Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

Mkuu wangu kwa nini tuandikie mate wakati wino Upo.... Yeye sii anajua hizo kanuni nimemwomba hivi:- Sasa wewe unayejua kanuni za NCCR nambie ama nionyeshe mahala inaposema mtu asipokuwa na confidence na kiongozi mwenyekiti afukuzwe uanachama. Ukinionyesha hilo tu, sina maelezo zaidi na kama hutakuja na jibu hilo basi sina sababu ya malumbano..

Akiweza kunionyesha hilo ubishi huu wa nini maana tutakuwa tumejifunza wengi hapa janvini maana yeye anajua sana ya NCCR!
 
Mkandara kilichomponza Kafulila si hayo unayomuuliza Lema ila ni NIDHAMU yake, hata Kafulila aki file case mahakamani na kusema amefukuzwa NCCR kwa kumpinga mwenyekiti definitely atashindwa kesi. Unaweza kuwa uko sahihi kuwa Kafulila alikuwa sahihi kutokuwana imani na mwenyekiti wake kitu ambacho hata mimi sikipingi lakini je alitumia njia sahihi kupresent hoja yake bila kukiuka kanuni za chama?
 
navyokumbuka mimi kama nilisoma vizuri, Kafulila na wajumbe wengine wali file case hii ktk kikao cha Nec mwezi jana na habari hizi tulizijua wengi tu na Kafulila alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ni baada ya kuwakilisha malalamiko yao.

Mkuu wangu chama chochote kinapomfukuza uanachama hadi mgombea Urais wake na wajumbe wengine sijui 20 kwa tuhuma za kutoa siri ambayo inamweka mwenyekiti kufanya kazi na CCM, kisha mnadai ilikuwa siri ya chama hapo mnawatisha hadi wananchi na wanachama...NCCR inajiweka mahala pabaya zaidi kwa sababu katibu hakutakiwa kutoa maamuzi yoyote hadi kikao kijacho cha Nec na kama ni dharura mwenye kushtakiwa alikuwa Mbatia na sio Kafulila wangeharakisha hilo basi kumsafisha kwanza.

Swala la Mbatia liliahirishwa hadi kikao kijacho cha chama ya Kafulila kikao cha dharura hivi kweli unatakiwa kuitisha kikao cha dharura kwa madai gani mazito! madai gani mazito kati ya Mwenyekiti anayefanya kazi na chama kingine au mtuhumu anayezungumza na magazeti. Kikao cha dharura kingekuwa dhidi ya Mbatia bila hata kufikiri sana...Nimemaliza mengine mtajaza wenyewe. Lema alitakiwa kushtuka kwa habari hizi na sio kuwasifia chama ambacho kinatia mashaka hata sisi wananchi kujiunga nacho - Ati siri za chama!

Simtetei Kafulila hata kidogo lakini Uongozi wa NCCR hawakutumia akili kabisa...wao ndio wanatisha sasa hivi it seems kama kuna conspiracy ya viongozi wote wa juu kuhusiana na ushirika wao na CCM na which makes them CCM - C.
 

word...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…