Jinsi ya kuhamisha Mshahara

Kamera

Senior Member
Sep 27, 2018
159
250
Habari wanajamii, mimi nilihama mwezi wa tatu mwaka huu kutoka halmashauri A kwenda B ndani ya mkoa huohuo na uhamisho wangu ulishughulikiwa na Katibu Tawala Mkoa.

Nimefatilia kuhamisha mshahara bila mafanikio, afisa utumishi wa kule nilikotoka aliskani taarifa na kuzituma utumishi na nlipokuwa naangalia kwenye watumishi portal nlikuwa naona kwamba mabadiliko tarajiwa ni transfer na nipo pending.

Mnamo mwezi wa sita nkapatwa na shida ya kunilazimu nipate mkopo bank, nkaenda kwa Afisa utumishi wangu wa sasa wa Halmashauri Bakasema hawezi nisaidia maana system inaonyesha bado nipo Halmashauri A. Hivyo nirudi kule ndo wanihamishie mshahara.

Kule A nao wakasema wameshafanya kazi yao bado tu utumishi waconfem. Ikabidi wanishauri nikopee kulekule ili waingizw makato kwenye mfumo nami nikakubali nikafanya hvo.

Sasa huyu Afisa Utumishi wangu wa halmashauri B anataka niamishe mshahara uhamie huku, kuangalia kwenye mfumo sasa hv ile transfer na pending haipo tena yaani kama hakuna kitu kinachosubiri ipo kawaida ba mshahara haujahama na wale wa halmashauri ya A wanasema wameshafanya kazi yao.

Ni usumbufu na hata sijui la kufanya, wenye msaada wa mawazo naomba mnishauri. Japo mshahara napata ila sina amani salary slip kusoma bado nipo kulekule miez 7 sasa.
 

Mr Adam Gella

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
1,327
2,000
Tatizo hapo ni Approver!wa utumishi anaeconfirm uhamaji wa mshahara huo...Halmashauri A anaweza hamisha ila approver asipoapprove bado wa B hatoweza fanya lolote!Hilo hata mimi linanicost saivi!
 

Kamera

Senior Member
Sep 27, 2018
159
250
Tatizo hapo ni Approver!wa utumishi anaeconfirm uhamaji wa mshahara huo...Halmashauri A anaweza hamisha ila approver asipoapprove bado wa B hatoweza fanya lolote!Hilo hata mimi linanicost saivi!

Una muda gani tangu umehama?
 

JAY MTAALAM

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
1,592
2,000
Tafadhali wasiliana na wahusika katika halmashauri uliyopo watakupa mwongozo kamili,kuwa na imani tu! Mambo yatakaa sawa.
Kazi njema.
 

2699s

Member
Aug 30, 2017
32
95
Mkuu nimeishafanya mawasiliano na nilikotoka wanasema wameishahamisha ila huku nilikohamia ndo nako bado haujasoma na mashaka je kama kule wanadai wameishatuma haiwezi kusababisha unakosa mshahara. Niliambiwa haujawa approved zaidi ya mwezi kweli utumishi wanachelewa hivo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom