Binafsi sijawahi kusikia chuo wanachofundisha kozi hiyo,isipokuwa watu wengi hujifunza kwa watu wenye ofisi zao na uzoefu katka kazi hiyo, mimi binafsi niemwahi kufundisha watu ktk ofisi yangu siku za nyuma na nikagundua vitu muhimu viwili,kwanza unaweza kumfundisha mtu kwa kumpa lectures na akwa anachuka hata notes lakini mwisho wa siku akashindwa kufanya kazi, pili ukamchukua mtu hata shule hajasoma kabisa lakini ukakaa nae ofissini baada ya miezi michache utakuta anajua kuflash na kutengeneza vizuri sana! sasa hapo kama ni mtu mkomaaji kwenye forums na ameisha jifunza kazi kwa vitendo basi atakuwa mtalaam safi kabisa!