Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,773
Wengine mnafahamu kuwa ulaji wa vyakula vya wanga kiwango cha sukari katika mwili kinaongezeka. Kama mwili unazalisha insulin vizuri chembe hai zinauwezo wa kuchukua sukari hii na kuigeuza kua nguvu inahohitajika kwa shughuli za kila siku. Kama mwili hauna uwezo wa kuzalisha insulini vizuri sukari hii inabaki kwenye mzunguko wa damu na mwili unakosa nguvu, unajisikia kuchoka kila saa. Hii ni dalili ya kisukari (diabetes). Sukari inayozidi baada ya matumizi ya chembehai inahifadhiwa kama glycogen katika ini na misuli ya mwili, pia kwenye damu (lipids).
Kwa mtu mwenye afya njema na mwili unaweza kujiregulate wenyewe, ukichelewa kupata chakula uzalishaji wa insulin unasimama na mwili unatumia sukari iliyohifadhiwa kwenye ini, damu na misuli. Na baada ya kula chakula tu sukari ikizidi mwili unarelease insulin kurekebisha kiwango cha chakula.
Tunashauriwa kufanya mazoezi angalau kuweza kuunguza sukari iliyozidi na kuhifadhiwa kwenye ini, damu na misuli. Kuna wanaokwenda hospitali na kuambiwa una fatty liver au mafuta mengi kwenye ini, mafuta yanayohifadhiwa kwenye misuli ndiyo yanaleta beer belly, nyama uzembe, na vingine vingi.
Madhara makubwa zaidi ni kuwa ni stroke, tatizo la stroke lilikua na la watu wa makamo zamani, vijana wengi siku hizi wanapata stroke umri wa miaka kuanzia 30. Kama ujuavyo stroke ni ajali mbaya ambayo ikikunusuru na kifo inaweza kukuachia ulemavu wa maisha.
Stroke mara nyingi inasababishwa na kuziba ghafla ya damu inayopeleka damu kwenye ubongo (arteries) kuziba. Aina nyingine ya stroke ni kupasuka kwa arteries na kusababisha damu kumwagika kwenye ubongo. Yote haya yanapelekea ubongo kukosa damu kwa muda ambayo ndiyo njia pekee inayopekeleka oxygen na chakuka kwenyeubongo. Katika kila msukumo wa damu mahitahi ya ubongo 20%.
Moja ya vitu vinavyochangia stroke ni diabetes, high blood pressure, unywaji wa pombe kupitiliza, uvutaji wa sigara na high level of cholesterol kwenye damu.
Mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na kufanya healthy check kila mara kunaweza kutusaidia kuepukana na haya.
Kwa kuanzia unaweza kuongeza ulaji wa maboga na ndizi za kijani na kupunguza ulaji wa wali ugali, viazi na mihogo. Jinsi ya kutaarisha chakula pia, ndizi za kuchemsha, samaki wa kuoka na salad, au vipade vya maboga vya kuoka, salad na cabage la kusteam. Ni ushauri tu.