Shemasi Jimmy
Member
- Apr 23, 2021
- 93
- 104
Na Shemasi Jimmy 0659 611 252
Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni uhakika wa mambo tusiyoyaona. Waebrania 11:1
Watu wa dunia hii hutangulia kushinda kisha wakashangilia lakini mtu wa Mungu hushangilia kabla ya kushinda kwa kua wanahakika ya kua kila walioliomba kwa Imani litageuka na kua lao.
Yakobo alitangulia kushinda hata kabla ya ushindi wenyewe. Alijua kucheza na hisia za kaka yake ambaye hakuona umuhimu wa nafasi yake ya uzaliwa wa kwanza na kisha kuiuza kwa gharama ya mlo mmoja(sahani ya dengu). Kwa sababu alikua na maono, maono ni kujenga nyumba kabla ya kuanza ujenzi, kufika unapoenda kabla hujaanza safari. Kumaliza mwaka kabla hujauanza. Kuona mafanikio ya biashara yako hata kabla ya kuanza kupata faida. Hayo ndio maono na hiyo ndio Imani tunayopaswa kuijenga.
Mara nyingi wenye maono hutangulia kushukuru hata ingawa hawajapokea chochote kutoka katika maombi yao. Kwa maana neno Mandiko yanasema tunaenenda kwa Imani na si kwa kuona, utakua umeibatilisha Imani ikiwa utahitaji kuenenda kwa kuona.
Wenye maono sio wepesi wa kukata tamaa kwa maana wanaamini kua lipotumaini pasipo na tumaini, ipo njia pasipo na njia, upo mwanga pasipo na mwanga. Ndio maana Yusufu hakukataa kuuzwa kwa waishimael, hakupingana na mashitaka bandia aliyobambikiwa na mke wa Potifa hata ingawa alikua mwenye HAKI. Hakupinga kwenda kwa mfalme kutafasiri ndoto, hakusita kuonesha unyenyekevu na hata kuishauri serikali ya farao juu ya matumizi mazuri ya chakula na mipango thabiti ya kuifadhi chakula. Hakuonesha nia ya kuitaka kazi hiyo kwa kua alikua na maono juu ya mwisho mwema wa maisha yake ya gerezani. Mwisho tunaona farao anaunda cheo kipya katika serikali yake ambacho kitaendana na hadhi na heshima ya Yusufu.
Israeli walipokua wakienda vitani walikua na tabia ya kuuliza manabii wao juu ya hali ya mbeleni. Neno ndio ushindi hakuna
Mwanadamu anamajibu ambayo Mungu amempa ila switchi ya ushindi wa matatizo hayo ni matatizo. Uwezo wa mwanadamu huonekana baada ya kukutana na mnama wa kutisha. Mfano mwanadamu anapotembea na gahafla akatokea simba, utashuhudia uwezo halisi wa yule mtu katika kujinusuru.