Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 282
- 272
Utengenezaji wa brand umebadilika sana kulinganisha na hali ilivyokuwa zamani,na hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na ufanyikaji wa dunia kuwa kijiji hivyo hali hii imepelekea hadi mfumo wa biashara nao kuhamia huko, mauzo yanayofanyika nje ya mitandao asilimia kubwa kwa sasa ni matokeo ya ushawishi ama kujitangaza vizuri kupitia mitandao ya kijamii .
Japokuwa tumekuwa tukiyaona na kuyashuhudia mabadiliko haya , bado hatujaweka mkazo mkubwa katika soko hili la kujitangaza online, mfano serikali inasema kuboresha vifungashio na muonekano wake hii inamaanisha lazima na soko la online( Mtandaoni) Uliangalie kama unataka biashara yako itoke sababu mtandao unafanya kazi dunia nzima na hicho ndicho kilichoufanya upate mwamko na kasi kubwa sababu unapokuwa kwenye mtandao unauwezo wa kujitangaza na dunia nzima ikakuona sasa ishu tuliyokuwa nayo ni kwamba kila kitu tunatengeneza chini ya kiwango lakini tunahitaji tuuze kwa kiwango cha juu.
Mfano: Huwa mara nyingi nasema kufanikiwa ama kufeli kwa biashara yako kunachangiwa ama kunatengenezwa na uwezo wa brand yako, taarifa ilionyesha tumepunguza mapato ya nje kwa billion kama 3 hivi ile ilikuwa ni kutokana na brand kuwa chini ya kiwango kama unatengeneza vizuri na umejitangaza vizuri huwezi kushusha mauzo kwa kiwango hicho hata kama kodi,makato yakiongezeka ukiwa umejibrand vizuri unauwezo wa kulifanya soko likufate, mfano kama wewe ni muuza maandazi mzuri na unauza kila siku maandazi sh.100 unauwezo kuwaambia wateja wako unga wa ngano umepanda maandazi sasa hivi ni 150 na watu wakakubali bila shida lakini kama wewe sio kiongozi ukipandisha inamaana watu watakuhama tu sababu wewe sio kiongozi na brand yako haina huo uwezo.
Kwa hiyo mtandao kwa sasa unanguvu kubwa sana katika mauzo ya biashara yoyote watanzania milioni 20, wanatumia mtandao hivyo inamaanishau ukitumia mbinu na njia sahihi za kujitangaza basi unaweza kuwafikia watu milioni 20 wanaotumia mtandao,sasa ishu inakuja haya mambo huku tunayapokea na hakuna mtu wa kutuongoza hivyo watu wanajifanyia fanyia tu bila kuwa na muongozo sahihi wa jinsi ya kufanya na hii ni tatizo kubwa sana, utakuta brand inauwezo wa kuwa kubwa na kuwafikia vizuri watu wake lakini haitumii ipasavyo mtandao husika ama maudhui tofauti na kile inachokifanya hii inapelekea wateja wengi kuishia njiani na kutokufikia kwenye ununuzi.
Twende mbele turudi nyuma mteja haumpati kwa kumlazimisha, ishu ambayo huwa wafanyabiasharana wajasiriamali wanasahau ni kuwa mteja haumlazimishi kununua kwako ila unamshawishi tu, wewe utatumia weledi na nguvu ili kumpata ila yeye atatumia uasili wake tu aidha kukukubali ama kukukataa.kwa hiyo ushawishi wako wote unapoufanya ni lazima uufanye ukitambua unaitafuta asili ya mteja, hili limekuwa tatizo kwa biashara nyingi sababu wamekuwa wakitumia komand( Ulazima) hadi kwa wateja wao yaani wanaweza wakafanya hata tangazo ambalo halina uhalisia ilimradi tu wao wanataka bidhaa zao zieleweke lakini matangazo mengi yenye mvuto na yanayopenda ama kusikilizwa huwa ni yale yaliyoingiza uhalisia ndani yake sasa hapo ndio inakuja kujitathmini tangazo langu lina uhalisia ndani yake ama nnalazimisha watu kutumia bidhaa/huduma yangu.
(Tangazo hadi mtoto analikariri sio kama ni mteja wako ila lina uhalisia na anaweza kuwa balozi mzuri kukumbusha kuhusu tangazo lako mara nyingi awezavyo)
Sasa basi ni lazima kaka mfanyabiashara ama mjasiriamali kuitambua nguvu ya mtandao katika kujitangaza na usifanye kama ni kitu cha kupita ama kujifurahisha unapotaka kufanikisha hilo kwa ufasaha ni lazima uifanye kama sehemu ya masoko kwako na biashara yako.
Baadhi ya vitu ambavyo unatakiwa utambue kama mfanyabiashara ama mjasiriamali.
Kitu ambacho unatakiwa kutambua kila sehemu kumekuwa na makanjanja hivyo unapoamua kutafuta watu ama sehemu za kujitangaza hakikisha ni sehemu ambazo zinaaminika pia process ya kutengeneza brand sio ya siku moja ama wiki hivyo tumia mda mwingi kufuata kanuni zake
Muda :
Muda mzuri wa kutuma matangazo yako kupitia mitandao ya kijamii nitakuandikia baadhi tu.

- Mtandao ni sehemu ya kutafuta masoko
- Tengeneza jina halisi
- Muda
- Ongeza shea za masoko
- Panua soko lako
- Miliki aina.
Kitu ambacho unatakiwa kutambua kila sehemu kumekuwa na makanjanja hivyo unapoamua kutafuta watu ama sehemu za kujitangaza hakikisha ni sehemu ambazo zinaaminika pia process ya kutengeneza brand sio ya siku moja ama wiki hivyo tumia mda mwingi kufuata kanuni zake
- Muonekano
- Picha ( Image)
- Maudhui
- Tengeneza line/ Focus
Muda :
Muda mzuri wa kutuma matangazo yako kupitia mitandao ya kijamii nitakuandikia baadhi tu.
- Facebook = 7 mchana - 10 mchana
- Linkeldin = 11 - 12 jioni
- Instagram 11 - 12 jioni ( 10 alfajir)
- Pinterest - 2- 5 usiku
- Google+ = 3 - 5 usiku