Jinsi ya kurejesha heshima yako katika jamii

Jinsi ya kurejesha heshima yako katika jamii

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
Hakuna kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini kuliko kawaida kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara makubwa.

Kitaalamu hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako ndani ya jamii unayoishi kunatokana na jinsi unavyotenda mambo yako.

Ninaposema hivyo ninamaanisha kuwa matendo yako, muonekano wako, kuzungumza kwako kunaweza kukufanya ukaonekana kituko na kushushwa daraja katika jamii.

Mwalimu wangu wa somo la maisha na saikolojia, Bw. Eric Shigongo aliwahi kuniambia ‘Nothing happens in the sky, but the elements should be there’ akimaanisha kuwa hakuna kitokeacho angani pasipo kuwa na dalili au sababu zake.

Naomba nianze kutoa njia za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujenga heshima yako.

MUONEKANO

Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani.

Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi. Linaweza kuwa jambo dogo sana lakini ni moja kati ya sababu kubwa inayochangia kuporomoka kwa thamani yako kwa watu.

Maana itafikia sehemu watu wanakwepa kuongozana na wewe kwa hofu ya kuaibika mtaani. “Tusiongozane naye atatutia aibu bure, mchafu sana bwana.”

Mazungumzo
Hapa naomba nieleweke kuwa unachokizungumza kinaweza kukujengea heshima au kukubomolea. Kauli zisizo na busara zitakufanya udharaulike kwa kila mtu. Uropokaji usiokuwa na mantiki huchangia kuporomosha heshima yako hasa kama utakuwa muongeaji zaidi.

UTENDAJI KAZI WAKO
Ndugu zangu, siku zote heshima ya mtu ni kazi. Watu wengi hawapendi kufanya kazi kwa bidii huku wengine wakijiendekeza kwa tabia ya kuombaomba, jambo hilo halifai kwa vile huchagia kubomoa heshima yako mbele ya jamii.

KUTOTIMIZA AHADI
Kama una tabia za kuahidi mambo halafu unashindwa kuyatekeleza, basi unajiweka katika nafsi mbaya ya kutunza heshima yako katika jamii unayoishi. Bora ukwepe kutoa ahadi kuliko kuahidi na kutotimiza.

SIFA ZISIZO NA MAANA
Nakumbuka msemo mmoja kutoka kwa Mwandishi mwandamizi aliyekuwa mtaalamu wa falsafa za maisha, Marehemu Adolf Balingilaki ambao unasema:

‘Ukitafuta heshima kwa gharama ya juu, basi utalipwa dharau kwa bei nafuu’
Msemo huu unamaanisha nini? Siku zote ukiwa unafanya mambo yako kwa ajili ya kusifiwa au mazungumzo yako kuwa ya kujifagilia na kujiinua basi watu huishia kukudharau na kukuona mshamba wa maisha.

Kwani hata katika maandiko matakatifu yanasema ajikwezaye hushushwa. Hivyo kujigamba na kujikweza kwako huchangia kwa kiwango kikubwa sana kuporomosha na kuondoa kabisa heshima yako hivyo kubaki mtu wa kudharauliwa tu.

KUTOKUWA MWAMINIFU
Suala la uaminifu ni pana, kuna uaminifu wa fedha, siri, dhamana na mambo kama hayo, hivyo ni vema kila unachoaminiwa lazima ukitunze ukiwa mtu wa kuvunja uaminifu fahamu kuwa utashusha heshima yako.
 
Hakuna
kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini kuliko
kawaida kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara
makubwa.


Kitaalamu hakuna jambo ambalo hutokea
maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako ndani ya
jamii unayoishi kunatokana na jinsi unavyotenda mambo
yako.


Ninaposema hivyo ninamaanisha kuwa matendo
yako, muonekano wako, kuzungumza kwako kunaweza kukufanya ukaonekana
kituko na kushushwa daraja katika jamii.


Mwalimu wangu wa somo la maisha na
saikolojia, Bw. Eric Shigongo aliwahi kuniambia ‘Nothing happens in the
sky, but the elements should be there’ akimaanisha kuwa hakuna
kitokeacho angani pasipo kuwa na dalili au sababu zake.


Naomba nianze kutoa njia za kukusaidia
kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu
zinazoweza kukusaidia kujenga heshima yako.


MUONEKANO

Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana.
Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla.
Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata
kama ana kipaji kikubwa kiasi gani.


Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili
huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi. Linaweza kuwa jambo
dogo sana lakini ni moja kati ya sababu kubwa inayochangia kuporomoka
kwa thamani yako kwa watu.


Maana itafikia sehemu watu wanakwepa
kuongozana na wewe kwa hofu ya kuaibika mtaani. “Tusiongozane naye
atatutia aibu bure, mchafu sana bwana.”


Mazungumzo
Hapa naomba nieleweke kuwa unachokizungumza
kinaweza kukujengea heshima au kukubomolea. Kauli zisizo na busara
zitakufanya udharaulike kwa kila mtu. Uropokaji usiokuwa na mantiki
huchangia kuporomosha heshima yako hasa kama utakuwa muongeaji
zaidi.


UTENDAJI KAZI WAKO
Ndugu zangu, siku zote heshima ya mtu ni
kazi. Watu wengi hawapendi kufanya kazi kwa bidii huku wengine
wakijiendekeza kwa tabia ya kuombaomba, jambo hilo halifai kwa vile
huchagia kubomoa heshima yako mbele ya jamii.


KUTOTIMIZA AHADI
Kama una tabia za kuahidi mambo halafu
unashindwa kuyatekeleza, basi unajiweka katika nafsi mbaya ya kutunza
heshima yako katika jamii unayoishi. Bora ukwepe kutoa ahadi kuliko
kuahidi na kutotimiza.


SIFA ZISIZO NA MAANA
Nakumbuka msemo mmoja kutoka kwa Mwandishi
mwandamizi aliyekuwa mtaalamu wa falsafa za maisha, Marehemu Adolf
Balingilaki ambao unasema:


‘Ukitafuta heshima kwa gharama ya juu, basi
utalipwa dharau kwa bei nafuu’

Msemo huu unamaanisha nini? Siku zote ukiwa
unafanya mambo yako kwa ajili ya kusifiwa au mazungumzo yako kuwa ya
kujifagilia na kujiinua basi watu huishia kukudharau na kukuona mshamba
wa maisha.


Kwani hata katika maandiko matakatifu
yanasema ajikwezaye hushushwa. Hivyo kujigamba na kujikweza kwako
huchangia kwa kiwango kikubwa sana kuporomosha na kuondoa kabisa heshima
yako hivyo kubaki mtu wa kudharauliwa tu.


KUTOKUWA MWAMINIFU
Suala la uaminifu ni pana, kuna uaminifu wa
fedha, siri, dhamana na mambo kama hayo, hivyo ni vema kila
unachoaminiwa lazima ukitunze ukiwa mtu wa kuvunja uaminifu fahamu kuwa
utashusha heshima yako.

Kha! Mwalimu wako ni Shigongo? Huyu anaekula kwa mgongo wa kuwachafua wengine? Duh hata hizo point zako zimekuwa bure kabisa
 
Kha! Mwalimu wako ni Shigongo? Huyu anaekula kwa mgongo wa kuwachafua wengine? Duh hata hizo point zako zimekuwa bure kabisa

watu bana, wanajichafua ndio maana shigongo anapitia mgongoni kwao, kufa kufaana , maisha yenyewe ndo hayahaya
 
Back
Top Bottom