasa ukitaka iwe inakaa tu bila kwisha itabidi usiwe unaitumia
 
Leo wamenitumia ujumbe wa kitapeli ili nijibu wanikate pesa zangu.

Vodacom ni matatizo inaongozwa na wahuni wauza k na matapeli.

Vodacom is distributing Tsh 25 Billion usage benefits to M-Pesa customers. To know your share send AMOUNT to 15300. Keep using M-Pesa to benefit in next payouts
 
Mi nilishaizika lain ya voda kitamboo njooni Halotel jero(500)...mb 330 bila chenga au nenda airtel utafurahi
 
Kampuni ya Vodacom kifurushi cha 500 unapata mb 150 plus 20 mb bonus. Kifurushi cha 1000 unapata mb 500 plus 50 mb bonus. Sasa usanii uko hapa ukitumia ukimaliza hizo bonus tuu, wanabadilisha charges! Zinakuwa kawaida kama hujaweka bundle! Kwa kila bundele inakuwa sh 0.2/kb, ni sawa na 200TSH kwa Mb 1. ambayo pia haikai! Sasa najiuliza kwanini mb za bonus ziende bila limitation kwanini hizi ambazo nimenunua ziwe 200tsh kwa Mb? Sio jipu hili?

Sichoki kurudia kusema kuwa vodacom ni wanyan'ganyi wa mchana kweupe!
 
Mimi nilinunua bando la wiki la 2000 sijapata hata mb1.najaribu kuwasiliana nao bila mafanikio.sijuwi tatizo ls . Kiufundi au wanjanja wachache wameingia
 
Leo wamenitumia ujumbe wa kitapeli ili nijibu wanikate pesa zangu.

Vodacom ni matatizo inaongozwa na wahuni wauza k na matapeli.

Vodacom is distributing Tsh 25 Billion usage benefits to M-Pesa customers. To know your share send AMOUNT to 15300. Keep using M-Pesa to benefit in next payouts

mimi mwenyewe nimetumiwa kiukweli sijaelewa mantik yake
 
mimi mwenyewe nimetumiwa kiukweli sijaelewa mantik yake
Mkuu hapo ukijiroga kutuma unakatwa pesa.

Kama kila mteja atattuma ujumbe unadhani watakusanya kiasi gani cha pes?

Tunafanyiwa upumbavu wakati mamlaka husika wapo tu
 
Leo wamenitumia ujumbe wa kitapeli ili nijibu wanikate pesa zangu.

Vodacom ni matatizo inaongozwa na wahuni wauza k na matapeli.

Vodacom is distributing Tsh 25 Billion usage benefits to M-Pesa customers. To know your share send AMOUNT to 15300. Keep using M-Pesa to benefit in next payouts
Ujumbe nimeufanyia kazi na punde nikapokea gawiwo langu la faida kwa kutumia Mpesa!
 
Ni kwel kuna uwiz sana, hawa jamaa sijui vip, hata tukilalamika hawabadiliki, mi nimehamia halotel mana tsh 500 = 330mb

Voda tsh 500= 150mb + 150mb za bure, lakin hizo za bure hutaziona kabisa..!!
 
Mbona TIGO mambo murua!....
Tsh.500=500MBs
Tsh.1000=1GB...(Wiki nzima na Watsapp bure siku 7)
Tembelea OFA MAALUM sheikh!
 
Waliniudhi sana hawa, ni baada ya kununua kifurushi cha wiki kwa m pesa na kutokurudisha majibu mapema nikasubiri kama dakika kumi halafu nikaangalia salio nikakuta bado hela nliyonunulia kifurushi haijakatwa ikabidi ninunue kwa mara ya pili mchezo ukawa huo huo sijibiwi, nikaangalia tena salio nikakuta bado hawajakata! Nikasubiri tena weeee kwa mda kama nusu saa na zaidi ghafla zikaingia sms mbili zikifukuzana zote hongera kwa kununua kifurushi cha wiki, hela ikakatwa mara mbili nimepatwa na butwaa! Huu ni utapeli wa wazi kabisa...hawarudishi majib mapema unaponunua bando kwa m pesa ili wakukombe zote....kuanzia sasa sinunui tena bando kupitia m pesa!!!!
 
Back
Top Bottom