Jinsi ya kupika chapati za nazi na nido

princewilly

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
259
526
MAHITAJI
Unga wa ngano 1kg
Maziwa ya nido vijiko viwili vya chakula
Blue band vijiko viwili vya chakula
Mafuta ya kupikia nusu lita
Nazi moja pia unaweza tumia nazi ya pkt
Chumvi kijiko kimoja cha chakula
Sukari vijiko viwili vya chai

JINSI YA KUKANDA
Unachukua unga wako unaweka kwenye bakuli alafu unaweka maziwa yako ya unga pamoja na chumvi na sukari ukishamaliza unachanganya alafu unachukua blue band yako unaweka then unachanganya ili blue band ichanganyikane na unga vizuri inakupasa uchanganye na mikono yote miwili uku ukipikicha unga wako taratibu hatua inayofata unachukua tui lako la nazi inatakiwa liwe kama nusu lita hiv.

Then unaanza kukanda uku ukiweka maji kidogo kidogo mpaka pale unga wako utakuwa mlaini usikande ukawa mgumu chapati zako hazitakuwa nzuri hatua inayofata unaendelea kukanda unga wako mpaka Ulainike kabisa unaweza pia ukaongeza blue band kidogo ili unga uweze kuwa mlaini ukishamaliza kukanda funika tonge la unga vizuri hakikisha unafunika vizuri kama lisa limoja hivi litaufanya unga wako kuwa mlaini zaidi.

Hatua inayofata unakata unga wako matonge ya wastani ukishamilaza sukuma matonge paka mafuta alafu unayafunga ukishamliza weka kikaangio chako jioni hakikisha moto unakuwa wa wastani ili chapati zako ziweze kuiva vizuri na pia zisibabuke sukuma tonge lako vizur chapati ziwe za wastani
93672a8fcc57be1325a2d84b00777bb0.jpg
879890274335cb25b67f844e18ec2425.jpg
4435b76750fd0559ae4d16b12c82559d.jpg
nimejaribu kuweka video nimeshindwa
6dbfb54f4f873f1c76876f65a385171f.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom