Jinsi ya kupunguza Data Transfer | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kupunguza Data Transfer

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kang, Mar 26, 2009.

 1. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Watanzania wengi tunatumia Internet connection zenye "Data Cap" kwa mwezi e.g 2GB kwa Mwezi au ambazo unalipia kulingana na matumizi e.g 200Tsh kwa Megabyte. Hapa nitaorodhesha baadhi ya vitu unavyoweza kufanya ili kupunguza matumizi hayo ya Data.

  Add-On ni nini? Add-On inaongeza feature fulani kwenye Browser ambayo haipo kwenye official version.

  Kwa upande wa browser nitaongelea Firefox lakini tofauti sio kubwa sana ukiweza kupata Add-On za Internet Explorer.

  Add-On zote za Firefox zinapatikana hapa.
  https://addons.mozilla.org/en-US/firefox/
  Dumbukiza jina kwenye hiyo search tu!  1. Zima Picha

  Picha zinachukula Data sana ukifananisha na maandishi, hivyo ukizima picha utapunguza sana matumizi. Add-On nzuri ya kuzima picha ni ImgLikeOpera hii inakuwezesha kuzima/kuwasha picha jinsi utakavyo pia inaweza kuruhusu picha ambazo ziko kwenye cache(Ziko kwenye PC tayari hivyo hazili data) peke yake.

  2. Zima Flash
  Flash inatumika kuweka animation kwenye websites na pia kuonyeshea video kama za Youtube, hizi zinachukua data nyingi sana na hiyo kuzizima inasaidia sana. Add-On ya kuzima Flash Inaitwa FlashBlock, hii inazuia Flash na inakuruhusu kuiruhusu Flash ya site fulani kwa urahisi ukitaka.


  3.Zima matangazo (Ads)
  Matangazo ni kama Banners na hata ya maandishi (e.g Google Ads)
  Add-On ya kuzuia matangazo inaitwa Adblock Plus. Inazuia matangazo automaticaly, pia uaweza kuruhusu matangazo fulani kirahisi kama unataka.
  Kitu kimoja cha kufikiria ni kuwa website nyingi zinajiendesha kwa kutegemea mapato ya matangazo, hivyo kuzuia matangazo inaweza ikafananishwa na wizi!:)


  4. Zima Updates
  Windows Updates unaweza kuzizima kwa kwenda kwenye control panel >> Security Centre. Hizi zinaweza kuwa 100Mb or more each! So kuzizima ni muhimu!

  Antivirus Updates >> Sikushauri kuzizima! kwa sababu za kueleweka.

  Program zengine kama Adobe Reader nazo zinafanyaga Auto Update, uzimaji unategemea na program ila mara nyingi ni kwenye Options somewhere.

  Kama kawa maswali Welcome, nitajaribu kuuleza zaidi kama kuna kitu hakijaeleweka!
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  200 Tsh per Megabyte?
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Yes?!
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Huwa nabadilisha Antivirus update schedule; badala ya "kila siku" naweka kila wiki. Updates itafanyika mara 4 tu kwa mwezi.

  Kwa wale wanao-download email nyingi, mfano ume-subscribe kwenye "groups" kama vile eThinkTankTz, kuna settings zinazoweza kukusaidia ikiwa email account yako umei-configure kwenye Outlook.
  Tools - Send/Receive - Send/Receive Settings - Define Send/Receive groups
  Edit - Download headers only.  Halafu ukizingatia wingi wa spam siku hizi!
   
Loading...