Jinsi ya kukabiliana na uchovu wa Jumatatu (Monday Blues)

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
1. Tambua tatizo

Kama unapata tatizo la 'monday blues' kila wiki, ina maana hilo si tatizo la kupuuzia. Ni dalili kuwa hufurahii kazi yako na unahitaji kulitatua au kutafuta kazi nyingine.

2. Jiandae kwa ajili ya Jumatatu kuanzia Ijumaa

Jumatatu inakuwa changamoto zaidi kama kuna kazi zilizolundikana kutokea wiki iliyopita na kwa wengine huwa changamoto kurudi tena katika hali ya utendaji kazi.

Kuepuka hili ni vema kufanya kazi zisizokupendeza sana mwisho wa wiki ili uanze wiki kwa uchangamfu. Jipange vizuri kwa ajili ya wiki mpya na hutopata tatizo la uchovu na uvivu jumatatu.

3. Andaa orodha ya vitu vinavyokufurahisha

Huwa tunapendelea kuangalia zaidi vitu vinavyotusumbua badala ya vile vya kufurahisha. Siku ya jumapili andika vitu vitatu vinavyokufurahisha kazini na isome ukifika tu ofisini jumatatu. Itakupa furaha na nguvu mpya kwa siku nzima.

4. Jiachie siku za wikiendi

Kama kuna uwezekano epuka kufuatilia mambo ya kazi siku za wikiendi. Weka mipaka kati ya kazi na muda binafsi kwani itakusaidia sana. Ukiondoka ofisini Ijumaa, acha mambo ya kazi hapo na ufurahie wikiendi ili ukirudi ofisini uwe na shauku ya kazi.

5. Pata usingizi wa kutosha na uamke mapema

Inashauriwa kulala mapema siku ya jumapili ili uamke fresh na tayari kuianza kazi. Pia ni vema kuamka dakika 15 au 30 mapema zaidi siku ya jumatatu ili upate muda kwa ajili yako na usijihisi kubanwa na kazi na pia kuweza kupata kifungua kinywa kwa raha.

6. Vaa kitanashati.

Mavazi yanaweza kubadili 'mood' yako nzima. Ukivaa vema na kujiona umependeza, utaweza kuwa na nguvu, ujasiri na kujiona na uwezo wa ziada wa kufanya kazi.

7. Kuwa na mawazo chanya

Anza wiki kwa mawazo chanya na hali ya shukurani kwa vitu vyote vinavyokuzunguka. Ikiwezekana sikiliza muziki uupendao zaidi na epuka kulalamika ofisini.

8. Mfurahishe mtu mwingine

Mfanye mtu mwingine awe na furaha. Weka nia ya kufanya kitu cha kufurahisha kwa ajili ya mtu kila Jumatatu asubuhi. Hii itanyanyua 'mood' yako na pia kufanya eneo la kazi liwe na hali ya upendo na furaha hivyo kunyanyua morali ya kazi.

9. Fanya ratiba yako ya Jumatatu iwe nyepesi

Kama ilivyosemwa kwenye point namba mbili, ni vema usiwe na mzigo mkubwa jumatatu. Kama kuna mikutano ni vma ipangwe jumanne au jumatano. Hii itasaidia kwenda kazini jumatatu na wepesi.

10. Furahi Kazini

Punguza tension kazini kwa kuongelea wikiendi na wafanyakazi wenza, kufanya vitu vinavyokufurhisha. Hii itasaidia kusogeza muda na kufanya kazi ziende kiurahisi.

11. Kuwa na mpango baada ya kazi

Kuwa na mpango baada ya kazi kutafanya uone kuwa siku yako si mbaya kwani kitu kizuri kinatarajiwa mwishoni. Yaweza kuwa kutoka na marafiki, kuogelea, kupika chakula ukipendacho zaidi n.k
 
Namba 6 nakubaliana na wewe 100%.
Huwa nikivaa kinadhifu, basi Jumatatu huwa naamka niko na nguvu mpya.
Na ndio maana huwa napenda kama nuna nguo mpya huwa naivaa Jumatatu tu
 
Back
Top Bottom