Jipatie viwanja kwa mkopo - Madale Mbopo

Mangi wa Rombo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
207
Reaction score
148
Habari!

Viwanja vinapatikana, Madale Mbopo (Mwendo wa DK 30 kutoka Round about ya Madale). Viwanja vinapimwa kuanzia Square Meter 20x20... Bei kwa kila square meter ni sh 13,000/ TZS.. Mteja anaruhusiwa kulipa kidogo kidogo kwa awamu nne, akianza na 30% ya gharama ya kiwanja husika na inayobaki akimalizia ndani ya miezi mitatu inayofuata.

Huu sio mradi wa kampuni bali ni eneo la mtu binafsi ambaye alibahatika kuwa na eneo kubwa na sasa anauza! Viwanja havijapimwa, lakini utaratibu wa kupima upo kwenye mchakato, kutakuwa na nyaraka halali za makubaliano ya mauzo toka serikali za mtaa.

Mfano wa gharama za kiwanja:
20x20 = 400 Sq Meters, 400 x 13000 = 5,200,000TZS, mteja atalipa 30% kama advance ambayo ni sawa na 1,560,000 kisha iliyobaki ambayo ni sawa na 3,640,000 atailipa ndani ya miezi 3 inayofuata.

N;B,
Muuzaji hausiki na kumtafutia mteja hati. Hilo no jukumu binafsi la mnunuaji,

Kama unahitaji kuviona viwanja:
Tafadhali fanya mawasiliano kwenye namba hii 0658402450.

Karibuni sana!
 
Kama nilimsikia Mheshimiwa Waziri akisema kuwa SERIKALI YA MTAA haina mamlaka ya kusimamia mauzo ya ardhi.
 
Mkataba wa mauziano huandikwa na kusainiwa na mtendaji, ni mkataba halali na unatambulika kisheria na ndio maana hata hizo form ni similar (zinafanana kwa kata yeyote utakayokwenda) ndio mkataba mama (primary contract) kwenye kurasimisha ardhi..
 
Ahaa, sasa nimeelewa. Afisa Mtendaji ni mwajiriwa wa serikali kuu kama mwakilishi katika serikali ya mtaa, inamake sense. Ila kiasi kinachobaki miezi mi3 mzee baba utaua wananchi. Binadamu wengi awamu hii 1m ndani ya mwezi haishikiki, miezi 6 wanadamu wangefarijika
 
Habari,

Kuna nafasi ya mazungumzo pia ndugu kwa hiy niwatoe wateja hofu juu ya hilo. Hata maaumuzi ya kufikia kuviuza kwa malipo ya awamu ni baada ya kuona ugumu wa malipo ya pamoja kutokana na hali halisi ya kiuchumi!

Karibu sana!
 
Habari!

Viwanja vinapatikana, Madale Mbopo (Mwendo wa DK 30 kutoka Round about ya Madale). Viwanja vinapimwa kuanzia Square Meter 20x20... Bei kwa kila square meter ni sh 13,000/ TZS.. Mteja anaruhusiwa kulipa kidogo kidogo kwa awamu nne, akianza na 30% ya gharama ya kiwanja husika na inayobaki akimalizia ndani ya miezi mitatu inayofuata.

Huu sio mradi wa kampuni bali ni eneo la mtu binafsi ambaye alibahatika kuwa na eneo kubwa na sasa anauza! Viwanja havijapimwa, lakini utaratibu wa kupima upo kwenye mchakato, kutakuwa na nyaraka halali za makubaliano ya mauzo toka serikali za mtaa.

Mfano wa gharama za kiwanja:
20x20 = 400 Sq Meters, 400 x 13000 = 5,200,000TZS, mteja atalipa 30% kama advance ambayo ni sawa na 1,560,000 kisha iliyobaki ambayo ni sawa na 3,640,000 atailipa ndani ya miezi 3 inayofuata.

N;B,
Muuzaji hausiki na kumtafutia mteja hati. Hilo no jukumu binafsi la mnunuaji,

Kama unahitaji kuviona viwanja:
Tafadhali fanya mawasiliano kwenye namba hii 0658402450.

Karibuni sana!
 
Unaposema mwendo WA dakika 30, huoni Ni uongo maana watu wanatofautiana ukubwa WA barua na mwendokasi WA kutembea?
Weka kwa kipimo cha kilomita ngapi tokea hiyo round about na sio dakika
 
Ni wastani wa muda kwa kutumia gari ndugu!
 
Angalizo:

Umakini unatakiwa kwa kiasi kikubwa hapo !

Kama huyo ni muhusika yani mmiliki halali wa eneo baada ya kujiridhisha vyakutosha sawa mtu waweza nunua!

Sababu kule wavamizi wametamalaki kwa kiasi kikubwa sana!

Kuna kikundi cha watu wamevamia maeneo ya watu !

Serikali imeanza kushughulikia kuhakikisha wamiliki halali wanatejeshewa maeneo yao.
 
Watu wamekopa mikopo wakanunua maeneo yao,
Wengi hadi leo bado wanakatwa marejesho halafu eti wavamizi wanachukua maeneo ya watu ?!

Wananchi wanamsubiri Lukuvi kwa hamu!

Hata hivyo serikali imeonekana kuingilia kati kuhahakisha wenye maeneo yao halali waweze kurejeshewa haraka
 
Nasikia kuna msomali eti ndo kinara wa huo mtandao wa uvamizi!

Lakini serikali chini ya uncle Magu haiwezi kushindwa kusimamia jambo hilo na kuhahakisha wale wamiliki halali wanarejeshewa maeneo yao haraka.
 
Kunapotokea jambo ambalo baya inabidi kujiuliza linaanzishwa na kina nani?
Asili ya hao watu au huyo mtu ikoje?

Roho ya namna hiyo na ujasiri wa kufanya jambo au mambo mabaya kiasi hicho kaitoa wapi?

Kwa wastani watanzania hatunaga roho za kufanya mambo mabaya ya kutisha,

Kunapotokea jambo ambalo linakuwa siyo la kawaida baya ni vema kuchunguza kwa kina kupata ukweli wa mambo utakaopelekea kuchukua hatua za kisheria na hatimae kufanya maamuzi ya haki.
 
Tatizo hapa hao wenye maeneo hawakuyaendeleza. Sasa hivi hao wavamizi wanalipishwa kodi ya ardhi. Ni jambo gumu hili. Ila ilikuwa ni vigumu kuelewa watu wanamiliki acre 10 au zaidi. Ndio yale ya kina Sumaye. Tena umiliki huo ni mjini. Bahati mbaya hawa wavamizi wanazidi kujenga na wanapelekewa Huduma za kijamii
 
Wangeyaendeleza saa ngapi ikiwa yamevamiwa?
Wengine walikuwa nasubiri kumalizia kulipa mikono ili waendeleze hayo maeneo!

Kwani sheria imesema eneo lisipoendelezwa livamiwe?

Itakuwa ni jamii ya aina gani tunajenga ya vurugu na hatari?

Serikali ilishasema hata mtu ajenge gorofa ndefu kuliko zote duniani ajiandae kubomolewa !

Hilo angalizo lilishatolewa mapema!

Haki ya mtu haipotei.
 
Uvamizi siyo jambo Jena. Bahati mbaya sana Serikali inachukua kodi ya pango la ardhi kwa wananchi wale. Mie nadhani ni vyema wenye maeneo muende mahakamani
 
Hiyo si hoja!

Muulize yule jamaa wa Victoria station na wengine wengi, walikuwa wanalipa kodi zote tena kwa fedha nyingi sababu thamani ya maeneo yao ilikuwa kubwa, walikuwa na hati na vielelezo vyote vya serikali lakini mwisho wa siku kwa kuwa haikuwa haki yao wamenyang’anywa umiliki na kurejeshwa kwa wenye haki.

Kwa hiyo kulipia kodi si hoja wala msijidanganye!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom