Mhh ni changamoto kweli...but kwa uelewa wangu ,hongera na endelea kujenga mazingira ya kirafiki akueleze anayopitia huku ukimpa live madhara ya kuanza mahusiano akiwa mdogo,kuangalia porn na pia mueleweshe kuhusu condoms mana ni wazi kama hajaanza basi ataanza siku si nyingi si unajua tena wanaume wanawahi (relatively to girls ),nakumbuka my mom na mamdogo walikuwaga so open na confidence za kutosha watu mnapewa lecture kabla ya kwenda shule ,chuo nk,imetusaidia..mi sio mzazi yet so sijui mengi, watasema vizuri wenye experience
alichonijibu'Mama usiwe na hofu na mimi pili wasichana wa shule wanajigonga wenyewe niwatake ili niwasaidie Mathe..sasa mimi niwaachie? Eeh mungu wangu nilichoka nabaki kujiuliza
Shida imeanzia hapa kama mtoto umemlea kwenye maadili mema atathubutu kukuambia mimi niwaachie? umemzoesha hivyo.
Huyo ilikuwa ni kiboko tu,matokeo ya kuwalea watoto kama yai ndiyo haya.
"Usimnyime mtoto mapigo"
"umlee mtoto katika njia impasayo hata akiwa mzee hataiacha"
mhhhhhh ulikosea hapo kwenye simu ungeanza kumpa kitochi badala ya smart phone
pamoja na yote kijana wako yaonekana ameshajiingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi mpaka anawatch porn movies lakini hujachelewa sana jaribu kufatilia na marafiki alionao huko shule na mtaani pia kuhusu simu waweza mpa nokia ya tochi kwa sasa huku ukimwahidi akionyesha mabadiliko utambadilishia aina ya simu muhimu mtafutie majarida ya fema mkae mkisoma pamoja ajue madhara ya ngono katika umri mdogo
Tatizo simu za tochi au zisizo access internet hazitaki....na nilimbadilishia ndio kwanza kaiweka kwenye droo
Habari wana Jf
Jamani nina mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 15 wa marehemu dada yangu(Mwenyezi mungu amrehemu huko aliko)bahati mbaya mama yake alifariki kipindi cha uzazi kwa hiyo anajua mimi ndiye mama yake mzazi ,sababu nimemlea mpk sasa
Naomba kusema nampenda sana huyu mtoto nafanya kila niwezalo apate kile kilicho bora na kusema kweli ni kijana mwenye akili sana darasani ameshapat awards kibao toka yuko primary mpk sasa secondary.
Kesi zilianza kipindi cha pasaka alimwandikia mwanafunzi mwenzie wa kike love letter ambayo ilikuja kushikwa na wazazi wa binti huyo, wale wazizi wa huyo binti walichukia sana wakaniita nimuonye kijana wangu hawataki mazoea na binti yao.
Nikaa na mtoto wangu kirafiki na kuongea nae kuhusu kujiushisha kimapenzi katika umri mdogo alichonijibu'Mama usiwe na hofu na mimi pili wasichana wa shule wanajigonga wenyewe niwatake ili niwasaidie Mathe..sasa mimi niwaachie? Eeh mungu wangu nilichoka nabaki kujiuliza ina maana keshaanza ule mchezo wa kikubwa? Sipati jibu.
Tatizo la pili limetokea wiki 2 zilizopita baada ya kufanya vizuri darasani na kushika nafasi ya kwanza alitaka zawadi ya simu na mimi kuwa na furaha ya matokeo yake nikamnunulia Sony utra z smartphone japo nilimuekea masharti na mipaka ya kutumia simu....sasa kuna siku nimemfuma anacheki porn movies kwenye simu yake nilichukia na uamuzi nikampokonya na simu yenyewe.
Sasa kilichotokea kanuna hataki kula au akila ni kidogo sana ,haongei wala kucheka kama zamani ,mpk mwl wake amenoti mabadiliko yake darasani akifika shule yeye ni kimya tu hata akiulizwa swali hajibu.
Jamani nifanyeje sasa au ndio balahe? Msaada niishi nae vipi kijana akianza balahe?
Samahi kwa kuandika maelezo marefu
Nafikiri najitahidi kumlea katika malezi mazuri na ya kirafiki zaidi na uwazi kwa kunijibu hivyo sioni kama ni big deal
basi mtafutie ya kawaida yenye internet lakini sio smart phone yuko kidato cha ngapi kwa sasa
Muombee.Au mtafutie watu wenye nguvu za Mungu wamuombee.Bado hujachelewa nae na hakuna jambo la kumshinda Mungu iwe case ya bailojia, mazingira au spiritual.
katika sehemu iliyokosea ni kumpa simu
mamaaa weeweee simu ni hatari kwa watoto wa shule usimrudishie kabisa
pili tatizo lako lipo kwenye malezi unamdekeza sana huyo mtoto
hivi kweli mtoto akujibu jibu hilo kama majibu ya hapa jf ambapo mara nyingi member akijibu mods wanaanza kumuwinda akikosea tena anapigwa ban??
nitampenda mwanangu ila hatakaa anijibu hivyo kwa msaada wa mungu
ingia chumbani muombee huyo mwanao lakini pili kufaulu midterm test ndo unampa simu?.?????
je ajifaulu necta???si utampa gari aende nalo club na wala usimuulize??
kwa kuwa sio mwanao haimaanishi usimchape na kumuonya vikali kwa adhabu mbalimbali hata biblia inasema hivyo