Asali inauwezo wa kung'arisha ngozi yako kwa sifa yake kuu ya kuzuia na kupambana na uchochezi wa chembechembe za bakteria katika ngozi, hivyo inasaidia kupunguza muonekano wa makovu na kuchochea afya ya ngozi. Chembechembe za umajimaji za asali na mafuta ya nazi pia zinasaidia kuboresha seli ya ngozi, pia kufanyia masaji mchanganyiko huu inasaidia kuboresha mzunguko, ukuaji na pia ufufuaji wa seli za ngozi.
JINSI YA KUANDAA MCHANGANYIKO HUU.
1) Weka kijiko kimoja cha chai cha asali mbichi katika bakuli yako safi ya mchanganyiko.
2) Changanya na kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi katika bakuli yako yenye asali.
3) Changanya vizuri na paka mchanganyiko wako kwenye eneo lililo athirika kwa kusugua taratibu kutumia ncha ya kidole chako.
4) Endelea kusugua taratibu kwa dakika moja au mbili, kisha weka kitambaa kilichochemka na maji ya moto kwenye eneo ulilopaka mchanganyiko wako mpaka kipoe.
5) Rudia hivyo kila siku utayaona mabadiliko baada ya wiki mbili.
N.B Inashauriwa kutumia asali mbichi ambayo haija chakachuliwa.
Usisahau kuleta matokea baada ya wiki mbili.
Kwa maswali zaidi andika hapo chini ili watu wajifunze usinitumie PM maana sitakujibu.
Asanteni, by Mugisha.
Sent using
Jamii Forums mobile app