Jinsi ya Kupata Kazi (Part 1)

Jinsi ya Kupata Kazi (Part 1)

dr_vivo_dar

Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
17
Reaction score
12
Kama bado unahangaika kupata kazi. Nitakupa wazo moja litakalokusaidia kupata kazi kwa haraka. Kama unataka lakini.

Huu sio ushauri. Bali ni "wazo." Unaweza ukatekeleza au ukapuuzia. Uamuzi ni wako.

Mwaka 2016 nilipataga kazi Tigo. Ilikuaa ni connection niliyopewa na mtu ninayemjua. Ilikua ni kazi ya sales. Wanaitwa Direct Sales Agents.

Nilikuwa nalipwa katika mfumo wa commission. Na kuna kipindi nilipata wateja wengi kiasi kwamba nikawa natengeneza zaidi ya milioni 1 kwa mwezi..Fresh from school.

Kazi kubwa ilikuwa ni kutafuta wateja wanunue vifurushi ambavyo vinalipiwa baada ya siku 30. (Postpaid)

Nilikuwa natembea juani mpaka suti niliyokuwa navaa ikapauka. Lakini nilijifunza mengi. Na nikakutana na watu wengi. Na nikatengeneza uwezo wangu wa ku "hustle" kutafuta hela.

Nilijifunza kushawishi watu wanipe hela. Na staff wenzangu walikuwa wananichukulia mimi kuwa namba 1.

Unaweza ukawa unawaza: mimi sio mtu wa sales. Sina uwezo kuongea saaana.

Mimi mwenyewe pia sio muongeaji. Lakini mpaka leo nipo kwenye hii tasnia. Na maisha yanaendelea.

Nilichojifunza ni kwamba wateja hawanunui bidhaa yako kwasababu unaongea sana. Wananunua kama "wanataka" bidhaa unayouza. Unaweza ukawachekesha lakini kama hawana hitaji hawatanunua.

Unapataje kazi kama hii?

Temebelea Sales office yeyote ya makampuni ya simu. Tafuta "Team Leader" mwambie una uwezo wa ku convince wateja. Mpe CV. Tembelea ofisi nyingine. Fanya hivyo mpaka ufanikiwe.

Kazi huwa zipo. Wanachotaka Team Leader ni watu wenye uwezo wa kuwaletea wateja.

Vaa vizuri. Nyoa nywele. Kata kucha. Tafuna big ji. Hakikisha "muonekano" wako unakuuza. Na hakikisha unaongea kwa uchangamfu. Na hakikisha unaenda na CV. Hakikisha pia unatembelea ofisi zaidi ya moja.

Ongea pia na watu wao wa sales. Waambie na wewe unataka kuwa kama wao. Unatafuta kazi. Omba wakuunganishe na Team Leaders wao. Na jifunze kutoka kwao.

Pointi ya ujumbe huu ni hii: Kama bado huna kazi anza kwa kutafuta kazi za sales. Ni rahisi sana kuzipata. Wajasiriamali wote wakubwa walianza kwenye sales. Ndio ujuzi unaohitaji kama unataka kutengeneza hela nyingi. Kupanda cheo kazini n.k

Na ukifanikiwa kupata kazi soma kila kitabu cha sales. Na tekeleza unachojifunza. Kila la kheri.
 
Wazo zuri, Hicho unacho sell kiwe on demand otherwise nahisi utapoteza nauli na muda bure.
 
Nilipiga izi kazi wakati nipo chuo ... noma sana ilikua direct una report kwa Chanel Manager wa Airtel.... dealing na corporate customers ... tumekaa sana kijiwe cha wazee wa mjini Mkwepu street na Gymkhana 😂
 
Wakati unaingia ndio nilikuwa nimeacha na kuhamia taasisi nyingine, nimefanya hizo mishe lakini haikuwa rahisi kazi ilikuwa ngumu ile halafu pesa nayo ikawa haba sana ukilinganisha na mahitaji!

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom