Jionee Mossad ilivyopanga na kujipigia Mpersia

Jionee Mossad ilivyopanga na kujipigia Mpersia

Obugwa Izoba

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
10,467
Reaction score
11,641
Marekani na Israel zilikuwa zikijiandaa kulipiza kisasi haraka na kikali kwa Iran usiku kucha. Shukrani kwa ujasusi uliopangwa kwa njia tata za majasusi na marubani wa Israeli.


Ilipobainika kuwa Israel ilikuwa karibu kuishambulia Iran, makamanda wa jeshi la anga la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran walikusanyika katika chumba kimoja cha underground ili kupanga namna ya kujibu kwa haraka mashambulizi hayo.

Lakini Israeli walijua itifaki hiyo ya dharura ya Iran na eneo la bunker watakapojificha hao majamaa. IDF iliharibu na kumuua kamanda mkuu na wakuu wa vikosi vya ulinzi. Walikuwa miongoni mwa makamanda zaidi ya dazeni walikusanyika kupanga mikakati. Wakuu wa IRGC, jeshi la Iran na makao makuu ya kijeshi ya dharura ya Iran wote waliuliwa shambulio la kwanza na la mapema.

Eneo lingine kuu lililolengwa lilikuwa ni mifumo ya ulinzi wa anga wa Iran na rada. Ujasusi wa Israeli ulijipanga na kupiga maeneo hayo katika shambulio la awali jambo lililoipa IDF uhuru wa kujitawala katika anga ya Iran bila kizuizi.

Wakati huohuo, shirika la kijasusi la Israel la Mossad lilikuwa likiendesha mfululizo wa hujuma za siri ndani ya Iran ili kuchukua ulinzi wa anga la Iran.

Mamia ya mawakala wa Mossad ndani ya Iran walihusika, ikiwa ni pamoja na kitengo maalum cha wahudumu wa Iran wanaofanya kazi Mossad.

Katika eneo jingine ndani ya Iran, Mossad ilisambaza kwa siri mifumo ya silaha na teknolojia za hali ya juu zilizofichwa kwenye magari. Wakati mashambulizi ya Israel yalipoanza, silaha hizi zililipuliwa na kuharibu malengo ya ulinzi wa anga ya Iran.

Mossad pia ilianzisha kambi ya ndege zisizo na rubani ndani ya Iran ambazo ziliingizwa kinyemela muda mrefu kabla ya operesheni hiyo, afisa wa ujasusi wa Israel alisema.

Wakati wa shambulizi la Israel, ndege zisizo na rubani ziliwashwa na kurushwa kuelekea kwenye vituo vya makombora vya Iran kwenye kituo cha Esfajabad karibu na Tehran na kuharibu makombora yote ya Balistic ambayo yalipangwa uelekeo wa Israel.

IDF ilikuwa tayari kwa hali mbaya zaidi ikikadiria kuwa Iran ingerusha kwa haraka makombora 300-500 ya balistiki kuelekea Israeli, afisa wa ujasusi wa Israeli alisema.

Badala yake na kwa kuchukua muda mrefu toka Israel ashambulie, Iran ilijibu kwa takriban drones 100 ambazo zilidhibitiwa kiraisi na IDF.
 
Iran kawa mnyonge sana, amepoteana na marafiki zake wamsaidie
 
Hawa wote ni top layer wametangulizwa kwa mabikra
iran.jpg
 
Back
Top Bottom