Old Member (Retired)
JF-Expert Member
- Sep 29, 2012
- 3,401
- 1,618
Yaani madalali wamekuwa kero miji mingi Tanzania hasa jiji la Dar, wiki chache zilizopita gazeti moja liliripoti kuwa kuna madalali mpaka ikulu wanaotapeli watu kwa kusema wanawatafutia ajira ofisi ya raisi.
Sasa wewe ukitaka kumzunguka dalali, unaweza sema unataka kiwanja then yeye ataenda kukuonyesha hicho kiwanja na baada ya yeye kukuonyesha hicho kiwanja unamwambia ngoja nikafikirie then ndani ya wiki hii nitakutafuta.
Baada ya hapo we keshon yake unarudi mpaka kwenye kile kiwanja unawauiliza majirani nani ni mmiliki wa hicho kiwanja utaambiwa ni fulani na anaishi wapi na utaomba namba yake ya simu kisha unampigia simu unamueleza shida yako mtapanga jinsi ya kuonana kisha unafanya manunuzi. Utakaposhangaa ni pale mwenye kiwanja atakwambia kiwanja anauza milioni 8 wakati dalali alikwambia kinauzwa milioni 20.
NB: Tumia ujanja huo au unaofanana na huo na unaweza kuuboresha zaidi katika madalali wa kila aina waotaka pesa za bure kwa kushinda vijiweni
ww kweli bado mgeni Dar Es Salaam karibu sana...unadhani watu wote wanaotafuta chumba/kiwanja hawana mawazo kama hayo!?
kwa taarifa yako huku mjini mwenye nyumba/kiwanja hawezi kukuuzia kitu chochote bila uwepo wa dalali na hata ukienda kwake straight atakwambia nenda kwa dalali uje nae hayo ndio makuliano yao

Kweli kabisa dalali professional huwezi kumzunguka. Wale jamaa wakishaoneshwa mali hata mwenyewe akiuza wanakwenda kudai chao kwani huwa wameingia makubaliano. Ila kama ni dalali wa jua kali hapo unaweza kumzunguka. Dalali kamili yeye hukabidhiwa mali na mwenye mali hawezi tena kurudi na kufanya mapatano na mteja. Na kama wewe ni mwenye mali ukijifanya kumzunguka dalali wakati ulishampa dili anaweza hata kukuua au hata kukufilisi mali yako. Madalali ni watu muhimu sana kwani ndio wanaotafuta masoko. Unaweza kuwa unauza kitu wewe mwenyewe kisinunuliwe lakini ukimpa dalali hakichukui round.Labda kama hicho kiwanja hakijakamatwa na dalali mzoefu. Dalali mzoefu huwezi kumzunguuka kitoto hivyo!..yeye ndio anamiliki kiwanja na mwenye mali anamsikikiza yeye!..mikataba yote anatengeneza dalali na mwenye mali anasikiliza tu! Wewe umekutana na dalali underground
Kiukweli hawa jamaa wababoa na kila kukicha wanazidi kuongezeka na kujikita kila mahali. Hata sokoni ukienda mkulima/mfanya biashara hana nafasi ya kuamua bei bali madalali.
Siwapendi na nikishajua na deal na dalali siendelei tena na hiyo biashara.
Najua hata humu wapo, hapo juu nimewasoma na nitaendelea kuwasoma lakini siwapendi. Jitu zima linakaa mjini halifanyi kazi unasubiri mtu ahame uanze kudalalia chumba. Jenga yako.