Jinsi ya kuwithdraw pesa kwa visa/ master card

nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,055
2,000
Ningependa kusema kuwa mimi ni mmoja kati ya wafanyabiashara ya forex. Sina muda mrefu kwenye hii biashara ila nimeweza kugundua changamoto kadhaa.

Changamoto ya kwanza ni namna ya kuchukua pesa zako pale unapozihitaji. Yaani limekua gumu kiasi cha kukatisha tamaa hasa kwa ma brokers ambao hawana option ya mpesa. Broker ambaye nilikua nikimtumia ni FXTM. Na bank niliyotumia kudeposit ni eco bank.

Kusema kweli, imekua changamoto kubwa sana kwenye suala la kuchukua pesa zangu. Tangu nilipo withdraw tar 22 nevomber, mpaka sasa sijapata hela zangu. Ilikua ijumaa nilipojaribu kuwasiliana nao. Wakanitumia kitu kinaitwa ARN. Wakaniambia hela zimeshatumwa kwenye acc yangu.

Hivyo niende na ARN hizo bank ili wamalizie hatua za upokeaji hela. Cha kushangaza ni kwamba pale bank wameniambia hawajui hata hizo ARN zina maana gani na hawajawahi kukutana na kitu kama hicho. Kwa kweli imekua changamoto.

Ila kuna broker mmoja anaitwa templerfx, huyu ni mzuri kwani unaweza toa na kuweka kwa mpesa. Unapata hela yako kati ya kisaa limoja mpaka Massa 6.

Kwa yeyote aliyewahi kukutana na tatizo kama hilo na akafanikiwa, naomba anielekeze alifuata taratibu zipi mpaka akafanikiwa.

Ahsanteni sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom