Jinsi ya kuwa mwanateknoljia bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kuwa mwanateknoljia bora

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Apr 25, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  1. Jifunze jambo au habari mpya kila siku.
  Kwa kutumia gooogle na mitandao mbali mbali mbali ni rahisi kujifunza mambo mapya ya kitenolojia. Changamoto ni chanzo ni chanzo na habari gani hasa zina mafunzo. Kutokana na uelewa , fani tofauti watu tuna prority tofauti
  Mfano zaidi ya jf tovuti nyingine ambazo natumia kujfunza na kupata tech news ya issue mbali mbali ni DailyTech http://www.howstuffworks.com to name a few .

  Cha msingi watu tuelewe internet ina kila aina ya habari nzuri na ina kila aina ya habari za ajabu. Mfano nimeona hapa kuna baadhi ya member wanapost article za kuhusu virus amabazo sio za kweli.(Hoax) Ujumbe unaasema eti virus ataburn the whole HDD. Hivi kuna virus anaweza kuunguza HDD.??????. So tusiamini na kucukua kizima kizima kila tunachoona kwenye net. Some time tuchunguze na tujirizishe.

  2. Fanyia kazi na jaribu mambo kwa vitendo
  Binafsi naona watanzania wengi tuna utaalam wa theory. Ikija kwenye nadharia na vitendo tunakwama na ukutana na vikwazo vingi. Hii inatokana na watu kuridhika nadhiria kitu amabcho si kizuri sana. Kifupi hatupendi kupigika. Nimewahi kufanya kazi na mtu ambaye alikuw hapendi kuonekana kashika cripping tool. Alichukia kweli kuitwa fundi au techinician Teh the teh. Yeye alitaka aitwe Network admin au engineer. Mwisho wa siku tunakuwa na vyeti safi lakini hatuna good practical experince

  3. Jiulize na uliza maswali magumu
  Kuna wataalamu hawapendi au wanaona aibu kuonekana wanauliza maswali .Binafsi naamin tutakuwa watalmu bora kama tutakubali kuwa una wakati tunaweza kuwa "wanafunzi" na kuna wakati tunaweza kuwa "walimu". Pausing kama mwalimu tuuuu au kama mwanafunziii tuuuuuuu siku zote haiwezi kumjenga mwanateknolojia. Na hata wanasiasa..

  Mfano una watu nimeona wanajiuliza maswali ya kuchakachua TV decoder ili wapte channel za bure. Lakini sio wengi wa watu hawa wamejiuliza swali gumu kwanza la HowStuffWorks "Satellite TV System".. Mtu aisoma articles mbali mbali kuhusu hili anaweza kujua urahisi na ugumu wa kuchakachua channel na atauwa kajifunza.

  Mtu akikuuliza kama mtaalam unajirate vipi utaalam wako wa iwe ni ICT, umeme programming, etc .? Wewe ni Advanced, Avarage or just end user. Binafsi i treat myself an avarage but competent ICT techician.


  4. Penda majadiliano endelevu
  kuna baadhi ya watuu hapa kwenye teknoloja na hata huko kwenye siasa na majukwaa mengine hawapendi kutoafautiana kwa mawazo, approach na ideas.. Ukimkosoa kitu anakuona adui au anakuwa mkali Vile vile kuna wale wengine kwa kuwa wajua sana akiona mtu anafanya au kaandika kitu fulani anamponda. Tena mbaya zaidi kwa lugha ya dhiaki.

  Tunachotakiwa kufanya ni simple kwanza tukubali kutaofautina na pili tukubali na tukaribishe majadiliano endelevu kwa lugha nzuri..

  Mfano kuna jamaa ana screen name ya shy. Mara nyingi nimesoma makala zake nzuri tu lakini tatizo la huyu mtaalam haendelezi mijadala ya makala alizoanzisha. . So kama akisoma maka hii abadilike.


  5. Wezesha end user kutatua matatizo yao wenyewe

  Kuna watalaam wanapenda kuendelea kutatua matatizo madogomadogo badala ya uwaambia wahusika nini cha kufanya wenyewe. huu unaweza kuwa ni uchoyo na vile vile kuna watu hawapendi kufuata proceure kusoma manual ya vifaa vyao huu nao ni Uvivu mbaya. So upande wa wataalam ni vizuri kuwawezesha watu kutatua matatizo madogo madogo ili wasisumbe tena na upande wa watuamiji wa kawiada uipta tatizo soma manual yakifaa au tafuta manua ya kifaa mtandaoni.

  Je kuna jambo nimeliacha, nimekosea au sijaligusia?

  Tuendeleeee
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Ujumbe mzuri mkuu, nami pia nitauzingatia... Gracias!
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  umeeleweka Mkuu,ni mwendo wa kugoogle mwanzo mwisho
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Safi sana mtoa mada, umegusa matatizo mengi ya hawa wanaojiita wataalam wetu. Hapo kwenye no. 5 ndo umepiga msumari, mimi ni end user lakini ninayependa kujishughulisha na matatizo yangu mwenyewe. Kuliko kukimbilia wanafunzi wa Comp. Sc ambao ni weupe, vitu vingi wamekariri na kuna tymes mimi ngwini huwasaidia kurekebisha matatizo yao ya software. Big up mkaka/mdada!
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mi mkaka nadhani wewe ni mdada tena unaweza kuwa mmasai maana naona kwenye avator nyonyo ziko nje nje na umevaa kiasili :rofl:
   
 6. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  safi sana mkuu
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Binafsi nimefurahishwa sana na thread yako,me mwenyewe ni mwanatknolojia,nashukuru sana kwa upeo wako wa kuona mbali,tuko pamoja mkuu.
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mhm, mbona unanitisha braza? Mi mkaka bwana, jees picha tu hiyo.
   
 9. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ahsante kwa shule mkuu
   
 10. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa kboko...post zake zinaeleweka na argument zake ni za maana,big up.
   
 11. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ya kuongezea:
  • Angalia vitu vidogo vidogo vinavyowasumbua watu kisha tafuta njia rahisi ya kuvitatua. Kwa mfano, wanawake (wengi ni hawa) wanapata taabu sana kuinamisha mgongo wakati wa kupiga deki; je, wewe ungewasaidiaje?
  • Chunguza teknolojia zilizopo, na uziboreshe (yaani, jaribu kuondoa mapungufu yake). Zingatia usemi huu: "Don't re-invent the wheel, but try to make it better".
   
 12. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  .....Mtazamaji uko sahihi kabisa.......
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  na wakati mwingine ukiwa unauliza kitu au unafanya kitu jikubali mwenyewe ndo baadae ushirikishe wengine..
   
Loading...