Jinsi ya kutambua kama uzito umezidi

southern boy

Member
Jan 12, 2016
59
121
Katika maisha na kwa ajili ya kuwa na afya njema ni vizuri ukajua kama uzito uliokuwa nao umezidi, umepungua au upo sawa. Hii itasaidia kuepuka na baadhi ya magonjwa au matatizo ambayo huja baada ya uzito kuongezeka au kupungua.

Na pale unapogundua kuwa uzito umeongezeka au umepungua ni vizuri kuchukua hatua za haraka za kuongeza uzito kama umepungua au kupunguza uzito na kama umeongezeka.

Jinsi ya kungalia kama uzito wako upo katika hali gani

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (W.H.O) ili kutambua kama uzito umezidi, upo sawa au upo chini ya uzito utajua kwa kuangalia Body Mass Index (BMI). Na BMI inayotakiwa ni kati ya 18.5 - 24.9. Ili kutambua hiyo BMI yako kitu unachotakiwa kujua ni uzito katika kilogram na urefu wako katika mita. Ambayo unaweza kukokotoa kwa mlinganyo huu:-

BMI = uzito / (urefu x urefu )

Uzito katika kilogram na urefu katika mita.
bmi2.png

Kama BMI ni chini ya 18.5 basi upo chini ya uzito na kama ni katika ya 18.5 - 24.5 upo na uzito unaotakiwa. Ikizidi 25 basi uzito umezidi. Angalia jedwali hapa chini kuusu BMI na uzito

uzito.png

Au unaweza kuingiza moja kwa moja na kujua kuusu uzito wako kwa ku bofya hapa
Tambua uzito kama umezidi
 
Ndugu nadhani hiyo formula ina ukakasi , hata kabla sijatumia. Kwa units ulizotaja (sentimeta na kilogramu) basi labda wenye kilo kuanzia 200kg ndio watakaopata whole namba. Mtu mwenye kilo 60 na urefu wa sentimeta 180 atakuwa na BMI ya 0.00185
 
Naona sijui unazidisha mia. Maana ukienda kwenye hyo link ukafanya hvyo hvyo inaleta BMI kamili sio ya 0.0 sasa inakuwa inafanana na hyo lakni hyo haianzi na 0.
 
Ndugu nadhani hiyo formula ina ukakasi , hata kabla sijatumia. Kwa units ulizotaja (sentimeta na kilogramu) basi labda wenye kilo kuanzia 200kg ndio watakaopata whole namba. Mtu mwenye kilo 60 na urefu wa sentimeta 180 atakuwa na BMI ya 0.00185
 
Ndugu nadhani hiyo formula ina ukakasi , hata kabla sijatumia. Kwa units ulizotaja (sentimeta na kilogramu) basi labda wenye kilo kuanzia 200kg ndio watakaopata whole namba. Mtu mwenye kilo 60 na urefu wa sentimeta 180 atakuwa na BMI ya 0.00185

Nimeshaedit Mr. Ymollel urefu ni katika mita na siyo sentimeta
 
Ndugu nadhani hiyo formula ina ukakasi , hata kabla sijatumia. Kwa units ulizotaja (sentimeta na kilogramu) basi labda wenye kilo kuanzia 200kg ndio watakaopata whole namba. Mtu mwenye kilo 60 na urefu wa sentimeta 180 atakuwa na BMI ya 0.00185
amekwambia urefu uwe kwenye Mita na so sentimeta
 
Back
Top Bottom