Habari wana JF
mwaka 2013 unaisha je umewahi kutathimini ni mambo mangapi umefanikiwa?
mangapi umeshindwa? kwa nini?naomba niwashirikishe uzoefu wangu ktk
maisha.
Jua hv hakuna jambo lolote linalotokea bila KUPANGA.kupanga ni kuamua
unataka ufanye nini....na kama hujapanga ni vigumu kujua umefanikiwa au
umeshindwa..kupanga kumenisaidia toka nikiwa olevel mpaka nikamaliza
vyuo vikuu.na kufanikiwa ktk maisha yani Elimu,Kiuchumi,Familia nk.sasa
narudi kwenye kiini cha uzi huu.tunapoingia mwaka 2014 fanya yafuatayo
kama una lengo la kufanikiwa ktk maisha yako
1.PANGA
Hakikisha umepanga mambo ya kufanya hapa uwe na diary au note book ili
uandike usije sahau kuna mipango ya mda mfupi hii inafanyika ndani ya
mwaka na ya mda mrefu zaidi ya mwaka mfano kujenga kuoa nk
2.AMINI
Hakikisha unaamini kwamba utayafanikisha malengo yako kwa 100%
3.MUDA
Hakikisha unaweka mda wa kukamilisha malengo yango kumbuka wakati ni
ukuta ukipita umepita haujirudii
4.TATHMINI(evaluation)
hakikisha unacheki mara kwa mara kama umefanya yale uliyopanga ainisha
vikwazo kisha amua kuvikabili sio kuacha au kukubali kushindwa
5.USIKATE TAMAA
Hakikisha unazikabili changamoto sio kukimbia
kwa sababu utakuwa umejifunza makosa hivyo utakaporudia utafanya vizuri
sana jua hata waliotengeneza ndege magari nk walikosea walirudia sana
mpaka wakafanikiwa
Samahani ntarudi badaye