Mwanambugulu
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 682
- 863
- Thread starter
-
- #21
Nashukuru mkuuUswauri mwingine wakukusaidia tu.
Anza kuuza vitu ambavyo uko navyo lakini hivihitaji.
Hapo ndani kwako kuna nini?
Uko na viatu havijaisha sana na huvivai?
Uko na chochote usichotumia?
Uza.
Nakwambia watu wanafikiri haiwezekani lakini inawezekana sana tu.
Ukipata chapaa kidogo nenda sehemu wanauza vitu bei rahisi nunu halafu uza kwa bei ya juu.
Watu watanunua tu. Muhimu uwe na "jicho" la kujua bidhaa watu wanahitaji
Lenga kwenye product inayotatua changamoto za wateja unaowalenga.
Kama umwemwona mtu amevaa shati kuukuu na wewe una shati zuri lakini hulivai mshawishi umuuzie.
Jifunze kuwa seller.
Usijiaminishe na hiyo elimu uchwara uliyonayo.
Hii njia yakujifunza kuuza inaweza tengeneza spirit ya ajabu siku moja ukawa mfanya biashara.
Nashukuru sana mkuu talifanyia kazi hilihongera kwa kuwa mstahimilivu na kaza mkuu, mi sikupi pole.
Kuna wakati unatakiwa kuweka vyeti ndani, na kuomba kazi ya ujumla, mfano
*juzi kati red cross walitangaza nafasi, ile ilikuwa fursa tosha maana kuna nafasi hazihijaji vigezo vya kitaaluma sana.
*restaurants nyingi wafanyakazi wanasumbua sumbua, tumia hiyo nafasi kuomba kazi popote hata kuhudumia wateja, baadaye haohao wateja wanaweza kuwa chanzo cha wewe kupata deal jingine.
*mtaani kuna vikundi vya vijana vilivyosajiliwa na vinakopesheka, unaweza tafuta kimoja ujiunge kama njia ya kutokea.
*badala ya kuchat sana mtandaoni, tumia mda kupitia sites za ajira,bila shaka unazifahamu mbili tatu kila baada ya siku kadhaa kuona updates.
* jifunze taaluma mpya kila siku ukiwa free kwa kutembelea workshops tofautitofauti za watu na kujenga nao urafiki.
hasta la vista[emoji123][emoji123]
Duh nao n mtazamoKuna kitu binafsi kinanipa shida kwanini Biashara inaonekana ni kazi ya walioshindwa maisha!!
Mtu yoyote aidha aliajiriwa kastaafu au kafukuzwa kitu cha kwanza biashara hii ndio sababu watu wanashindwa biashara sababu ni hiyo
Ushauri wangu kwako....hapa mjini unatakiwa kukomaa bila kujali kazi gani unafanya muhimu uwe na malengo kwamba hii kazi ninayofanya ni kama daraja kunifikisha ninakotaka kwenda
watu wengi wanakwama hata akipata kibarua kidogo anaoa mwisho maisha yanakufa kabisa
Hebu ch kukusaidia nenda tawi lolote la bancAbc walizitqngaza nafasi za DSA wanachukua tu mtu yoyote wakiona anafaa kwa kuwa busy kwanza ili akili isipate kutu na kuongeza uzoefu na kazi yao ni kuziuza product zao na kwa kuwa wanatangaza na internal vacancy kwa kuwa wametanua matawi dodona na mwanza basi itakua rahisi kupata ajira ya kudumu,hiyo DSA mshahara wako ni namna unavyouza hizio account so kambi popote anza mdomdo....maana kila aliefanikiwa asilimia kubwa wamepitia changamoto nyingiMkuu nina bachelor of taxation from institute of finance management (2014)
Pia nguvu za kutosha kufanya kazi yoyote ile na eneo lolote lile kwa uwezo wote
Uzuri sichagui kazi kabisa
Pia ni mwaminifu na mchapakazia
Mbona unamtishaWait umesoma Tax ? haki utaendelea kulalama labda ukajiajiri!
Mkuu ngoja niende sasa hivi nalifahamu tawi lao pale posta ngoja nipeleke cv leo leo mana kila kitu kipoHebu ch kukusaidia nenda tawi lolote la bancAbc walizitqngaza nafasi za DSA wanachukua tu mtu yoyote wakiona anafaa kwa kuwa busy kwanza ili akili isipate kutu na kuongeza uzoefu na kazi yao ni kuziuza product zao na kwa kuwa wanatangaza na internal vacancy kwa kuwa wametanua matawi dodona na mwanza basi itakua rahisi kupata ajira ya kudumu,hiyo DSA mshahara wako ni namna unavyouza hizio account so kambi popote anza mdomdo....maana kila aliefanikiwa asilimia kubwa wamepitia changamoto nyingi
Sawa fanya hivyo,na uzuri product zao zinauzika sana hasa prepaid card....ukifanikiwa useme....pia angalia nafasi walizotangaza maana kuna matawi mapya dodoma na mwanza bancAbcMkuu ngoja niende sasa hivi nalifahamu tawi lao pale posta ngoja nipeleke cv leo leo mana kila kitu kipo
Takupa mrejesho mkuu
Pole sana..ila usichoke kutuma maombi ya Kazi ipo siku yako tu Mungu atatenda
Nakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
Rugha LughaNakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
Ajira zimekua ngumu sana ndg,wengi hutumia mbinu ya kuomba internship na wakikubaliwa huwa wanapiga kazi hatari yan wanaonesha juhudi zote ktk utendaji kazi wao mpaka boss anashawishika kuwaajiri. ishu hapo ni kwamba hiyo pesa ya kwendea huko ofsini kufiga internship itatoka wapi, hapo ndo kasheshe mana maboss wengine wanaweza wakakukaushia hata miezi hawakuajiri mpaka mwenyewe unaamua tu kuondoka. Usikate tamaa ndg,endelea kupambana one day yesWakuu habari za muda huu?
Niende moja kwa moja kwenye mada mimi ni kijana wa late 20's nilimaliza shule mwaka 2014 lakin paka leo sijapata ajira rasmi zaidi ya kuunga unga tu na mission town za hapa Dar es salaam
Mzee wangu ni mkulima pia mama ni mkulima nina dada na ma kaka bahati mbaya wote walikimbia umande (shule) basi mimi tu ndio nilichomoka kwenye familia nikafika paka chuo sasa mzee alikua na matumaini sana na mimi pia na ndugu wengine ni kama walielekeza sana matumain yao ya mafanikio kwangu.
Kama unavyojua kwa familia zetu za wakulima huko ni kwamba ili uonekane msomi basi inabidi ukimaliza shule upate kazi alafu usaidie issue kidogo za home
Sasa wakuu mimi nimehangaika sana kupata ajira huwa naishia kupata zile za mikataba miezi mi tatu lakini mwisho hakuna kitu na malipo yake hayakizi kabisa(saizi hata hizo sizipati yena).Nimepiga vibarua hadi na watu wa darasa la saba viwandani lakin pesa unapopata unaishia kula na kodi tu
Nimesambaza cv katika makampuni kibao (auditing firm) za Dar lakin paka leo naona kimya pia mabenk na sehemu zingine lakin kupata ajira imekua ngumu sana
Nime fight sana angalau nipate mtaji basi nifanye hata biashara lakin familia ninazotokea ( pamoja na familia za ndugu) wote kwanza ndio wanasema bora umesoma sasa utusaidie na ww
Nikiangalia home hali ni mbaya sana sasa kimbembe kipo saizi hapa nadaiwa kodi mwezi ujao alafu ndani pia misosi imekata kabisa pia baya zaidi pesa hata nauli ya kutoka ili nizunguke imekata kabisa nimebaki home tu.
Nazunguka viwanda vya karibu kidogo hapa angalau nipige mzigo nipate hata hela ya gesi nako wiki hii wamenizingiua vibaya yani wanaita watu kwa kujuana bahat mbaya mimi sina ninae mjua
Juzi nimepiga dili kwenye kiwanda cha kufyatua matofali aisee nimekimbiza mzigo kuanzia asubui paka saa kumi na moja beba sana matofali nikaja kuramba elfu kumi jioni lakin nimeamka naumwa vibaya sana paka sijielewi yani
Mbaya zaidi nikiwaangalia washikaji zangu ambao tulikua tunapiga msuli pamoja aisee wameramba ajira saizi maisha smooth kabisa yani wanafunga ndoa tu alafu mi nikucheki geto cha muhimu ni kitandani tu labda na ka kompyuta kangu mana kuna madini
Sasa wakuu kwa waliowahi kukutana na changamoto kama hizi hivi mliwezaje kuzitatua? Mana hapa nina mawazo kiasi kwamba mda mwingine nawaza hadi najiogpa
Mbaya zaidi nilikua na rafiki wa kike (girlfriend ) wakati wote hatuna mission ilikua poa bahati nzuri akapata kazi mkoani basi ahadi kikawa nyingi pia alikua ananipaga tafu sana ila baada ya kama miezi 6 hivi mambo yakabadilika akawa hasomeki tukawa tunawasiliana tu hivo hivo ila ghafla simu yake ikawa haipatikani mwezi uliopita nimeona picha za harusi yake
Usiku silali aisee kichwa kinauma pia naweza Kuhisi njaaa lakini mda mwingine najikuta nimekata hata masaaa 18 bila kutia kitu na niko fresh tu
Nikiangalia matumaini wakati nasoma daah pia nikiangalia wanavyonichukulia kule home mkoani na mategemeo yao basi napotea kabisa
Ushauri wenu wakuu ili niweze kujikontroll angalau hata nipate usingizi mana situmiii kilevi chochote sasa usiku unakua mrefu sana alafu mchana ndio natembea kama chizi vile sielewi napishana na watu siwaelewi wengine hata siwaoni
Vyeti vinapata vumbi tu pia mtaji ndio hakuna daaah. Wakuu hebu nipeni ushauri nipunguze huu msongo wa mawazo
Nawasilisha,,
Wewe mkosoaji mwenyewe umeandika upupu rugha=lugha , jf kila mtu mjuaji/msomi sasa kama huna cha kumshauri ungekaa kimya tu,sio kukosoa halafu we mwenyewe dishi limepoteza networkNakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
Mkuu haya mambo sio ya kuchukulia serious watu tuko tofauti sanaWewe mkosoaji mwenyewe umeandika upupu rugha=lugha , jf kila mtu mjuaji/msomi sasa kama huna cha kumshauri ungekaa kimya tu,sio kukosoa halafu we mwenyewe dishi limepoteza network
Huu ni wivu wa wazi wazi unauonesha kuhusu elimu ya jamaa. Wapo wenye PhD na wanakosea kuandika kama kawaida. Kumbuka jamaa hajaenda kusomea mambo ya uandishi wa habari huko chuoniNakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.