LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,943
- 37,837
Ndio kwanza nimemaliza kujifunza kuhusu AINA MBALIMBALI ZA TUNGURI NA MATUMIZI YAKE..Kuna zaidi ya tunguri elfu saba, na kila moja ina matumizi yake na nguvu zake.... Lilikuwa somo refu na gumu sana... Nikiwa katikati ya somo la TUNGURI, mwalimu wangu aliniambia kitu kimoja ambacho nimeona ni vyema nikaja kushare nanyi hapa JF. Nacho ni kuhusu WATU WASIO WEZA KUDHURIWA NA UCHAWI...
Bila shaka umewahi kusikia kuhusu watu ambao hawawezi kudhuriwa na nguvu za kichawi. Wafuatao ni miongoni mwa watu wasio weza kudhuriwa na nguvu za kichawi.
1. Watu walio okoka ( KIUKWELI UKWELI, SIO WALE WASANII )
2. Vichaa....
3. Ni kundi la watu ambao si wachamungu sana, ila wao wamezaliwa wakiwa na karama hiyo ya kutokudhuriwa na uchawi wa aina yoyote ile..
KWANINI WATU HAWA HAWAWEZI KUDHURIWA NA UCHAWI ? ; Ni somo refu sana, nitalieleza siku nyingine. Leo nina taka nieleze jinsi ya kujitambua kama hauwezi kudhuriwa na nguvu za kichawi.
UNATAKA KUJUA KAMA HAUWEZI KUDHURIWA NA NGUVU ZA KICHAWI....
Kuna njia moja tu na pekee ya kufahamu kwamba wewe hauwezi kudhuriwa na uchawi..Nayo ni KUJARIBU KUFANYA UCHAWI WA AINA YOYOTE ILE IWE NI WA MAPENZI AU JAMBO LOLOTE LILE ( Mara nyingi kipimo cha uchawi wa mapenzi hutumika kwa sababu uchawi wa mapenzi hauna madhara makubwa kama uchawi mwingine )
Endapo utafanya uchawi juu ya jambo fulani halafu jambo hilo lisifanikiwe, basi jua wewe una nguvu ambazo zipo juu ya nguvu za kichawi, uchawi hauwezi kukusaidia, wala huwezi kukudhuru... Ili uchawi uweze kukudhuru ni lazima uwe na nguvu ndogo kuliko uchawi, vivyo hivyo ili uchawi uweze kukusaidia ni lazima wewe mwenyewe kwanza uwe na nguvu ndogo kuliko uchawi. Kama nguvu zako ni kubwa kuliko uchawi, basi uchawi hauwezi kukusaidia wala kukudhuru....
Hujawahi kujiuliza kwanini watu wengine wanafanikiwa sana kwa kutumia uchawi, na wengine hawafanikiwi kabisa pamoja na kutembea kwa waganga na waganga ? Jibu ni kwamba watu hawa wana nguvu kubwa kuliko uchawi , tatizo ni kwamba hawajai tambua nguvu hiyo...
WHAT SHOULD BE DONE : Ukishajigundua hivyo, achana kabisa na mambo ya kwenda kwa wachawi, ongeza bidii katika shuguli zako, mtegemeze zaidi Mungu na utafanikiwa sana....
WISHIN YOU A HAPPY 2014