Jinsi ya kutengeneza Chocolate Cake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kutengeneza Chocolate Cake

Discussion in 'JF Chef' started by Michael Amon, Jul 28, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  MAHITAJI


  • Unga uliyotayarishwa tayari kwa kupikwa (pakiti moja - 500g)
  • Mayai matatu
  • Mafuta ya kupikia 80ml
  • Maji safi 200ml
  • Butter kiasi

  Kwa ajili ya topping

  • Nunua chokolate yenye karanga
  • Maziwa kikombe kimoja

  JINSI YA KUPIKA

  • Tayarisha oven yako kwa kuiwasha katika moto wa nyuzi 185 centigrade (365F)
  • Paka butter kiasi kwenye kikaangio chako kisha kiweke pembeni
  • Koroga mayai, changanya na maji safi, mafuta ya kupikia pamoja na unga uliyotayarishwa mpaka vichanganyike vyema
  • Nyunyuzia unga wa cocoa au unga wa ngano katika kikaangio chako ulichokipaka butter
  • Weka mchanganyiko wa unga, mayai, mafuta ya kupikia pamoja na maji safi ndani ya kikaangio chako kisha ingiza ndani ya oven na funga mlango uache keki iive kwa dakika zitegemeazo aina ya kikaangio chako.
  (Iwapo kikaangio chako ni shepu ya mstatili na kina vipimo hivi: 5 X 33 X 22cms = 2 X 13 X 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 - 45 kupika keki yako).

  (Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 22cms = 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 - 45 kupika keki yako).

  (Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 15cms = 6 inches basi utatumia muda wa dk 55 - 60 kupika keki yako).


  • Tumia toothpick au kijiti cha mbao kisafi kuchomeka katikati ya keki yako kuangalia kama imeiva vyema, baada ya hizo dakika hapo juu kupita. wapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka bila ya ungaunga basi keki yako imeiva vyema, iepue na uzime jiko. Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka na unga unga basi ujue bado keki yako haijaiva vyema. Funga mlango na uache iive kwa muda. Hakikisha kijiti kinatoka bila ya unga unga.
  • Iache keki yako ipoe kwa dakika 15 - 20 kabla hujaiondoa kwenye kikaangio

  Namna ya kutengeneza topping

  • Weka sufuria safi kwenye jiko
  • Vunja vunja chokolate yako na iweke kwenye sufuria yenye moto
  • Ongeza maziwa kikombe kimoja yenye moto
  • Koroga mchanganyiko huo mpaka uchanganyike vyema
  • Epua mchanganyiko wako weka na anza kupaka kwa kutumia brashi kwenye keki yako ambayo itakua imeshapoa
  • Keki yako ipo tayari kwa kuliwa

  Waweza kula na soda, chai, juice, maji, maziwa au hata peke yake.
   
 2. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwa iyo unanunua chokoleti idadi ya kiwango unachotaka pikia?
  nataka nijaribu kama itatokea ivo ilivo apo

  ni keki niyayopenda vibaya sana
   
 3. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  mkuu chocolate kiasi gani ..?!
   
 4. N

  Namour Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Asante kwa maujuzi sasa hiyo topping karanga si zitabaki juujuu,mi nataka ile ya karanga zikiwa ndan.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Dec 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Weka gunia zima...(just kidding) Kadiria mwenyewe unavyoona inafaa.
   
Loading...