Jinsi ya kuzuia tagging usizozitaka facebook

Jinsi ya kuzuia tagging usizozitaka facebook

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
38,343
Reaction score
77,132
Kutokana na facebook ilivyo unaweza kuombana urafiki na mtu usiyejua tabia zake au mienendo yake, urafiki utakuwepo kama haupo kwa siku kadhaa kisha kuna siku unaamka unakuta notification kua Fulani Kibomba amekutag kwenye picha.

Ugumu utakuja utakapokuta picha yenyewe ni ya kingono na wewe una ndugu, wafanyakazi wenzako, wanafunzi wenzako, watu unaheshimiana nao na haupo tayari waione hiyo picha ambayo Fulani Kibomba alikutag. Wengi wetu tutakimbilia google au JamiiForums na kuuliza jinsi gani utajiondoa katika hiyo picha aliyokutag. Suluhisho utapata ila ni utakua umeondoa hiyo post katika profile yako ila marafiki wataendelea kukuona kwenye feeds na search zao.

Hapa nitaelezea jinsi ya kuzuia kabisa uwezekano wa Fulani Kibomba kukutag katika post ambayo hauitaki. Utakachofanya ni kuwezesha akaunti yako iwe inareview post ambayo wakina Fulani Kibomba watakutag kabla hujakubaliana nayo.

Hatua ya kwanza.
Ingia kwenye akaunti yako kupitia kifaa chako kisha bonyeza vimistari vitatu vilivyokaa kwa kupangana kwenda juu.
1479374371683.jpg


Hatua ya pili.
Shusha chini mpaka kwenye sehemu iliyoandikwa 'account settings' bonyeza na ingia hapo.
1479374403304.jpg


Hatua ya tatu.
Nenda kwenye 'timeline and tagging' bonyeza na ingia hapo.
1479374437044.jpg


Hatua ya nne.
Nenda kwenye 'review tags people add...'
1479374460524.jpg


Hatua ya tano.
Nenda kwenye 'tag review' na switch on.
1479374492965.jpg
 
Nashukuru sana mkuu ngoja nikacheki, ila yangu mara nyingi tags zinanitaka nicomfirm kwanza kabla hazijatokea barazani, inawezekana ikofresh eeh??
Yea yako itakua iko fresh mkuu
 
Utazuia picha aliyokutag isiwepo kweny timeline yako kwa kui-hide ila still tag ipo palepale.
 
Mbona kila nikijaribu kuswichi on inakataa unagusa wapi ili kuswichi on?
 
Mbona kila nikijaribu kuswichi on inakataa unagusa wapi ili kuswichi on?
katika picha ya kuswitch on (hatua ya mwisho) kuna sehemu juu kulia imezungushiwa duara jekundu ndiyo hapo.
 
Back
Top Bottom