Jinsi ya kujua kama mmewe/mchumba anachepuka

Selwa

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
572
577
Juzi nilikuwa na maongezi marefu na rafiki yangu mmoja. Yeye na mchumba wake walikuwa wafunge ndoa mwezi huu ila wameachana na nashangaa yeye kuniambia hakujua kama mchumba wake alikuwa anachepuka muda wote wako pamoja. wanawake na nyie inabidi muwe makini sasa huwezi kua na mtu miaka 3 hujui kama anachepuka. hebu niwape vionjo vya mtu anaechepuka ili msipoteze mda wenu ila. kesho ntaleta mbinu za kujua mwanamke anaechepuka
1. kama unahisi kama mwenza wako anachepuka. anachepuka. hisia zetu hazidanganyi hata siku moja.
2. anatoka zaidi siku hizi, yuko na marafiki kwa sana.
3. amekiwa mbinafsi anajijali yeye zaidi yani anajiweka yeye kwanza kutojali mahitaji yako
4. ukaribu kati yenu umepungua
5. mitandaoni anajifanya bonge la single boy hahaaha hii siiijui kwanini dada zangu hamshtuki
6. kawa msiri kupindukia. mipango yake hasemi simu zina password mia anaficha mambo yake.
7. marafiki zake wakianza kukutongoza. iko hivi, jamaa asipoheshimu uhusiano wake majamaa wenzake nao hawataheshimu mahusiano yenu maana wanajua hapo jamaa anapita tu.
ila ni muhimu utambue. kila mwanaume anachepuka. tofauti ni anaekupenda akichepuka hautajua. asiekupenda utaona dalili zote na hatajali kukuumiza.
 
Sa utafanyaje? Unaweza jipa shinikizo la damu mapemaaa. Mwanaume kama ananijali na anaonesha upendo, hanikosei heshima ishu ya mchepuko haiwezi niumiza akili. Ni kumuombea tu Mungu aepushe uwepo wa hiyo michepuko na amlinde.
Ntaachana na wa ngapi kisa michepuko?
Huwezi kumwambia mtu unayempenda achepuke....hamna moyo wa namna hiyo unless uwe kwake kwa maslahi sio mapenzi
 
Huwezi kumwambia mtu unayempenda achepuke....hamna moyo wa namna hiyo unless uwe kwake kwa maslahi sio mapenzi
Hamna mtu anaefurahia mwenzie achepuke... Nnachosema ni kwamba ni kuombea tu ikitokea awe na akili ya kutumia kinga na sio kuleta magonjwa. Wanaume wengi saana wanachepuka na wengine wanafanya kwa siri kubwa... The fact kwamba humuoni au haumuhisi kuchepuka haimaanishi kwamba hachepuki. Ishu ya michepuko ishakua janga!
 
Hamna mtu anaefurahia mwenzie achepuke... Nnachosema ni kwamba ni kuombea tu ikitokea awe na akili ya kutumia kinga na sio kuleta magonjwa. Wanaume wengi saana wanachepuka na wengine wanafanya kwa siri kubwa... The fact kwamba humuoni au haumuhisi kuchepuka haimaanishi kwamba hachepuki. Ishu ya michepuko ishakua janga!
The prblm unaweza kukuta hata ww mchepuko halaf hujui...
 
Sijawahi kupata presha kwaajili ya michepuko. Km ananipenda na kunijali, basi inatosha kbs. Hayo mengine wala sijali.
 
Duuh, huu msemo wa "kila mwanaume anachepuka" ulitoka wapi? Au siku izi watu wanafanyaga sensa ya michepuko!!
Na wakichepuka wanachepuka na nani kama sio wanawake?
Je hao wanawake hawana wapenzi?
Hii dunia kweli duara.
 
Mimi michepuko wala hainiumizi kichwa!!!
Hongera mwanamke una akili nyingi!
Mwanaume aliundwa kwa ajili ya kumiliki wanawake zaidi ya mmoja ndo maana ni vigumu mno kwa mwanaume kuwa na mwanamke mmoja!

Sheria za kiimani zinawabana lakini wanashindwa na kujikuta wameanguka tena na tena na tena!
Kama kuna mwanamke haamini hili basi na akae hivyo tu.
 
utaishi maisha marefu sana,ukiwa na moyo wa namna hii,kuna muda wanawake huwa mnahofia sana vitu kuzidi hata uhalisia wake,yawezekana hata mumeo hachepuki kiivyo ila kwa kuwa una wasiwasi unaanza kujitesa mwenyewe
Cha kufanya ni kumwambia tu ajali afya zetu...
 
Back
Top Bottom